Kweli Magufuli anataka kuifufua ATCL, ila hii "kachumbari ya ndege" anazonunua inatia mashaka

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Wakati tunaendelea kumpongeza Rais JPM kwa juhudi zake za kufufua shirika la ndege Tanzania(ATCL) tujipe na muda wa kutafakari pia mambo mengine na "kuhoji" kwa nia njema ya kutuondoa hapa tulipo kwenda mbele.Kuhoji kwetu ichukuliwe kama changamoto ya kulihuisha shirika letu na si kuliangamiza.Isije ikawa kuna watu hawamshauri vizuri Mzee au wanataka kumuingiza kwenye historia ya walioshindwa kuirudisha ATCL angani kama miaka ya 1980.

Rais JPM kwa mara moja amenunua ndege aina ya Bombardier Dash8-Q400(Next Generation),na sasa ametoa ahadi ya kuleta ndege nyingine aina ya Bombardier CS300.Ndege hizi zote ni "Kabila" moja la Bombardier lkn ni "ukoo" tofauti,moja ni turboprop engines wakati mwingine ni jet engines.Hawa ni uzao wa "Kabila" moja toka Canada.

Baadae tumemsikia Rais akisema ameshaangiza B787(Dreamliner).Hivyo kufikia miaka mitatu toka sasa,ATCL itakuwa na Dash8-Q400,CS300 na B787(Dreamliner).Hii ni "kachumbari" isiyo na viungo...Inaweza kuliletea shirika changamoto na hata hasara huko mbele ya safari,na tukadidimia kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Masharika mengi duniani na hasa yanayotaka kuinuka kurudi ktk ushindani wa soko la usafiri wa anga,huwa wana kitu wanaita "Fleet Commonality";yaani shirika la ndege linaamua kununua au kukodisha ndege za jamii moja,zinazotoka kwa manufacturer mmoja lkn zikawa na model pamoja na generation tofauti.

Yaani mnaamua kama ni kuwa ni Airbus,basi shirika linakuwa na ndege zote toka Airbus lkn zikatofautina model na generation,au mkatumia Boeing,Bombardier,ATR,Embrer nk.

Hii "Fleet Communality" ina aina nyingi;inaweza kuwa same model and Same Generation ya ndege,mfano Boeing 737-700,B737-700ER na B737-700c au Same model na different Generation,mfano Boeing 737-700 New Genaration au MAX737 nk.

Kuna faida nyingi kwa shirika kuamua kuwa na ndege kutoka kampuni/mzalishaji mmoja kuliko kuwa na shirika lenye ndege kama "kachumbari".Yaani shirika l moja kama ATCL lina ndege kutoka Bombardier,Boeing na Airbus.Huu ni mseto unaotishia ukuwaji wa shirika kibiashara na kiutaalamu.Faida kubwa ni kuwa mnapunguza ghalama za ku-train marubani na pia kupunguza ghalama za maintanance.

Mpaka sasa ATCL imeleta ndege aina ya Bombardier,na hatukuwa na marubani wa kurusha aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa darasani,hatukuwa na wahandisi wa aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa pia darasani kufungua modules za Q400.Na hata sasa,bado tumeazima wahandisi toka Zimbabwe na Malawi walio na uzoefu wa kuhudumia ndege hizo.

Hii ni kusema hata sasa shirika kama ATCL linatakiwa lijizatiti lenyewe kwa kuwa na wahandisi wake na si wa kuazima na marubani wake na si wa kuazima,ile ile dhana ya kuongeza faida na kubana matumizi itimie.

Kenya na "vurugu" zake katika usafiri wa anga,Dreamliner zimawatia adabu.Hao Ethipia wana Dreamliner kadhaa,lkn mpaka sasa mainnjia na marubani wa ndege hizo ni kutoka nje ya Ethiopia;yaani wanakodi kuanzia Pilot in Command,First Officer na Injinia.Hawajawa na mainjinia walio "certfied" kuigusa na kuikarabati Dreamliner...

