Kweli Magufuli anataka kuifufua ATCL, ila hii "kachumbari ya ndege" anazonunua inatia mashaka

Barafu pamoja na kujaribu kufanya analysis yako ionekane ina mwelekeo, naona kama ina mambo mengi ya kujiuliza kuhusu hicho ulichokiita kachumbali. Rwanda Air wana boeing, Q400, na airbus, Ethiopia pia wana mchanganyiko huko huo. Air Tanzania wana Bombardier na wanategemea kuleta Boeing. Je nani ana fleet commonality? Biashara ya ndege imekuwa ikibadilika sana na kile kilichoaminiwa zamani sio lazima kuwa kwa mazingira ya kisasa kinaendelea kuwa ukweli. Kiukweli ushindani katika soko la usafiri wa anga kwa sasa linataliwa na uwezo wa ndege zako katika matumizi ya mafuta na uwezo wa injini . Ndio sababu kila mmoja anahama kutoka kabila moja ya ndege kwenda ingine kwa kuangalia ni ndege kabila ipi itampatia faida ya ushindani (competitive advantage). Swala la commonality katika mazingira ya sasa ni kama Lina kosa usahihi wenye uhakika na ndio sababu Ethiopia na Rwanda wamechanganya au wanakachumbali kubwa sana. Kwa ndege za mapanga zilizopo tanzania, Q400 imeonyesha kuwa na performance nzuri sana na hili si kwa Tanzania tu bali dunia ni kote. Hata hivyo ATcL lazima ajiulize ni soko lipi analolilenga na kama Q400 zitamwezesha kushindana. Jibu ni lazima afikiri nje ya Q400 kwa kutilia maanani kuwa kina Rwanda, Kenya, South Africa, na Ethiopia wako huko na wanatumia regional jet, boeing, airbus, embraer, nk. Hivyo ni lazima aliangalie soko kwa mtizamo huo pia. Kwa kigezo cha faida ya kiushindani Cseries inamfaa na sio Q400 maana ndio iko katika jamii ya regional jet! Angalia ni mashirika mangapi yameshawikika kununua cseries na sababu ni ipi. Commonality ameendelea nayo maana bado yuko kwenye familia moja ya bombardier tofauti ni aina ya ndege. Commonality sio kutumia Q400 tu bali mtengenezaji mmoja. Kwa kufuata kigezo cha commonality, ATCL angefikiria pia kupata wide body (ndege kubwa) kutoka bombardier ili aweze kuwa na uwezo wa kushindana beyond soko la regional jet. Kwa bahati mbaya bombardier hana wide body hivyo ni lazima aende airbus au boeing kama anataka ajitanue zaidi kiushindani. Kwa kigezo kile kile cha kupata faida ya ushindani ameona boeing 787 ni bora kuliko airbus 330 au 350!
Naomba mnisaidie kunionyosha iko wapi hiyo kachumbali. Je Ukimfananisha ATCL na Rwanda au Ethiopia nani ana kachumbali? Je, faida ya ushindani kwa kuwa na commonality bado ipo katika mazingira ya sasa ukiangalia swala la mafuta na engine performance? Nisaidieni kujibu.

Wakati tunaendelea kumpongeza Rais JPM kwa juhudi make za kufufua shirika la ndege Tanzania(ATCL) tujipe na muda wa kutafakari pia mambo mengine na "kuhoji" kwa nia njema ya kutuondoa hapa tulipo kwenda mbele.Kuhoji kwetu ichukuliwe kama changamoto ya kulihuisha shirika letu na si kuliangamiza.Isije ikawa kuna watu hawamshauri vizuri Mzee au wanataka kumuingiza kwenye historia ya walioshindwa kuirudisha ATCL angani kama miaka ya 1980.

Rais JPM kwa mara moja amenunua ndege aina ya Bombardier Dash8-Q400(Next Generation),na sasa ametoa ahadi ya kuleta ndege nyingine aina ya Bombardier CS300.Ndege hizi zote ni "Kabila" moja la Bombardier lkn ni "ukoo" tofauti,moja ni turboprop engines wakati mwingine ni jet engines.Hawa ni uzao wa "Kabila" moja toka Canada.

Baadae tumemsikia Rais akisema ameshaangiza B787(Dreamliner).Hivyo kufikia miaka mitatu toka sasa,ATCL itakuwa na Dash8-Q400,CS300 na B787(Dreamliner).Hii ni "kachumbari" isiyo na viungo...Inaweza kuliletea shirika changamoto na hata hasara huko mbele ya safari,na tukadidimia kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Masharika mengi duniani na hasa yanayotaka kuinuka kurudi ktk ushindani wa soko la usafiri wa anga,huwa wana kitu wanaita "Fleet Commonality";yaani shirika la ndege linaamua kununua au kukodisha ndege za jamii moja,zinazotoka kwa manufacturer mmoja lkn zikawa na model pamoja na generation tofauti.

