Kweli maisha hayana formula, jifunze kitu hapa hakika hutaondoka patupu

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,489
BABA alipanda na mwanaye ghorofani. Wakasimama dirishani ghorofa ya tatu. Wakaitazama barabara yenye msongamano. Baba akamtaka mwanaye atazame chini, atafakari, kisha aeleze alichojifunza.

Akasema, aliona magari, yenye kwenda kulia na kushoto. Pikipiki, baiskeli na watembea kwa miguu. Kuna gari lililokuwa linasukumwa.

Yapo magari yaliyokuwa yanakwenda kasi, mengine polepole. Yalikuwepo yenye kuendeshwa vibaya na kuna yaliyogongana.

Baba akamwambia mtoto wake: “Unachokiona ndio tafsri halisi ya maisha. Dunia na wana wa dunia, hali zao za kimaisha na hatua wanazopiga kila iitwapo leo.”

Akaendelea: “Magari yamezidiana. Yupo anaendesha gari la mabilioni, mwingine mamilioni. Wote wana magari lakini wamezidiana mbali. Kuna wa pikipiki na baiskeli. Kisha wapanda usafiri wa umma na watembea kwa miguu.

“Wapo wenye magari ila hawana nyumba. Kuna wasio na magari ila wana nyumba. Yupo mtembea kwa miguu alimfukuza kwenye nyumba mwenye gari kwa kushindwa kulipa kodi. Halafu, dunia inao walio na vyote, nyumba na magari, ila nyumbani hapakaliki.

“Gari linalosukumwa ni kipimo kuwa hata ukiwa nacho utahitaji msaada wa asiyenacho. Usafiri wa umma ni tafsiri kuwa wenyenacho huwaona wasionacho ni fursa. Wafanyakazi wa usafiri wa umma hukimbilia fursa kwa wenyenacho. Hivyo, hata iweje, wewe ni fursa.

“Magari kwenda kushoto na kulia ni kuonesha kwamba unapotoka mwingine ndio anakwenda. Watu wanalowea ughaibuni kusaka fursa. Wakati kwenye nchi zao wamejaa raia wa kigeni waliokimbilia fursa. Kuna Watanzania China. Halafu Wachina wapo Tanzania.

“Watu walitoka Geita kwenda Dar es Salaam kusaka maisha, ila kuna waliopaona Dar pagumu wakaenda kufanikiwa Geita. Watu wanaacha fursa karibu na kuzifuata mbali. Wengine huona hata aibu kurejea nyumbani baada ya kufeli mbali. Aliowaacha wamefaulu, yeye bado anachechemea.”

Baba akamtazama mtoto wake, akamwambia: “Unapoyaelekea maisha zingatia utofauti huu. Huwezi kuwa kila mtu. Utakuwa wewe na hali yako. Yashinde maisha ila ukumbuke kuwa hata uwe na hali gani, lazima utahitaji watu. Hata hivyo, hutahitaji kila mtu. Akili ikae mahali pake.”
 
Maisha ni Siri nzito sana aliyeweka Muumba,,

Ila Kuna juhudi na mipango ndani yake.

Maisha ni karata,,

Changa karata zako vizuri.

Maisha ni vile wewe mwenyewe ulivyoyapanga,

Yanafata kama mkondo wa maji.
 
Hii ni shule na nusu
 
Maisha ni Siri nzito sana aliyeweka Muumba,,

Ila Kuna juhudi na mipango ndani yake.

Maisha ni karata,,

Changa karata zako vizuri.

Maisha ni vile wewe mwenyewe ulivyoyapanga,

Yanafata kama mkondo wa maji.
Mkuu huwa wanasema "wakati wewe unapanga yako muumba naye anapanga yake" hiyo imekaaje
 
Ndy maana nimeweka Siri kubwa ya Muumba.

Ila maisha ni vile unavyoyatengeneza,

Mfano kusoma,
Kuwekeza ,,nk.

Hivi mtu uishi Kwa kukaa tu kijiweni huna ramani ,,wala huumizi kichwa useme maisha yatabadilika?

Labda upate bahati ya mganga PAZI.
 
Nondo za Mfalme Sulemani katika kitabu cha Mhubiri 1 zinahusika hapa. Ukifikiria vizuri na kwa undani wake life is a joke (ubatili mtupu)....
Screenshot_20221115-041904_Swahili%20Bible%20Offline.jpg
 
BABA alipanda na mwanaye ghorofani. Wakasimama dirishani ghorofa ya tatu. Wakaitazama barabara yenye msongamano. Baba akamtaka mwanaye atazame chini, atafakari, kisha aeleze alichojifunza.

Akasema, aliona magari, yenye kwenda kulia na kushoto. Pikipiki, baiskeli na watembea kwa miguu. Kuna gari lililokuwa linasukumwa.

Yapo magari yaliyokuwa yanakwenda kasi, mengine polepole. Yalikuwepo yenye kuendeshwa vibaya na kuna yaliyogongana.

Baba akamwambia mtoto wake: “Unachokiona ndio tafsri halisi ya maisha. Dunia na wana wa dunia, hali zao za kimaisha na hatua wanazopiga kila iitwapo leo.”

Akaendelea: “Magari yamezidiana. Yupo anaendesha gari la mabilioni, mwingine mamilioni. Wote wana magari lakini wamezidiana mbali. Kuna wa pikipiki na baiskeli. Kisha wapanda usafiri wa umma na watembea kwa miguu.

“Wapo wenye magari ila hawana nyumba. Kuna wasio na magari ila wana nyumba. Yupo mtembea kwa miguu alimfukuza kwenye nyumba mwenye gari kwa kushindwa kulipa kodi. Halafu, dunia inao walio na vyote, nyumba na magari, ila nyumbani hapakaliki.

“Gari linalosukumwa ni kipimo kuwa hata ukiwa nacho utahitaji msaada wa asiyenacho. Usafiri wa umma ni tafsiri kuwa wenyenacho huwaona wasionacho ni fursa. Wafanyakazi wa usafiri wa umma hukimbilia fursa kwa wenyenacho. Hivyo, hata iweje, wewe ni fursa.

“Magari kwenda kushoto na kulia ni kuonesha kwamba unapotoka mwingine ndio anakwenda. Watu wanalowea ughaibuni kusaka fursa. Wakati kwenye nchi zao wamejaa raia wa kigeni waliokimbilia fursa. Kuna Watanzania China. Halafu Wachina wapo Tanzania.

“Watu walitoka Geita kwenda Dar es Salaam kusaka maisha, ila kuna waliopaona Dar pagumu wakaenda kufanikiwa Geita. Watu wanaacha fursa karibu na kuzifuata mbali. Wengine huona hata aibu kurejea nyumbani baada ya kufeli mbali. Aliowaacha wamefaulu, yeye bado anachechemea.”

Baba akamtazama mtoto wake, akamwambia: “Unapoyaelekea maisha zingatia utofauti huu. Huwezi kuwa kila mtu. Utakuwa wewe na hali yako. Yashinde maisha ila ukumbuke kuwa hata uwe na hali gani, lazima utahitaji watu. Hata hivyo, hutahitaji kila mtu. Akili ikae mahali pake.”

Sijajifunza kitu kwa kweli
 
Hawakupi formula kwasababu kuna Mbambamba nyingi.
Ni kwl,halafu wakija humu jukwaani wanapaza sauti kubwa kwamba Maisha hayana formula.

Maisha yana code nyingi mno.

Ukitaka kujuwa code za waliofanikiwa basi ukae nao karibu.

Utagunduwa code nyingi sana za maisha.
 
Back
Top Bottom