Kumpata rubani Tanzania hii mwenye masaa(rating) ya kuendesha Dreamliner sio kazi ya mwaka mmoja,na kumpata injinia wa kuihudumia Dreamliner aliyekuwa certified siyo kazi ya mwaka mmoja.Ni safari ndefu.Haiwezekani rubani mwenye rating ya pangaboi aingie moja kwa moja kwenye dreamliner.Inahitaji muda na pesa.

Kununua tu hiyo "Flight Simulator" ya Dreamliner kwa ajili ya kufundishia marubani ni sawasawa na kununua bombardier nyingine.Mwisho wa siku,hizo ndege zikija,na kwa kiwango cha kimataifa tutakodisha kuanzia rubani mpaka injinia wa dreamliner sbb kuwapata wazawa itachukua muda mrefu kidogo.Wakati tunataka kurirudisha shirika angani,basi tungefuata "Fleet Commonality" ili baadae ndio tuingie kwenye hiyo "Cross Manufacturing".

Mashirika mengi yamefanya hivyo,Kenya imezingatia na inamiliki ndege aina moja za E170 na E190 pamoja na Boeing.Hii inawasaidia kuwa na marubani wenye ujuzi wa aina hizo za ndege na hivyo kuepusha ghalama,pia inasaidia sbb wanakuwa na injinia wenye leseni za E190 na hivyo kupunguza ghalama.Ethiopia yeye ameamua kuwa na Bombardier na Boeing tu.Kuanzia B737,735,767,777 na 738.Rwanda alichofanya amenunua Bombardier,Boeing na sasa Airbus na "amekodisha" marubani na wahandisi wote toka Ethiopia ili wamfundishie vijana wake kwa mkataba wa miaka 7.

Kutoka kuwa shirika "mfu" na kuacha kuzingatia "Fleet Commonality" ni kama tunarudi kulekule walikoshindwa waliotangulia.

Uliletwa uzi humu watu "wanalalamika" kuiona Pangaboi ikizunguka Dsm siku nzima badala ya kuanza safari za mikoani.Ile ilikuwa ni "Touches and Goes" ili wale marubani walioenda darasani kufanya kwa vitendo kabla ya kukabidhiwa.Sasa ikumbukwe mafunzo yake sio kama gari,kwamba unajifunza huku ukiwa na chombo.Kwenye ndege ni "Flight Simulator" ambayo baada ya kumaliza,ndio unapewa ndege huku ukiwa na instructor,na kukabidhiwa ndege ni hadi pale utakapoonekana umefudhu kweli(usije kuuwa watu)

Sasa hata kama tulipeleka marubani sita kwa maana ya pair tatu,basi hapo wenye uwezo wa kurusha ni watatu tu,huku hawa wengine wakitumia hata mwaka mzima kupata uzoefu na masaa ya kuwa pilot in command.Gharama hizi zote tunaweza kuziepusha kwa kuzingatia "FLEET COMMONALITY" kwa kuwa na ndege za kampuni moja itakayotusaidia kuzalisha wahandisi namarubani walio certified kwa aina fulani ya ndege, kuliko kukimbilia kwenye "haterogenious fleet" itakayoongeza ghalama zaidi.

Tujifunze kwa LAM(Mozambique) walioamua kuwa na Boieng na E190, Kenya walioamua kuwa na Boieng na E190,Ethiopia walioamua kuwa na Boeing na Bombardier,South Africa Airways walioamua kuwa na Airbus na Boeing,Egypt Air walioamua kuwa na Boeing na Airbus. Hii "kachumbari" ya Pangaboi,CS300 na Dreamliner, inaweza kuturudisha kulekule tulipojikwaa.

Kuhama toka kwenye "bombadia" mpaka kwenye "Dreamliner" ambayo ni B787(New Generation) wakati tumeacha wala hatuna wataalamu wa B737,B738,B739,B767 na B777...tumeruka generation yote ya kati mpaka kurukia latest ya B787....

Ni mtazamo tu;hatuisimangi ATCL
 
barafu ushauri muruwa mm naona kuna kutafuta sifa kama nimenunua ndege nzuri instead ya kusimamisha shirika maana atakuja na airbus kutusifia na pia tutanunua hebu tuwe makini madam nia rais kaonyesha aache wataalam wafanye yao
 
Kwa ipande mmoja upo sahihi. Mimi napenda kufahamu zaidi kuhusu namna ya kuwapata marubani na wahandisi wa aina yoyote ya ndege.