Yaani mnaamua kama ni kuwa ni Airbus,basi shirika linakuwa na ndege zote toka Airbus lkn zikatofautina model na generation,au mkatumia Boeing,Bombardier,ATR,Embrer nk.

Hii "Fleet Communality" ina aina nyingi;inaweza kuwa same model and Same Generation ya ndege,mfano Boeing 737-700,B737-700ER na B737-700c au Same model na different Generation,mfano Boeing 737-700 New Genaration au MAX737 nk.

Kuna faida nyingi kwa shirika kuamua kuwa na ndege kutoka kampuni/mzalishaji mmoja kuliko kuwa na shirika lenye ndege kama "kachumbari".Yaani shirika l moja kama ATCL lina ndege kutoka Bombardier,Boeing na Airbus.Huu ni mseto unaotishia ukuwaji wa shirika kibiashara na kiutaalamu.Faida kubwa ni kuwa mnapunguza ghalama za ku-train marubani na pia kupunguza ghalama za maintanance.

Mpaka sasa ATCL imeleta ndege aina ya Bombardier,na hatukuwa na marubani wa kurusha aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa darasani,hatukuwa na wahandisi wa aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa pia darasani kufungua modules za Q400.Na hata sasa,bado tumeazima wahandisi toka Zimbabwe na Malawi walio na uzoefu wa kuhudumia ndege hizo.

Hii ni kusema hata sasa shirika kama ATCL linatakiwa lijizatiti lenyewe kwa kuwa na wahandisi wake na si wa kuazima na marubani wake na si wa kuazima,ile ile dhana ya kuongeza faida na kubana matumizi itimie.Kenya na "vurugu" zake katika usafiri wa anga,Dreamliner zimawatia adabu.Hao Ethipia wana Dreamliner kadhaa,lkn mpaka sasa mainnjia na marubani wa ndege hizo ni kutoka nje ya Ethipia;yaani wanakodi kuanzia Pilot in Command,First Officer na Injinia.Hawajwa na mainjinia walio "certfied" kuigusa na kuikarabati Drwmliner...

Kumpata rubani Tanzania hii mwenye masaa(rating) ya kuendesha Dreamliner sio kazi ya mwaka mmoja,na kumpata injinia wa kuihudumia Dreamliner aliyekuwa certified siyo kazi ya mwaka mmoja.Ni safari ndefu.Haiwezekani rubani mwenye rating ya pangaboi aingie moja kwa moja kwenye dreamliner.Inahitaji muda na pesa.

Kununua tu hiyo "Flight Simulator" ya Dreamliner kwa ajili ya kufundishia marubani ni sawasawa na kununua bombardier nyingine.Mwisho wa siku,hizo ndege zikija,na kwa kiwango cha kimataifa tutakodisha kuanzia rubani mpaka injinia wa dreamliner sbb kuwapata wazawa itachukua muda mrefu kidogo.Wakati tunataka kurirudisha shirika angani,basi tungefuata "Fleet Commonality" ili baadae ndio tuingie kwenye hiyo "Cross Manufacturing".

Mashirika mengi yamefanya hivyo,Kenya imezingatia na inamiliki ndege aina moja za E170 na E190 pamoja na Boeing.Hii inawasaidia kuwa na marubani wenye ujuzi wa aina hizo za ndege na hivyo kuepusha ghalama,pia inasaidia sbb wanakuwa na injinia wenye leseni za E190 na hivyo kupunguza ghalama.Ethiopia yeye ameamua kuwa na Bombardier na Boeing tu.Kuanzia B737,735,767,777 na 738.Rwanda alichofanya amenunua Bombardier,Boeing na sasa Airbus na "amekodisha" marubani na wahandisi wote toka Ethiopia ili wamfundishie vijana wake kwa mkataba wa miaka 7.

Kutoka kuwa shirika "mfu" na kuacha kuzingatia "Fleet Commonality" ni kama tunarudi kulekule walikoshindwa waliotangulia.

Uliletwa uzi humu watu "wanalalamika" kuiona Pangaboi ikizunguka Dsm siku nzima badala ya kuanza safari za mikoani.Ile ilikuwa ni "Touches and Goes" ili wale marubani walioenda darasani kufanya kwa vitendo kabla ya kukabidhiwa.Sasa ikumbukwe mafunzo yake sio kama gari,kwamba unajifunza huku ukiwa na chombo.Kwenye ndege ni "Flight Simulator" ambayo baada ya kumaliza,ndio unapewa ndege huku ukiwa na instructor,na kukabidhiwa ndege ni hadi pale utakapoonekana umefudhu kweli(usije kuuwa watu)

Sasa hata kama tulipeleka marubani sita kwa maana ya pair tatu,basi hapo wenye uwezo wa kurusha ni watatu tu,huku hawa wengine wakitumia hata mwaka mzima kupata uzoefu na masaa ya kuwa pilot in command.Ghalama hizi zote tunaweza kuziepusha kwa kuzingatia "FLEET COMMONALITY" kwa kuwa na ndege za kampuni moja itakayotusaidia kuzalisha wahandisi namarubani walio certified kwa aina fulani ya ndege,kuliko kukimbilia kwenye "haterogenious fleet" itakayoongeza ghalama zaidi.

