Kweli, Maiti Haina Haki wala Rafiki:

BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
6,033
3,944
Jana tarehe 4 Juni kwenye gazeti kubwa la Mwananchi kuna habari za kusikitisha kuhusu vifo vya Wanawake Wawili vilivyotokana na Watu walio Karibu Yao.

Kilichonisikitisha zaidi kwenye ni jinsi Vifo hivyo vinavyoshughulikiwa tofauti na vyombo vyetu vya Usalama na vyombo vya habari.

Katika kifo cha kwanza marehemu, anayeshukiwa kufanya mauaji hayo, ndugu na hata marafi wa marehemu wametajwa kwa majina yao wakizungumzia kile wanachodhani kuwa ndicho kilichosababisha mauaji hayo!

Huku kwenye Msiba wa pili uliotokea Kinyerezi Dar es Salaam hali ni tofauti kabisa.
Zaidi ya jina la Marehemu, hakuna jina lingine lililotajwa. Sio la Mshukiwa wa Mauaji hayo wala la rafiki na majirani wa marehemu, kwa maelezo tu kwamba 'hakutajwa jina'!
Nimeshangaa sana hata Mkuu wa Kituo husika mauaji hayo yalipo aliponukuliwa akisema 'anayeshukiwa kwa mauaji hayo hajatajwa jina'...lakini anajulikana kuwa ni Shemeji wa marehemu!...ila jina ndio halitajwi!

Nikakumbuka kwamba habari hii ilipogonga kurasa za habari mara ya kwanzailieleza kuwa familia ya upande wa mshukuwa wa mauaji, wifi mtu, ilikuwa inafanya jitihada za kuficha jina lake na hata kuzuia familia ya marehemu kushiriki msiba ili kujua kinachoendelea!

Unapoisoma habari ile kwenye gazeti husika unapata ukakasi kwamba sio tu chombo cha Usalama kimehusika katika kuficha jina la mtuhumia na familia yake, tofauti kabisa na yale mauaji ya Iringa ambayo kila kitu kimewekwa Wazi, haya Mauaji ya Kinyerezi hata vyombo vya habari vimetumika katika kuficha jina la mtuhumiwa wa Mauaji, wifi mtu.
Marehemu Mwalimu ana Haki tena hapo??
 
Ungeweka na links basi vinginenevyo na wewe hutoi msaada

Weka habari kamili ya huyo anaefichwa watu waanze kumtaja hapa
Bahati mbaya sana sina utalaamu mzuri wa kuweka links. Samahani sana, ila habari ilo kwenye gazeti la Mwananchi la jana na ninakumbuka kama juzi iliwekwa humu. Ngoja niitafute ingawaje uwezo wangi wa kuweka links ni wa mashaka!
 
Zamani Tanzania ilikuwa na utaratibu wa kisheria wa "Innocent until proven guilty beyond reasonable doubt by a court of law". Utaratibu huo bado uko?
 
Wanaharakati UCHWARA wako wanashughulika na Sabaya naMwendazake. Washukiwa wangekuwa na nasaba na hao ingekuwa twiter, tumekuwa na mihemuko mno watoa maamuzi na watawala wasipokuwa makini watahukumu mengi kwa HISIA na MIHEMUKO
 
Jana tarehe 4 Juni kwenye gazeti kubwa la Mwananchi kuna habari za kusikitisha kuhusu vifo vya Wanawake Wawili vilivyotokana na Watu walio Karibu Yao.

Kilichonisikitisha zaidi kwenye ni jinsi Vifo hivyo vinavyoshughulikiwa tofauti na vyombo vyetu vya Usalama na vyombo vya habari.

Katika kifo cha kwanza marehemu, anayeshukiwa kufanya mauaji hayo, ndugu na hata marafi wa marehemu wametajwa kwa majina yao wakizungumzia kile wanachodhani kuwa ndicho kilichosababisha mauaji hayo!

Huku kwenye Msiba wa pili uliotokea Kinyerezi Dar es Salaam hali ni tofauti kabisa.
Zaidi ya jina la Marehemu, hakuna jina lingine lililotajwa. Sio la Mshukiwa wa Mauaji hayo wala la rafiki na majirani wa marehemu, kwa maelezo tu kwamba 'hakutajwa jina'!
Nimeshangaa sana hata Mkuu wa Kituo husika mauaji hayo yalipo aliponukuliwa akisema 'anayeshukiwa kwa mauaji hayo hajatajwa jina'...lakini anajulikana kuwa ni Shemeji wa marehemu!...ila jina ndio halitajwi!

Nikakumbuka kwamba habari hii ilipogonga kurasa za habari mara ya kwanzailieleza kuwa familia ya upande wa mshukuwa wa mauaji, wifi mtu, ilikuwa inafanya jitihada za kuficha jina lake na hata kuzuia familia ya marehemu kushiriki msiba ili kujua kinachoendelea!

Unapoisoma habari ile kwenye gazeti husika unapata ukakasi kwamba sio tu chombo cha Usalama kimehusika katika kuficha jina la mtuhumia na familia yake, tofauti kabisa na yale mauaji ya Iringa ambayo kila kitu kimewekwa Wazi, haya Mauaji ya Kinyerezi hata vyombo vya habari vimetumika katika kuficha jina la mtuhumiwa wa Mauaji, wifi mtu.
Marehemu Mwalimu ana Haki tena hapo??
Watuhumiwa wote wa mauaji waote wametajwa labda wewe ndio haujui ,aliyeua mwalimu ni binti mdogo wa miaka 22 na picha zake zimo ,social media zina power kuliko hayo magazeti.
 
Back
Top Bottom