1. Inachukua miaka mingapi kuwafundisha. Gharama kwa mtu mmoja ni kiasi gani?

2. Kwa nini wakati huu tunapoagiza ndege na kutanguliza kishika uchumba tusianze pia kuwasomesha hawa wataalamu?

3. Hivi wazungu wao hawaishiwi wataalamu hata kama ni aina mpya ya ndege imebuniwa. Inakuwaje wao aina mpya ya ndege ikitoka wanakuwa na marubani na mainjinia WAZOEFU tena wa kuyosha? Hii taalima ya urubani na uhandisi wa ndege ikoje kwamba rubani wa CS 300 hawezi ongoza A220? Mbona mie naendwsha beetle toyota na hata bugati kwa kuelekezwa tu mara moja?

Nayasema haya kwani kimezuka baadhi ya taalima ambazo wana taalima wake hujoona wao ni WATEULE. Na pia kuna katania ka wazungu kutaka kuwa marubani wa airliner zote duniani.
 
Haya matumizi makubwa ya fedha sijui yamepangiwa bajeti na wizara gani na bunge letu tukufu, au mkulu anachepua mwenyewe toka hazina!? Nachelea kuona watoto wanakosa chanjo za degedegeu,polio,surua na pepopunda kutokana na budget deficit.
 
Sababu nyingine itakayoiua Air Tanzania ni gharama za "ground handling". Swissport ndiyo imetawala na sidhani kama Air Tanzania wana uwezo wa kuwa na kampuni yake binafsi ya kufanya shughuli hizo.
Mashirika mengine duniani yanapunguza gharama za uendeshaji kwa kuzihudumia ndege zao wao wenyewe, lakini ninapata wasiwasi kama Air Tanzania itaweza kumudu kuilipa Swissport gharama za kuhudumia ndege zake kwa wakati na bila usumbufu hasa ikizingatiwa kuwa kwa zaidi ya mwaka mmoja shirika litafanya biashara kwa hasara. Je, serikali itamudu kutoa ruzuku kwa kipindi chote cha hasara?
Ili shirika liweze kuwa na msuli wa kwenda mbele ni lazima ndege zote ziwe zinajazwa na abiria; je, upo uwezekano wa hilo kutokea?
Naamini mpaka sasa kuna madeni kibao ambayo Air Tanzania inadaiwa huku na kule; ikitokea shirika linadaiwa na kampuni ya mafuta ya ndege kiasi cha kukataliwa kuwekewa mafuta mpaka walipe cash maana credit facility imevurugwa watamudu?
Haya mambo yapo na ni baadhi ya sababu zilizopelekea Precision Air kuyumba na hata kurudisha baadhi ya ndege mfano zile Boeing 737 walizokuwa nazo.
Sijui kama utafiti yakinifu umefanyika au ni mihemko tu ya kuiga nchi zingine.
Tusishangae hizo Bombardier CS300 na Dreamliner zikaja zikaishia kupaki tu uwanjani na kufunikwa maturubai; biashara ya ndege ni extremely complex na haihitaji siasa wala uzalendo uchwara ambao inaonekana unataka kuletwa. Zaidi ya hapo hata Mkurugenzi Mkuu wa Air Tanzania hatakuwa na final say kwenye maamuzi badala yake kila kitu kitaongozwa na bwana yule na hilo ndilo litakalokuwa kaburi la shirika hili.
Je, kuna mkakati wa kupambana na RwandAir, Kenya Airways na wengineo na kuwashinda? Maana asije mtu akadhani wamelala usingizi, la hasha wanaangalia kila move inayofanyika na tukumbuke wana nia ile ile ya kutawala soko la hapa kwetu maana usafiri wa anga huwa hauna mipaka.
Haya ni baadhi tu ya mambo ya kuzingatia.
 