Tujifunze kwa LAM(Mozambique) walioamua kuwa na Boieng na E190,Kenya walioamua kuwa na Boieng na E190,Ethiopia walioamua kuwa na Boeing na Bombardier,South Africa Airways walioamua kuwa na Airbus na Boeing,Egypt Air walioamua kuwa na Boeing na Airbus.Hii "kachumbari" ya Pangaboi,CS300 na Dreamliner,inaweza kuturudisha kulekule tulipojikwaa.

Ni mtazamo tu;hatuisimangi ATCL
 
Sababu nyingine itakayoiua Air Tanzania ni gharama za "ground handling". Swissport ndiyo imetawala na sidhani kama Air Tanzania wana uwezo wa kuwa na kampuni yake binafsi ya kufanya shughuli hizo.
Mashirika mengine duniani yanapunguza gharama za uendeshaji kwa kuzihudumia ndege zao wao wenyewe, lakini ninapata wasiwasi kama Air Tanzania itaweza kumudu kuilipa Swissport gharama za kuhudumia ndege zake kwa wakati na bila usumbufu hasa ikizingatiwa kuwa kwa zaidi ya mwaka mmoja shirika litafanya biashara kwa hasara. Je, serikali itamudu kutoa ruzuku kwa kipindi chote cha hasara?
Ili shirika liweze kuwa na msuli wa kwenda mbele ni lazima ndege zote ziwe zinajazwa na abiria; je, upo uwezekano wa hilo kutokea?
Naamini mpaka sasa kuna madeni kibao ambayo Air Tanzania inadaiwa huku na kule; ikitokea shirika linadaiwa na kampuni ya mafuta ya ndege kiasi cha kukataliwa kuwekewa mafuta mpaka walipe cash maana credit facility imevurugwa watamudu?
Haya mambo yapo na ni baadhi ya sababu zilizopelekea Precision Air kuyumba na hata kurudisha baadhi ya ndege mfano zile Boeing 737 walizokuwa nazo.
Sijui kama utafiti yakinifu umefanyika au ni mihemko tu ya kuiga nchi zingine.
Tusishangae hizo Bombardier CS300 na Dreamliner zikaja zikaishia kupaki tu uwanjani na kufunikwa maturubai; biashara ya ndege ni extremely complex na haihitaji siasa wala uzalendo uchwara ambao inaonekana unataka kuletwa. Zaidi ya hapo hata Mkurugenzi Mkuu wa Air Tanzania hatakuwa na final say kwenye maamuzi badala yake kila kitu kitaongozwa na bwana yule na hilo ndilo litakalokuwa kaburi la shirika hili.
Je, kuna mkakati wa kupambana na RwandAir, Kenya Airways na wengineo na kuwashinda? Maana asije mtu akadhani wamelala usingizi, la hasha wanaangalia kila move inayofanyika na tukumbuke wana nia ile ile ya kutawala soko la hapa kwetu maana usafiri wa anga huwa hauna mipaka.
Haya ni baadhi tu ya mambo ya kuzingatia.
Mkuu kwenye para ya mwisho umenena vyema. Nakumbuka tamko la bwana yule wakati akiwa kwenye harakati za kununua ndege alidai kwamba alipewa ushauri na kagame anunue Dear bomba na ndizo hizo kanunua. Biashara ya ndege ina figisu nyingi ili uweze kufanikiwa na bwana yule akitaka kuliona hili ajaribu tena kuomba ushauri kwa kagame ndipo hapo atakapopewa mbinu ambazo zinaweza kusabbisha ATCL kuingia kaburini, huwezi kumpa adui yako mbinu ya kukuangamiza. Nia ya kulifufua shirika hili ni njema lakini bwana yule hakutaka ushauri wa wataalamu kabla ya kufanya uamuzi. Katika dunia ya sasa yenye ushindani mkubwa katika uendeshaji wa mashirika ya ndege ni vigumu ATCL kuinuka toka hapo ilipo pamoja na nia hiyo ya serikali. Tungejiuliza kwanza hivi chanzo cha ATCL kuporomoka ni kitu gani na je iwapo litainuka linaweza kupambana kibiashara na mashirika mengine?, tatizo la shirika hili lina madeni makubwa kuliko thamani ya mali inazomiliki na kila senti inayopatikana toka kwenye Dear bomba itakuwa inalipa madeni hivyo ni vigumu sana kuinuka kwa shirika hili
 
Wakati tunaendelea kumpongeza Rais JPM kwa juhudi zake za kufufua shirika la ndege Tanzania(ATCL) tujipe na muda wa kutafakari pia mambo mengine na "kuhoji" kwa nia njema ya kutuondoa hapa tulipo kwenda mbele.Kuhoji kwetu ichukuliwe kama changamoto ya kulihuisha shirika letu na si kuliangamiza.Isije ikawa kuna watu hawamshauri vizuri Mzee au wanataka kumuingiza kwenye historia ya walioshindwa kuirudisha ATCL angani kama miaka ya 1980.

