Kweli maisha ya Mnyonge hayana hadhi wala haki :Baraza lasema hakuna noma

Mugishagwe

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
300
58
Posted Date::3/8/2008
Baraza lawasafisha madaktari MOI
Na Jackson Odoyo


HATIMA ya madaktari wanne Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) kati ya saba waliotuhumiwa kuhusika na upasuaji tata, itaamriwa na Mkurugenzi wao baada ya kuonekana hawana hatia mbele ya Baraza la Madaktari.


Msajili wa Baraza la Madaktari nchini (MCT) Dk Polloty Luena alisema kwamba amechukua uamuzi huo baada ya kuwasikiliza madaktari wote na kubaini kuwa kuhusika kwa hao wanne katika upasuaji huo kunatokana na sababu za kiutawala wa MOI.


Alisema , hakuona sababu ya kuwafanyia uchunguzi kwani ushahidi wa kimazingira unatosha kumpatia ushahidi juu ya kuhusika kwao katika upasuaji huo.


Hata hivyo hakutaka kuweka bayana juu ya mambo ambayo ameyagundua katika maelezo yao na yaliyoweza kumridhisha mpaka asiwafanyie uchunguzi huo kwa madai kwamba bado ni mapema mno na kwamba watamueleza Mkurugenzi huyo, Profesa Laurent Mseru.



Msajiri huyo alisema kwamba mbali na kuwasikiliza watuhumiwa hao pia alizingatia maelezo yaliyotolewa na uongozi wa MOI na kupitia ripoti ya tume iliyoundwa na Mkurugenzi huyo pamoja na ile iliyoundwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa.


Kuhusu madaktari watatu waliobaki Dk Luena alisema wata fanyiwa uchunguzi wa kina juu ya tuhuma zao kwa sababu walishiriki moja kwa moja katika upasuaji huo .



Madaktari hao waliwafanyia wagonjwa wawili upasuaji kinyume na matatizo yao Novemba mosi mwaka jana katika taasisi hiyo.


Wagonjwa hao ni Emmanuel Didas aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mkuu na hadi sasa bado amelazwa katika taasisi hiyo kwa matibabu zaidi.


Mgonjwa mwingine ni Emmuael Mhagaya aliyefanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa na kwa sasa ni marehem.
 
Sasa mtu anapasuliwa kichwa badala ya mguu na bado wahusika wanaambiwa hawana hatia....

Only in Tanzania
 
Sasa mtu anapasuliwa kichwa badala ya mguu na bado wahusika wanaambiwa hawana hatia....

Only in Tanzania

Ndiyo Masatu .Habari za masiku .Yaani Serikali inaungana na kuua raia wake kwa maamuzi kama haya .Lawama hatuwezi kuziacha Muhimbili pekee bai tutazipeleka wizarani hadi kwa JK .Je angalikuwa ni mtoto wa JK ama kigogo wa CCM kafanyikwa haya kesi hii ingaliishia wapi ?Ama kwa vile wao wana pesa huishia SA na Ulaya kwa matibabu ?
 
Back
Top Bottom