Nimeanza kupinga ununuzi wa ndege tangu awamu ya JK na nitaendelea kupinga kwa angalau kipindi cha miaka 5 ijayo!! Si kwamba hakuna umuhimu wa kuwa na shirika la ndege lakini mabilioni yanayotumika kununua ndege, hata kama shida yetu ni uwekezaji, bado naamini kuna best investment alternatives with higher multiplier effect kuliko ndege!!! Sioni cha maana kwenye kununua ndege hivi sasa zaidi ya stupid & worthless pride... "yaani hata nchi ndogo kama Rwanda wana ndege!!"
 
Kwa mtazamo wa haraka sioni shida kubwa kwa vile Q400 na CS300 tayari zina commonality hapo isipokuwa kwenye engine pekee ni za mfumo tofauti ingawa zinaweza kuwa zimetengenezwa na manufacturer mmoja labda Rolls Royce au GE (sina hakika hapa)
Kwa soko la Tanzania ndege za class ya Q400 ziko nyingi mfano zile ATR kwa hiyo hakuna competitive advantage kwenye soko kwani mapanga shaaa shaaa ni yaleyale hivyo huwezi kuvutia wateja kwa safari ya saa moja dakika 50 wakati mwenye A320 au 737 anatumia saa moja dkk 10. Kwa hiyo naunga mkono wazo la kuleta CS300 ili iweze kuchallenge hizi 320 na 737 kwenye soko lakini pia soko la Tanzania kama ukiamua kufanya low costflight kujaza abiria 150 ni dakika mbili tu ndio maana Fastjet ali expand haraka sana hadi alipobadili module ya biashara na kuanza kuchaji mabei makubwa.

Kwenye Dreamliner nadhani mzee wetu katumia ile hulka ya kingosha, ile ya unaingia dukani na hela ya kuuza pamba unasema nataka shati kama la Masanja na Baskeli kama ya Ng'wana Maduhu. Biashara ya ATCL haijakua kiasi cha kuhitaji Dreamliner kwa hiyo mostly itakuwa idle haina safari za kwenda. Ladba waje waipige safari kama za daladala kwa kuweka bei poa Dar to Mwanza au Kia au Mbeya kwa 100,000- ili kila mtu akimbilie hapo. International flights soko limebana watasubiri sana na kwakuwa gharama za uendeshaji ni kubwa hii itanyonya mapato yote ya shirika.

All in all lazima tumuunge mkono mzee wetu kwa juhudi hizi za kufufua shirika kwa vile amethubutu. Something is better than nothing
 
Mkuu umechambua vizuri sana na kitaalamu. Mimi nipo nje ya nchi na ninafanyakazi za kilimo, hawa jamaa wao matractor yao hupenda kununua kutoka kampuni moja na pia hununua aina ambayo wakulima wengi wanatumia kwani inakuwa ni rahisi na gharama inakuwa ni kidogo kuyahudumia. Nakubaliana na wewe ila tatizo ya sisi wabongo hasa viongozi wetu ukitoa ushauri kama huu watasema umetumwa, mara wewe ni chadema, oh wewe ni mchochezi, wwengine watasema sisi hapa kazi tu, na utawasikia wakisema unaisoma namba au ulizoea kupiga dili......!! Na hapo ndio mwisho wa kujadili kwao. Shirika likifa utasikia mkurugenzi alikuwa fisadi anatakiwa atumbuliwe....!!! Yaan sisi ni shida sana
 
Mkuu uzi murua Kabisa. Lakini tujiulize, Sasa tunaishi kwenye soko huria. Pilots wako wengi wanatafuta kazi. Cha msingi ni wewe unawalipa vipi? Kwa vile ATC imekuwa marehemu mda mrefu in hakika tutapata changamoto Siku za mwanzoni. Lakini penye nia pana njia. Swala la fleet commonality lina changamoto zake. What if nchi husika ikikuwekea vikwazo? Why should you surrender your future into the hands of a single country? Stragecically it makes sense. Let's stop comparing our nascent ATCL with KQ or Ethiopian. We are still in a take off phase.