Rais JPM kwa mara moja amenunua ndege aina ya Bombardier Dash8-Q400(Next Generation),na sasa ametoa ahadi ya kuleta ndege nyingine aina ya Bombardier CS300.Ndege hizi zote ni "Kabila" moja la Bombardier lkn ni "ukoo" tofauti,moja ni turboprop engines wakati mwingine ni jet engines.Hawa ni uzao wa "Kabila" moja toka Canada.

Baadae tumemsikia Rais akisema ameshaangiza B787(Dreamliner).Hivyo kufikia miaka mitatu toka sasa,ATCL itakuwa na Dash8-Q400,CS300 na B787(Dreamliner).Hii ni "kachumbari" isiyo na viungo...Inaweza kuliletea shirika changamoto na hata hasara huko mbele ya safari,na tukadidimia kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Masharika mengi duniani na hasa yanayotaka kuinuka kurudi ktk ushindani wa soko la usafiri wa anga,huwa wana kitu wanaita "Fleet Commonality";yaani shirika la ndege linaamua kununua au kukodisha ndege za jamii moja,zinazotoka kwa manufacturer mmoja lkn zikawa na model pamoja na generation tofauti.

Yaani mnaamua kama ni kuwa ni Airbus,basi shirika linakuwa na ndege zote toka Airbus lkn zikatofautina model na generation,au mkatumia Boeing,Bombardier,ATR,Embrer nk.

Hii "Fleet Communality" ina aina nyingi;inaweza kuwa same model and Same Generation ya ndege,mfano Boeing 737-700,B737-700ER na B737-700c au Same model na different Generation,mfano Boeing 737-700 New Genaration au MAX737 nk.

Kuna faida nyingi kwa shirika kuamua kuwa na ndege kutoka kampuni/mzalishaji mmoja kuliko kuwa na shirika lenye ndege kama "kachumbari".Yaani shirika l moja kama ATCL lina ndege kutoka Bombardier,Boeing na Airbus.Huu ni mseto unaotishia ukuwaji wa shirika kibiashara na kiutaalamu.Faida kubwa ni kuwa mnapunguza ghalama za ku-train marubani na pia kupunguza ghalama za maintanance.

Mpaka sasa ATCL imeleta ndege aina ya Bombardier,na hatukuwa na marubani wa kurusha aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa darasani,hatukuwa na wahandisi wa aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa pia darasani kufungua modules za Q400.Na hata sasa,bado tumeazima wahandisi toka Zimbabwe na Malawi walio na uzoefu wa kuhudumia ndege hizo.

Hii ni kusema hata sasa shirika kama ATCL linatakiwa lijizatiti lenyewe kwa kuwa na wahandisi wake na si wa kuazima na marubani wake na si wa kuazima,ile ile dhana ya kuongeza faida na kubana matumizi itimie.Kenya na "vurugu" zake katika usafiri wa anga,Dreamliner zimawatia adabu.Hao Ethipia wana Dreamliner kadhaa,lkn mpaka sasa mainnjia na marubani wa ndege hizo ni kutoka nje ya Ethipia;yaani wanakodi kuanzia Pilot in Command,First Officer na Injinia.Hawajwa na mainjinia walio "certfied" kuigusa na kuikarabati Drwmliner...

Kumpata rubani Tanzania hii mwenye masaa(rating) ya kuendesha Dreamliner sio kazi ya mwaka mmoja,na kumpata injinia wa kuihudumia Dreamliner aliyekuwa certified siyo kazi ya mwaka mmoja.Ni safari ndefu.Haiwezekani rubani mwenye rating ya pangaboi aingie moja kwa moja kwenye dreamliner.Inahitaji muda na pesa.

Kununua tu hiyo "Flight Simulator" ya Dreamliner kwa ajili ya kufundishia marubani ni sawasawa na kununua bombardier nyingine.Mwisho wa siku,hizo ndege zikija,na kwa kiwango cha kimataifa tutakodisha kuanzia rubani mpaka injinia wa dreamliner sbb kuwapata wazawa itachukua muda mrefu kidogo.Wakati tunataka kurirudisha shirika angani,basi tungefuata "Fleet Commonality" ili baadae ndio tuingie kwenye hiyo "Cross Manufacturing".

