Kweli Magufuli atataifisha mashamba ya Mwinyi, Mkapa, Mangula na Sumaye au hapa Uongo Tu?


Mkuu JokaKuu,
viongozi wa CCM siku zote ni waongo waongo tuu na hadaa kwa wingi!, wanatoa ahadi kwa paying the lip service tuu kutafutia kura, akishachaguliwa, hakuna kitu!, ni maneno matupu tuu haya!.

Hata Prof. Tibaijuka, alipoingia, aliingia kwa kupiga mkwala mzito kwa kuahidi, kuvirejesha viwanja vyote vya wazi vilivyovamiwa, alipokuta kumbe anayeongoza kwa uvamizi na uporaji wa viwanja vya wazi ni CCM!, alishika breki!, kumbe ule ulikuwa mkwala mbuzi tuu, na kama ni nguvu, then ilikuwa ni nguvu ya soda tuu!. Ukombozi wa kweli wa pili wa nchi hii ni kwa kupitia UKAwA tuu!.

Ila pia, kwenye tathmini yangu kumhusu Magufuli, he is very unpredictable and can make the worst dictator this country has ever had!.
Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5,


Huyu ni populist type, hivyo kama kuyataifisha would make him more popular, he can do it!, and not only that, anaweza hata kurudisha zile nyumba za serikali, majambazi haya, walizojigawia wenyewe, na vimada wao, kwa sababu ameishawaporomoshea maghorofa ya kufa mtu!. Mfano yule kimada wake, anayeanzia na jina la 'K', ndiye mwenye ile hoteli inayoanzia na jina la 'K', pale maeneo ilipo!.(kutaja majina na mahali ilipo ni umbeya, na sisi humu jf, hatutaki umbeya!)

Tukisema la ukweli, Magufuli ni mzuri kuliko Lowassa, tatizo sio Magufuli, tatizo ni CCM, watu ameichoka CCM mpaka basi! kiasi cha kuifananisha na shetani, hivyo CCM wanaonekana kama ni mashetani fulani! kiasi kwamba hata ukimleta malaika kuja kuongoza CCM, ataonekana ni shetani tuu!, huku wale mashetani, waliotoka CCM kujiunga upinzani, wanaonekana wao ni malaika!.
Pasco
Kumbukizi... September, 2015

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..kweli Magufuli amebadilika.

..hivi kuna aliyetegemea atakuja kujimilikisha jipande la ardhi kuzidi hata wale aliokuwa akiwashambulia?

cc Erythrocyte , tindo
 
Nani Atamfunga Paka
download.jpeg.jpg
 
..Dr.Magufuli amekuwa akijiapiza kwa wananchi kwamba atataifisha mashamba ya vigogo yaliyoko mkoani Morogoro na maeneo mengine nchini.

..hili suala la vigogo wa nchi hii kujimilikisha maeneo makubwa ya ardhi lilikuwa likipigiwa kelele kwa muda mrefu na Mh.Halima Mdee ambaye ni waziri kivuli wa ardhi.

..rekodi za hansard za bunge letu zinaonyesha kwamba vigogo waliojitwalia maeneo makubwa ya ardhi ni pamoja na Mzee Ali Hassan Mwinyi[eka 2000], Mzee Philip Mangula[eka 2000], Mzee Mkapa[eka 1000], Mzee Frederick Sumaye[eka 500], Brig.Gen.Hassan Ngwilizi[eka 100], Mzee Cygwiyemwisi Malecela[eka 100]. Kwa uchache niwakumbuka hao.

..wakati Halima Mdee akilipigania suala hili kwa kipindi[2010-2015] chote cha bunge lililopita, Dr.Magufuli alikuwa kimya. Hakuwahi kulizungumzia kwa namna yoyote ile.

..Zaidi, baadhi ya hao anaodai atataifisha ardhi zao, ndiyo waliompigania mpaka akapata nafasi hiyo, na vilevile ndiyo wapiga kampeni wake wakubwa.

..Je, ktk mazingira hayo tunaweza kweli kumuamini Magufuli na kauli yake ya kutaifisha ardhi za vigogo?

cc FJM, Nguruvi3, GalaxyS3, Rev. Kishoka, Alinda, VUTA-NKUVUTE, Pasco, Sikonge
Wapumbavu wengi sana nchiiii...
Ccm has made the country poorer and created a high number of unemployed people in this country in the last five years. Imagine the next five years how will it be worse than this . This I promise you things will be terrible, many people will lose their lives, unemployment will be higher, hakuna investors who will be coming to this country...we shall be chasing Zimbabwe as a rogue state.... Shauri yenu...
 
..kweli Magufuli amebadilika.

..hivi kuna aliyetegemea atakuja kujimilikisha jipande la ardhi kuzidi hata wale aliokuwa akiwashambulia?

cc Erythrocyte , tindo

Ndio maana analazimisha kampeni ziwe atakavyo yeye, eti uza sera na sio kumsema mtu. Kumbe lengo lake ni wizi wake usifahamike.
 
Back
Top Bottom