Yes we need Dreamliner. Kama unasafiri nje mara kwa mara utanielewa. Tz tunapata watalii wengi. Lakini lazima either wapite Kenya au waunge na ndege nyingine. Bwana yule anataka Hawa watalii waje directly. Huoni ni jambo la kupongeza? Na kwamba tutapata wateja kwenye ndege zetu ni swala la huduma ambalo si jukumu la bwana Yule. Hilo ni jukumu letu tunaopewa dhamana.

In all Iam optimistic na nina confidence na bwana yule. Is doing what no one before him ever dared.
 
Kwa ipande mmoja upo sahihi. Mimi napenda kufahamu zaidi kuhusu namna ya kuwapata marubani na wahandisi wa aina yoyote ya ndege.

1. Inachukua miaka mingapi kuwafundisha. Gharama kwa mtu mmoja ni kiasi gani?

2. Kwa nini wakati huu tunapoagiza ndege na kutanguliza kishika uchumba tusianze pia kuwasomesha hawa wataalamu?

3. Hivi wazungu wao hawaishiwi wataalamu hata kama ni aina mpya ya ndege imebuniwa. Inakuwaje wao aina mpya ya ndege ikitoka wanakuwa na marubani na mainjinia WAZOEFU tena wa kuyosha? Hii taalima ya urubani na uhandisi wa ndege ikoje kwamba rubani wa CS 300 hawezi ongoza A220? Mbona mie naendwsha beetle toyota na hata bugati kwa kuelekezwa tu mara moja?

Nayasema haya kwani kimezuka baadhi ya taalima ambazo wana taalima wake hujoona wao ni WATEULE. Na pia kuna katania ka wazungu kutaka kuwa marubani wa airliner zote duniani.
Mkuu ndege ni tofauti sana sana.Yaani rubani wa Q400 hawezi kuingia kichwahichwa kwenye CS300 mpaka aende darasani,afuzu na apate masaa(rating) ya kuendesha hiyo CS300.Ndio maana uliona hata baada ya wale rubani wa Tz walioenda kusomea Canada,walivyorudi iliwabidi waruke na Bombadia kila siku zaidi ya masaa 6 hapa Dsm kwenda Znz,Mafia kurudi Dsm ili wapate masaa ya kuwa certified kuendesha Q400,Na watu walileta uzi humu,kuwa kwanini pangaboi inazungukazunguka Dsm;Zaidi ya tofauti ya injini ya Q400 na CS300 pia zinatofautiana Cockpit Layout,hivyo ni lazima mtu akae darasani kuvijua hivi

Injinia wa Q400 hawezi kutengeneza CS300 hata siku moja bila ya kuingia darasani na kuwa certified,kuna models zinasoma na ninlazima mtu azifaulu,sasa unapomaliza modules moja unaenda nyingine,na ukishimdwa ktk modules moja basi unasubiri na kurudia.Sasa kw unyeti wa kazi hii ni ngumu kukuta mtu ana leseni ya bombardier na hapohapo na boeing,kama atakuwa na za bombadiaa basi ujue ni katika models na generation tofauti na sio manufacturer tofauti.

Fleet ya Precision ni ATR,na ubishi wao bado kitengo cha uinjinia kimejaa Wamalawi na Wazimbabwe,ATCL sasa kuna Watz,Wamalawi na Wazimbabwe.Nafikiri nimejibu kidogou
 
Umeandika vizuri sana..lakini tununue ndege Kwanza... Tuwe nazo km kumi na tano. Kachumbali ni nzuri pia
Mkuu kachumbari ina madhara yake,kuna opereting cost,maintanance cost pamoja na training costs.
Sisi ndio tunanyanyuka baada ya kuanguka kwa miaka mingi,tunatakiwa kuwa na Fleet commonality ili tujiimalishe ktk kitengo cha marubani,mafundi nk.

Ndege sio gari,kwamba jana gari uliipeleka gereji ya Sinza fundi akamliza kutengeneza spacio halafu akaja kwenye vitz yako,au we ulijifunza kuendesha gari aina ya Noah halafu ukanunua T.i na kuendesha.