Mashirika mengi yamefanya hivyo,Kenya imezingatia na inamiliki ndege aina moja za E170 na E190 pamoja na Boeing.Hii inawasaidia kuwa na marubani wenye ujuzi wa aina hizo za ndege na hivyo kuepusha ghalama,pia inasaidia sbb wanakuwa na injinia wenye leseni za E190 na hivyo kupunguza ghalama.Ethiopia yeye ameamua kuwa na Bombardier na Boeing tu.Kuanzia B737,735,767,777 na 738.Rwanda alichofanya amenunua Bombardier,Boeing na sasa Airbus na "amekodisha" marubani na wahandisi wote toka Ethiopia ili wamfundishie vijana wake kwa mkataba wa miaka 7.

Kutoka kuwa shirika "mfu" na kuacha kuzingatia "Fleet Commonality" ni kama tunarudi kulekule walikoshindwa waliotangulia.

Uliletwa uzi humu watu "wanalalamika" kuiona Pangaboi ikizunguka Dsm siku nzima badala ya kuanza safari za mikoani.Ile ilikuwa ni "Touches and Goes" ili wale marubani walioenda darasani kufanya kwa vitendo kabla ya kukabidhiwa.Sasa ikumbukwe mafunzo yake sio kama gari,kwamba unajifunza huku ukiwa na chombo.Kwenye ndege ni "Flight Simulator" ambayo baada ya kumaliza,ndio unapewa ndege huku ukiwa na instructor,na kukabidhiwa ndege ni hadi pale utakapoonekana umefudhu kweli(usije kuuwa watu)

Sasa hata kama tulipeleka marubani sita kwa maana ya pair tatu,basi hapo wenye uwezo wa kurusha ni watatu tu,huku hawa wengine wakitumia hata mwaka mzima kupata uzoefu na masaa ya kuwa pilot in command.Ghalama hizi zote tunaweza kuziepusha kwa kuzingatia "FLEET COMMONALITY" kwa kuwa na ndege za kampuni moja itakayotusaidia kuzalisha wahandisi namarubani walio certified kwa aina fulani ya ndege,kuliko kukimbilia kwenye "haterogenious fleet" itakayoongeza ghalama zaidi.

Tujifunze kwa LAM(Mozambique) walioamua kuwa na Boieng na E190,Kenya walioamua kuwa na Boieng na E190,Ethiopia walioamua kuwa na Boeing na Bombardier,South Africa Airways walioamua kuwa na Airbus na Boeing,Egypt Air walioamua kuwa na Boeing na Airbus.Hii "kachumbari" ya Pangaboi,CS300 na Dreamliner,inaweza kuturudisha kulekule tulipojikwaa.

Ni mtazamo tu;hatuisimangi ATCL
Hivi kwanini hukupeleka CV yako wakati magu anaanza huu mchakato?Mweh!
 
Ndiyo nikasema hatuna mkakati wa mida wa kati na wa muda mrefu wa kuandaa hawa wataalamu.

Mfano hiyo B787 dreamliner (aloyeipa jina hakukosea. Mashine iko poa sana kila idara) inategemewa kuwasili miaka 2 hadi 3 ijayo. Kwa sasa sibtungeanza kuandaa human resource ya kui handle?

Vivyo hivyo hata kama tunatarajia kikunua A380 au An245 miaka 50 ijayo. Si tuanze maandalizi mapema. Ama hakuna vijana wenye sifa za kusomea urubani na uhandisi wa ndege.

Namaanisha tuanze kuandaa human reaource kulingana na mipango yetu ya maendeleo. Ili siku ikifika unakuta wataalamu wapo.

Pia tuandae infrastructure zingine kama viwanja vya ndege kuanzia runway hadi majengo ya abiria (Lile la mwanza ni kichefuchefu) vyuo vya mafunzo au kitaala ya mafunzo husika. Kuimarisha utabiri wa halivya hewa na usalama wa hanga jwa ujumla.
Mawazo mazuri. Lakini chini ya CCM, hayawezi kutimizwa.
 
