Kweli maisha magumu yametufikisha hapa!?

mjukuum

JF-Expert Member
Dec 8, 2014
5,258
2,840
Jana Nimepanda daladala kutoka Bunju kwenda mawasiliano kufika kituo cha mbuyuni akapanda jamaa mmoja hivi anaonekana mlemavu

Unajua watanzaninia akapanda mlemavu au Mwenye Mtoto hupishwa kwenye kiti kuna watu wakawa wanampisha ili anae Lkn akasema hapana atasimama.

Hali ya hewa Kule ndani ikawa nzito ghafla Baada ya Yule jamaa kupanda gari

Alianza kuomba samahani kwa Sabb anawanukisha mikojo matatizo la kibofu ametoka hospital ili kutafuta hela ili abadirishwe

Najua anawasumbua Lkn umasikini Hata yeye najisikia vibaya kuwasumbua watu Lkn hana namna anaomba hela kiasi cha 3600/=ili ashuke abadilishe akapata hicho kiasi

Akashuka kituo kinaitwa rafia
Aliposhuja Kumbe kuna Dada alimwona asubuhi akiomba hivyo hivyo Ila asbh hakukata kitu watu walimshitukia kuwa wala haumwi Ila kafunga mikojo natembea nayo hii Hali inatuonyesha Nini kweli??
 
Mbona huo mchezo upo kitambo kaka,mi nshakutana na mtu kama huyo zaidi ya mara3 nikiwa natoka tegeta kwenda kariakoo,
Jamaa alikua anapandia pale magomeni hospital anafanya yake halafu anashukia mapipa.
 
Huyo Jamaa wa 3600,watu wamnote tu.
Nimeshakutana naye Morogoro Road kipande cha Rombo-Ubungo Maji.
Nilipomuona tu nilijua huyu msanii licha ya ulemavu wake alionao(kama mguu mfupi mmoja....).
Anachouzi analalamika kuhusu ndugu zake ;
*Amenyanyapaliwa kwa kukosa 3600
Hebu kwa mtu mwenye akili timamu ....ndugu wanaweza kukufukuza home kwa 3600(sawa inawezekana jamii kukosa 3600 ila si kukufukuza tena unaumwa?).
Watu hawakujiongeza wakatoa kuna dada akatoa 2000,jamaa mmoja 2000 akapata zaidi ya 3600.
Sinema aliyoicheza sasa....gari yetu inaenda Kariakoo....amepandia Rombo na pesa anadai ya Hospitali .
Ilipopatikana pesa nyingi tu (kwa maneno yake ya kutuhumu ndugu,mfuko wa mkojo alionao,maneno ya kiimani anayosema kama si mtu wa kujiongeza kwanza unatoa).....gari iko kwenye foleni maeneo ya Ubungo Maji akashuka....hakwenda mbele wala nyuma akasimama kituoni as anasubiri gari lingine.
Tuwe watu wa kujiuliza kwanza Jamani!!!
Huyu mtu wa 3600 yupo sana!!!
 
Mjini mipango.
population yote hii ktk nchi yetu na umaskini unaotuhadaa unafikiri watu wataishi vipi..?
let them play their part but politician they must finish it coz it shame to us.
 
Huyo Jamaa wa 3600,watu wamnote tu.
Nimeshakutana naye Morogoro Road kipande cha Rombo-Ubungo Maji.
Nilipomuona tu nilijua huyu msanii licha ya ulemavu wake alionao(kama mguu mfupi mmoja....).
Anachouzi analalamika kuhusu ndugu zake ;
*Amenyanyapaliwa kwa kukosa 3600
Hebu kwa mtu mwenye akili timamu ....ndugu wanaweza kukufukuza home kwa 3600(sawa inawezekana jamii kukosa 3600 ila si kukufukuza tena unaumwa?).
Watu hawakujiongeza wakatoa kuna dada akatoa 2000,jamaa mmoja 2000 akapata zaidi ya 3600.
Sinema aliyoicheza sasa....gari yetu inaenda Kariakoo....amepandia Rombo na pesa anadai ya Hospitali .
Ilipopatikana pesa nyingi tu (kwa maneno yake ya kutuhumu ndugu,mfuko wa mkojo alionao,maneno ya kiimani anayosema kama si mtu wa kujiongeza kwanza unatoa).....gari iko kwenye foleni maeneo ya Ubungo Maji akashuka....hakwenda mbele wala nyuma akasimama kituoni as anasubiri gari lingine.
Tuwe watu wa kujiuliza kwanza Jamani!!!
Huyu mtu wa 3600 yupo sana!!!

Kama watu walitoa kwa moyo wa kumsaidia wakiwa wamwguswa na shida yake kumbe yeye akiwa na nia ya kutapeli basi dhambi hiyo itaendelea kumtafuna, ipo siku atapata maradhi ya kweli na hakuna atakayekuwa na msaada kwake,

Naamini utapeli wa hivyo na ule wa kutumia vitabu vitakatifu kwa visingizio vya upako na uponyaji vina hatima mbaya mbele ya safari
 
Kuna jamaa alikuwa anapaka unga wa dengu dushe lake akidai kuwa anatokwa na usaha....watu walio na huruma walikuwa wanamsaidia sn. Siku moja alienda kanisa katoliki magomeni kuomna msaada padri akawatuma vijana waende naye kwa mhasibu ili awape hela wamsindikize hospitali. Njian jamaa akawaambia vijana wampe zile hela aende mwenyewe huko hospitali wale vijana wakakataa naye akawaacha hela zikarudi kanisani...maana wangempeleka hospitali angepewa risit ya matibabu. Tuwe makini.
 
Mimi mjini hapa sichangii mtu yoyote au jambo lolote.....hata msiba sichangii mpaka nione maiti......
 
Kuna mmoja alikuwa anashinda kituo cha pale msimbazi pale kariakoo....kutwa nzima ameshika mia mbili akitaka aongezewe ili apate nauli ya kwenda kimara.........
Ukitaka mgombane umuambie apande utamlipia.....
 
Ukiwasaidia watu waaina hiyo ndio unafanya waongezeke town, mm kitambo tu niliishaacha kusaidia omba omba kama serikal ya tz ilivyo
 
Tujivunie ombaomba wetu kwa kuwa wabunifu au na wenyewe pia waletwe kutoka nchi jirani kuja kuomba?
Nawaza kimwendokasi.
 
Kuna mmoja alipanda basi linaloenda kariakoo kutoka mbagala alipandia maeneo ya ufundi..style hio hio y 3600, basi kuna jamaa akasema huyu jamaa mimi nashuka nae naenda nae mpaka amana hospitali gharama za usafiri kila kitu atalipia ile tunafika kariakoo jamaa hayupo alishukia wapi sikumbuki.. .
 
Back
Top Bottom