Kweli mh Pinda umetangaza kuwapa kazi ya sensa walimu na watumishi wa umma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli mh Pinda umetangaza kuwapa kazi ya sensa walimu na watumishi wa umma?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Mwigamba son, Jun 30, 2012.

 1. Mwigamba son

  Mwigamba son Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ama kweli mwenye nacho ataongezewa na asiyenacho atanyang'anywa hata kile kidogo alichonacho hivi karibuni mh Pinda wakati akisoma bajeti ya wizara yake alisema zoezi la sensa litafanywa na walim pamoja na watumishi wengine wa umma.Jambo hili naona kama ni mwiba mkali kwa vijana waliotoka vyuoni wasio na ajira. kwani wangepewa fursa hiyo pengine wangejipatia mitaji kupitia zoezi hilo la sensa. Kitendo cha kuwapa walim na watumish wengine wa umma ajira hii wakati tayari wao wana ajira ni tusi kwangu mie kijana nisiye na ajira. Sasa nimeamini ccm haina sera yoyote ya kuongeza ajira kwa vijana.
  Kama ukosefu wa ajira kwa vijana ungekuwa uko kwenye vichwa vya watawala basi vijana wangekuwa wa kwanza kufikiliwa panapo fursa kama hizi. hivyo serikali iliyopo madarakani nadiliki kusema haina nia ya dhati ya kutatua taizo la ajira kwa vijana.Kweli Mh Pinda unatunyima vijana wa kitanzania tusio na kazi zoezi la sensa na kuwapa watumishi wa umma ambao tayari wana ajira na mpaka mmewalazimisha walimu kubadili mihula mashuleni.hivi kweli vijana hatuwezi kulifanya zoezi hili kikamilifu mbona mnatupuuza mheshimiwa
   
 2. H

  Henry Philip Senior Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 29, 2008
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa nini unamuita muheshimiwa, angekuwa muheshimiwa asingewanyima hako ka-ajira na kuwapa wenye afadhali.
   
 3. Msambaa mkweli

  Msambaa mkweli Senior Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 193
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mwalimu wenyewe hawataki kwani wamebana pesa za malipo (watalipa posho), bado kitakacho tokea ni usumbufu, kwani wanataka kutishia ajira zao pale ambapo kitakuwa hakieleweki.
   
 4. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kweli umetoa point ya maana sana. Serikali ya magamba bwana!!!
   
 5. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  yaan nakaribia kulia.
   
 6. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,867
  Likes Received: 1,149
  Trophy Points: 280
  Si uongo hawana nia nzuri na Vijana wa Tanzania wasiokuwa na Ajira. Vijana wana nguvu na wangeweza zoezi hili bila shaka. usisikie wakiongea hadi wanatoka povu kwamba ooooh vijana tutawapa ajira. Jaribu kwenda hata wilayani unawaambiwa kama huna CV ya Ualimu hii kazi hupewi.
  Waalimu wafunge shule wakafanye Sensa ambayo vijana wanaweza kwao ni sawa tu. ''Mwenye Nacho huongezewa na Asiykuwanacho hapewi hata kama anastahili kwa kuwa hana mtetezi''.
   
 7. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Ameikumbuka tamthiliya ya "NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE", lol. Inaonekana vijana wakipewa hii kazi watafanya kama Ngoswe, lol
   
 8. Mwigamba son

  Mwigamba son Member

  #8
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  si kweli kwamba vijana ni watovu wa nidhamu kazini Ngoswe alikuwa ni mdhaifu wa mapenzi na mlimbukeni wa mapenzi kijana wa leo anafaham mapenzi ni nini na hachanganyi kazi na mapenzi na ndio maana wanaimudu mitandao ya mapenzi mikubwa bila wenzi wao kujua wanachofanya ni kuheshimu ratiba na kuwapanga. ndio maana wameletewa kauli mbiu ya tuko wangapi tulizana hivyo mapenzi kwa sasa hayana nguvu ya kumchangaya kijana. tupo kikazi zaidi
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Liwalo na liwe.
   
 10. b

  bshayo Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Lakini vijana wapo kwenye kundi la walimu na watumishi wengine.
   
Loading...