Sababu nyingine itakayoiua Air Tanzania ni gharama za "ground handling". Swissport ndiyo imetawala na sidhani kama Air Tanzania wana uwezo wa kuwa na kampuni yake binafsi ya kufanya shughuli hizo.
Mashirika mengine duniani yanapunguza gharama za uendeshaji kwa kuzihudumia ndege zao wao wenyewe, lakini ninapata wasiwasi kama Air Tanzania itaweza kumudu kuilipa Swissport gharama za kuhudumia ndege zake kwa wakati na bila usumbufu hasa ikizingatiwa kuwa kwa zaidi ya mwaka mmoja shirika litafanya biashara kwa hasara. Je, serikali itamudu kutoa ruzuku kwa kipindi chote cha hasara?
Ili shirika liweze kuwa na msuli wa kwenda mbele ni lazima ndege zote ziwe zinajazwa na abiria; je, upo uwezekano wa hilo kutokea?
Naamini mpaka sasa kuna madeni kibao ambayo Air Tanzania inadaiwa huku na kule; ikitokea shirika linadaiwa na kampuni ya mafuta ya ndege kiasi cha kukataliwa kuwekewa mafuta mpaka walipe cash maana credit facility imevurugwa watamudu?
Haya mambo yapo na ni baadhi ya sababu zilizopelekea Precision Air kuyumba na hata kurudisha baadhi ya ndege mfano zile Boeing 737 walizokuwa nazo.
Sijui kama utafiti yakinifu umefanyika au ni mihemko tu ya kuiga nchi zingine.
Tusishangae hizo Bombardier CS300 na Dreamliner zikaja zikaishia kupaki tu uwanjani na kufunikwa maturubai; biashara ya ndege ni extremely complex na haihitaji siasa wala uzalendo uchwara ambao inaonekana unataka kuletwa. Zaidi ya hapo hata Mkurugenzi Mkuu wa Air Tanzania hatakuwa na final say kwenye maamuzi badala yake kila kitu kitaongozwa na bwana yule na hilo ndilo litakalokuwa kaburi la shirika hili.
Je, kuna mkakati wa kupambana na RwandAir, Kenya Airways na wengineo na kuwashinda? Maana asije mtu akadhani wamelala usingizi, la hasha wanaangalia kila move inayofanyika na tukumbuke wana nia ile ile ya kutawala soko la hapa kwetu maana usafiri wa anga huwa hauna mipaka.
Haya ni baadhi tu ya mambo ya kuzingatia.
Ruzuku itoke WAP wakati bunge halijui ?mkulu kaamua subirin muone kifo chake! Ni suala la time Tu!
 
Kuingia soko la ushindani ni kuingia kwa strategy ambayo ki environment unaiweza. Bombardier zipo kwa ajili ya locally transportation na nearby country market. Wenye ndege kubwa majirani sidhan kama wana accomodate regional flights mf East Africa kwa ndege kubwa kama dreamliner au boeng 787...yaan itoke Kenya ije Tz iende Uganda.... zaidi iende hata Morocco, huo ni upuuzi wa kupita kiwango.
Pangaboy zinafaa kwa soko la regional na zinahimili hali ya viwanja tulivyonavyo.
Kuwa na dreamliner labda ungehoji swala la route za kuanzia na sio kuwa na kachumbali....tutaanza na routes za wapi...ila as long as kuna strategy ya market entry eg cheapest flight na huduma ambazo ni executives, tunaweza ingia kwa ushindani....anywhere.
Swala la kukodisha experts sehem nyingine ni kawaida. Usidhan mashirika makubwa kama Qatar, emiretes na mengine marubani wote ni wa asili ya middle east. Wanalipa marubani kutoka nje na wanapata faida hata kuwalipa airhostess wa nchi tofautitafauti....mashirika yanayojifanya kutumia experts na airhostess ambao ni locally hayakui sana...nenda Asia kaangalie wachina...wajapan...wahindi kama wanakuwa...kuna shirika la India limekufa sababu ya uzalendo. Kuwa na ndege kwahitaji international thinking, sio locally. Sitashangaa kuona CEO awe mgeni toka hata kwa ngozi nyeupe ili kuliwezesha shirika kukua. Engineers akiwa mbongo yeye mwenyewe yamkini asipande (jokes yenye ukweli) akishafanya maintanance. So kama shirika linahitaji kukua kimataifa we have to think na ku act na globally, hakuna sehem inaendelea pasipo kuwa na blending ya skills.

Swala la kujiendesha ATCL lipate faida mjue kwanza linaweza amua likajiendesha kwa mwaka kwa kufanya breakeven marketing yaaan hadi baada ya services na kila kitu hadi kulipia wanaofanya kazi za kufagia maofisini ndo ikaanza kupata faida...hakuna ofisi inafunguliwa na kuanza na faida....

Tufikiri namna ya kuliwezesha shirika lijiemdeshe na sio kuwaza pessimistic....hatutakuwa kama tunakuwa na mawazo hasi...kachumbali ni flavor tofauti na kusaidoa huduma tofauti kwa level tofauti. Ni mojawapo ya issue muhimu sana kufanya diversification kwenye revenue. Inasaidia risk sharing pia ujue. Pia inatoa nafasi kwa employment opportunities kwa watu ambao li locally maana country short flight hazina huduma zenye kuhitaji kiwa rated sana. Labda kwa regional wise na still watu watakuwa concious sana na price.

Naomba kutoa hoja....viva ATCL.
 
