Kweli mkapa unawashangaa wazanzibar kukubali umoja wa kitaifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli mkapa unawashangaa wazanzibar kukubali umoja wa kitaifa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ICHONDI, Oct 7, 2010.

 1. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Gazeti moja la kila siku limeandika leo kuwa Mkapa amewashangaa Wazanzibari kukubali kuunda serekali ya mseto ya umoja wa kitaifa. Alikuwa anahojiwa na BBC.

  Binafsi nimeshangazwa na kauli ya mheshimiwa Mkapa, sikutarajia kama kauli hiyo imetoka kwenye mdomo wa mwanadiplomasia ambaye Tanzania inajivunia kuwa miongoni mwa wananchi wake. Ni mheshimiwa Mkapa ambaye alihusika kusuluhisha mgogoro wa Kenya mambo yalipochacha. Lakini mbaya sana ni Mkapa huyu huyu aliyeshuhudia mauaji ya kisiasa kule Pemba na matokeo yake ni kuvurugika kwa mfumo wa kawaida wa maisha wa wananchi wa Pemba kwa wengi wao kukimbilia uhamishoni na kuwa wakimbizi katika nchi jirana. Chini ya utawala wake wa kimabavu alitumia jeshi kuua, na kama hilo halikuwa jambo baya, akasema ni watu wawili watatu tu wamekufa, kana kwamba ni vifaranga vya kuku vimekufa- rejea mahojiano yake na idhaa ya BBC akiwa London, na alivyoongea kwa hasira na ubabe

  Leo hii anathubutu kuwashangaa Wazanzibari kukubali kuzika uhasama wao na kuunda umoja wa kitaifa. Jambo ambalo yeye , Salmin Amour, JK walishindwa kulisuluhisha, leo hii Karume na Seif wameileta Zanzibar pamoja anawashangaa.

  Hivi huyu Mkapa ni mtu wa namna gani. Kwanza ameshachafuka sana mbele ya jamii, ndiye yeye kwa ubinafsi wake aliamua kumpigia chapua JK awe raisi baada yake dakika za mwisho ili kulinda utajiri wake alioupata kwa njia za kiporaji. Akaamua kwa makusudi kuwa bora kuepusha ubawa wake, na kutuletea raisi aliyevuruga nchi na kuifanya kuwa ya hovyo na ya Kiswahili. Mkapa huyu huyu anatuhumiwa kwa mambo mbalimbali ya kifisadi, na mawaziri wake wamefikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka. Ni yeye ambaye chini ya utawala wale ulishuhudia wizi mkubwa wa fedha –EPA za wavuja jasho wa nchi hii zikikwapuliwa na kutumika kwa njia isiyo na maslahi kwa jamii. Ni yeye pia alishinikiza mkataba wa kinyonyaji wa Net Group Solution na Tanesco ili kumpa ulaji shemeji yake. Ni yeye aliyebariki mikataba mibovu ya Meremeta, Alex Sterwart etc ambayo imeifilisi nchi hii. Huyu Mkapa hana soni wala majuto, hana huruma, na wala hajawahi kuwaomba radhi wazanzibari, Wapemba kwa vitendo vya kikatili na kinyama walivyofanyiwa ambavyo havijawahi kufanyiwa kundi lolote katika nchi hii.

  Najiuliza, hiyo jeuri ya kusema kuwa anashangaa mfumo wa umoja wa kitaifa ameitoa wapi. Je anataka waendelee kuuana? Eti anasema katika enzi zangu, tulikuwa tunashinda kura, hivi kweli Mkapa ambaye ni mkristo anathubutu kusema kitu kama hicho? Anathubutu kusema mwaka 1995 alimshinda Mrema, wakati anajua uchaguzi ulivurugwa makusudi na usalama wa taifa ili ashinde, anajua alivyokuwa hakubaliki, anajua alivyomfanyia rafu JK kwa msaada wa Julius Nyerere, ili ashinde, anakumbuka alivyoshikwa mkono na mwalimu Nyerere latika kampeni na kuambulia asilimia 69 ya kura hata baada ya kuchakachuliwa?

  Watanzania wenzetu, tumpuuze huyu bwana, ni mtu kichwa ngumu na anayedhani kuwa amesoma na akili kuliko watanzania wote. Dharau na kiburi chake ndio umetufikisha hapa. Labda kwa kumkumbusha tu, japo picha ya 1995 na ya sasa zinafanana kwa mgombea wa Chadema kuvutia watu wengi kama ilivyokuwa kwa Mrema na kubebwa, mazingira ya leo ni tofauti na wakati ule. Wapiga kura wa leo si wa 95, elimu ya urai ni pana na si kama 95, watu wa leo wanajua haki yao na umuhimu wa kura kuliko 95, na mbaya zaidi, watu wanajua mbinu chafu za kuchakachua, si kama 95 ambapo hata mawakala wa vyama hawakuwepo vituoni wakati kura zinahesabiwa. Nilidhani kwa mtu mbabe na msomi kama Mkapa angetambua hilo. Limempita kwa kuwa ushabiki wake wa kisiasa ni mkubwa kuliko utashi wake wa kufikiri--
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Umeandika hii ndefu sana lakini hat a Mimi nashangaa serikali ya mseto ijayo..natafiti Kama muungano bado utakuwa valid?anyway sijui lakini nina Mashaka mazito sana
   
Loading...