Huku kwenye ndege huwezi kukamata ndege nyingine bila kuwa certified,na hiyo certification hawatoi wabongo kiasi upite njia ya mkato,wanatoa "wenyewe".Sasa rating ya kuinyanyua dreamliner na kuifanyia matengenezo si ya kitoto...kumbuka hizi dreamliner ni ETOPS(Extended-range Twin-Engine Operation Performance Standard)
 
Tunanunua ndege hizi kwa sababu analysis zote zinaonesha zitakuza uchumi wetu au ni prestige tu ya kusema na sisi tuna ndege? Inapendeza kuwa na shirika la ndege lakini sishawishiki kabisa kuwa hizi ndege zitatuongezea uwezo wetu wa kiuchumi, zaidi ninachoamini zitaendelea kula kidogo tulicho nacho.

Siamini kama ndege hizi zitaongeza utalii maana sijaona ni kwa namna gani.
 
Watabiri wamerudi tena!!!
Awamu hii Ni mwendo wa kutabiri kushindwa tu!!!
Lkn mtoa mada umejaribu kujenga hoja lkn haijitoshelezi!!! Hizo sio sababu kweli Za kuifanya ATCL ikwame Na hata ilipo kwama hapo nyuma kabla ya JPM sio kwa sababu hizo!!
RwandaAir wanazo Dreamliner na bombardier, Hao Ethiopia Airline nao hadi Leo hii wanazo Na hawajakwama, sisi ndio tumeanza naamini Na sisi hatutakwama!!!
 
Mkuu ndege ni tofauti sana sana.Yaani rubani wa Q400 hawezi kuingia kichwahichwa kwenye CS300 mpaka aende darasani,afuzu na apate masaa(rating) ya kuendesha hiyo CS300.Ndio maana uliona hata baada ya wale rubani wa Tz walioenda kusomea Canada,walivyorudi iliwabidi waruke na Bombadia kila siku zaidi ya masaa 6 hapa Dsm kwenda Znz,Mafia kurudi Dsm ili wapate masaa ya kuwa certified kuendesha Q400,Na watu walileta uzi humu,kuwa kwanini pangaboi inazungukazunguka Dsm;Zaidi ya tofauti ya injini ya Q400 na CS300 pia zinatofautiana Cockpit Layout,hivyo ni lazima mtu akae darasani kuvijua hivi

Injinia wa Q400 hawezi kutengeneza CS300 hata siku moja bila ya kuingia darasani na kuwa certified,kuna models zinasoma na ninlazima mtu azifaulu,sasa unapomaliza modules moja unaenda nyingine,na ukishimdwa ktk modules moja basi unasubiri na kurudia.Sasa kw unyeti wa kazi hii ni ngumu kukuta mtu ana leseni ya bombardier na hapohapo na boeing,kama atakuwa na za bombadiaa basi ujue ni katika models na generation tofauti na sio manufacturer tofauti.

Fleet ya Precision ni ATR,na ubishi wao bado kitengo cha uinjinia kimejaa Wamalawi na Wazimbabwe,ATCL sasa kuna Watz,Wamalawi na Wazimbabwe.Nafikiri nimejibu kidogou
Ndiyo nikasema hatuna mkakati wa mida wa kati na wa muda mrefu wa kuandaa hawa wataalamu.

Mfano hiyo B787 dreamliner (aloyeipa jina hakukosea. Mashine iko poa sana kila idara) inategemewa kuwasili miaka 2 hadi 3 ijayo. Kwa sasa sibtungeanza kuandaa human resource ya kui handle?

Vivyo hivyo hata kama tunatarajia kikunua A380 au An245 miaka 50 ijayo. Si tuanze maandalizi mapema. Ama hakuna vijana wenye sifa za kusomea urubani na uhandisi wa ndege.

Namaanisha tuanze kuandaa human reaource kulingana na mipango yetu ya maendeleo. Ili siku ikifika unakuta wataalamu wapo.

Pia tuandae infrastructure zingine kama viwanja vya ndege kuanzia runway hadi majengo ya abiria (Lile la mwanza ni kichefuchefu) vyuo vya mafunzo au kitaala ya mafunzo husika. Kuimarisha utabiri wa halivya hewa na usalama wa hanga jwa ujumla.
 
Back
Top Bottom