Wakati tunaendelea kumpongeza Rais JPM kwa juhudi zake za kufufua shirika la ndege Tanzania(ATCL) tujipe na muda wa kutafakari pia mambo mengine na "kuhoji" kwa nia njema ya kutuondoa hapa tulipo kwenda mbele.Kuhoji kwetu ichukuliwe kama changamoto ya kulihuisha shirika letu na si kuliangamiza.Isije ikawa kuna watu hawamshauri vizuri Mzee au wanataka kumuingiza kwenye historia ya walioshindwa kuirudisha ATCL angani kama miaka ya 1980.

Rais JPM kwa mara moja amenunua ndege aina ya Bombardier Dash8-Q400(Next Generation),na sasa ametoa ahadi ya kuleta ndege nyingine aina ya Bombardier CS300.Ndege hizi zote ni "Kabila" moja la Bombardier lkn ni "ukoo" tofauti,moja ni turboprop engines wakati mwingine ni jet engines.Hawa ni uzao wa "Kabila" moja toka Canada.

Baadae tumemsikia Rais akisema ameshaangiza B787(Dreamliner).Hivyo kufikia miaka mitatu toka sasa,ATCL itakuwa na Dash8-Q400,CS300 na B787(Dreamliner).Hii ni "kachumbari" isiyo na viungo...Inaweza kuliletea shirika changamoto na hata hasara huko mbele ya safari,na tukadidimia kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Masharika mengi duniani na hasa yanayotaka kuinuka kurudi ktk ushindani wa soko la usafiri wa anga,huwa wana kitu wanaita "Fleet Commonality";yaani shirika la ndege linaamua kununua au kukodisha ndege za jamii moja,zinazotoka kwa manufacturer mmoja lkn zikawa na model pamoja na generation tofauti.

Yaani mnaamua kama ni kuwa ni Airbus,basi shirika linakuwa na ndege zote toka Airbus lkn zikatofautina model na generation,au mkatumia Boeing,Bombardier,ATR,Embrer nk.

Hii "Fleet Communality" ina aina nyingi;inaweza kuwa same model and Same Generation ya ndege,mfano Boeing 737-700,B737-700ER na B737-700c au Same model na different Generation,mfano Boeing 737-700 New Genaration au MAX737 nk.

Kuna faida nyingi kwa shirika kuamua kuwa na ndege kutoka kampuni/mzalishaji mmoja kuliko kuwa na shirika lenye ndege kama "kachumbari".Yaani shirika l moja kama ATCL lina ndege kutoka Bombardier,Boeing na Airbus.Huu ni mseto unaotishia ukuwaji wa shirika kibiashara na kiutaalamu.Faida kubwa ni kuwa mnapunguza ghalama za ku-train marubani na pia kupunguza ghalama za maintanance.

Mpaka sasa ATCL imeleta ndege aina ya Bombardier,na hatukuwa na marubani wa kurusha aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa darasani,hatukuwa na wahandisi wa aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa pia darasani kufungua modules za Q400.Na hata sasa,bado tumeazima wahandisi toka Zimbabwe na Malawi walio na uzoefu wa kuhudumia ndege hizo.

Hii ni kusema hata sasa shirika kama ATCL linatakiwa lijizatiti lenyewe kwa kuwa na wahandisi wake na si wa kuazima na marubani wake na si wa kuazima,ile ile dhana ya kuongeza faida na kubana matumizi itimie.Kenya na "vurugu" zake katika usafiri wa anga,Dreamliner zimawatia adabu.Hao Ethipia wana Dreamliner kadhaa,lkn mpaka sasa mainnjia na marubani wa ndege hizo ni kutoka nje ya Ethipia;yaani wanakodi kuanzia Pilot in Command,First Officer na Injinia.Hawajwa na mainjinia walio "certfied" kuigusa na kuikarabati Drwmliner...

Kumpata rubani Tanzania hii mwenye masaa(rating) ya kuendesha Dreamliner sio kazi ya mwaka mmoja,na kumpata injinia wa kuihudumia Dreamliner aliyekuwa certified siyo kazi ya mwaka mmoja.Ni safari ndefu.Haiwezekani rubani mwenye rating ya pangaboi aingie moja kwa moja kwenye dreamliner.Inahitaji muda na pesa.

Kununua tu hiyo "Flight Simulator" ya Dreamliner kwa ajili ya kufundishia marubani ni sawasawa na kununua bombardier nyingine.Mwisho wa siku,hizo ndege zikija,na kwa kiwango cha kimataifa tutakodisha kuanzia rubani mpaka injinia wa dreamliner sbb kuwapata wazawa itachukua muda mrefu kidogo.Wakati tunataka kurirudisha shirika angani,basi tungefuata "Fleet Commonality" ili baadae ndio tuingie kwenye hiyo "Cross Manufacturing".

Mashirika mengi yamefanya hivyo,Kenya imezingatia na inamiliki ndege aina moja za E170 na E190 pamoja na Boeing.Hii inawasaidia kuwa na marubani wenye ujuzi wa aina hizo za ndege na hivyo kuepusha ghalama,pia inasaidia sbb wanakuwa na injinia wenye leseni za E190 na hivyo kupunguza ghalama.Ethiopia yeye ameamua kuwa na Bombardier na Boeing tu.Kuanzia B737,735,767,777 na 738.Rwanda alichofanya amenunua Bombardier,Boeing na sasa Airbus na "amekodisha" marubani na wahandisi wote toka Ethiopia ili wamfundishie vijana wake kwa mkataba wa miaka 7.

Kutoka kuwa shirika "mfu" na kuacha kuzingatia "Fleet Commonality" ni kama tunarudi kulekule walikoshindwa waliotangulia.

Uliletwa uzi humu watu "wanalalamika" kuiona Pangaboi ikizunguka Dsm siku nzima badala ya kuanza safari za mikoani.Ile ilikuwa ni "Touches and Goes" ili wale marubani walioenda darasani kufanya kwa vitendo kabla ya kukabidhiwa.Sasa ikumbukwe mafunzo yake sio kama gari,kwamba unajifunza huku ukiwa na chombo.Kwenye ndege ni "Flight Simulator" ambayo baada ya kumaliza,ndio unapewa ndege huku ukiwa na instructor,na kukabidhiwa ndege ni hadi pale utakapoonekana umefudhu kweli(usije kuuwa watu)

Sasa hata kama tulipeleka marubani sita kwa maana ya pair tatu,basi hapo wenye uwezo wa kurusha ni watatu tu,huku hawa wengine wakitumia hata mwaka mzima kupata uzoefu na masaa ya kuwa pilot in command.Ghalama hizi zote tunaweza kuziepusha kwa kuzingatia "FLEET COMMONALITY" kwa kuwa na ndege za kampuni moja itakayotusaidia kuzalisha wahandisi namarubani walio certified kwa aina fulani ya ndege,kuliko kukimbilia kwenye "haterogenious fleet" itakayoongeza ghalama zaidi.

Tujifunze kwa LAM(Mozambique) walioamua kuwa na Boieng na E190,Kenya walioamua kuwa na Boieng na E190,Ethiopia walioamua kuwa na Boeing na Bombardier,South Africa Airways walioamua kuwa na Airbus na Boeing,Egypt Air walioamua kuwa na Boeing na Airbus.Hii "kachumbari" ya Pangaboi,CS300 na Dreamliner,inaweza kuturudisha kulekule tulipojikwaa.

Ni mtazamo tu;hatuisimangi ATCL
MKuu umenena vyema!
 
Maelezo yako yamejikita zaidi kwenye gharama za uendeshaji wa ATCL hasa kwenye "Employees remuneration ,Training cost" na "Maintenance and repair" kwa jinsi nilivyokuelewa.

Aina ya mfumo unaosema (fleet communality) kweli unasaidia kupunguza "costs" za uendeshaji lakini pia lazima uangalie pia uwezekano wake wa kuzalisha "Cash and cash equivalent over a long run","competitiveness" na "risks" za kutegemea mfumo moja mi nafikiri "diversification is the best option " kwenye kupunguza "risks" ,kupanua ujuzi wa kutoa huduma ya Anga kikamilifu na kuwa "competitive" .

Lazima gharama za uzalishaji ziwe juu tuu kwa ATCL kwenye hizi hatua za Mwanzoni za "Restructuring" hata kama ingekuwa inatumia "fleet communality", Mimi naamini costs hizi ( "Employees remuneration ,Training cost" na "Maintenance and repair" ) zitaendelea kushuka kwa jinsi kampuni litakavyokuwa likiongeza upanuzi wa huduma zake kwa "pricing policy" ambayo ni "competitive" kwa kutumia "competitive advantages" ilizokuwa nazo na kuiwezesha ATCL kuwa miongozo mwa makampuni ya umma litalochangia kwa kiasi kikubwa kipato cha Taifa katika miaka ijayo.

Article.
 
barafu ushauri muruwa mm naona kuna kutafuta sifa kama nimenunua ndege nzuri instead ya kusimamisha shirika maana atakuja na airbus kutusifia na pia tutanunua hebu tuwe makini madam nia rais kaonyesha aache wataalam wafanye yao

Huu upuuzi wao unakera, iweje ndege mpya kila kukicha ni hitilaf tuuu

Leo tena imefia arusha!!
 
Hivi jamani kwani kuna ubaya gani kuwa na Yutong,Scania,Higer na Zongthong Bus kwenye kampuni moja?

Sipati mantiki kabisa
 
Tatizo lako unaangalizia mpaka mwandiko.
Hivi unaelewa strategy za competition, hahaha kujipambanua kuwa tofauti na wengine ni advantages.

Siamini kama hoja elementary kama hazikufikiriwa mapema. Prof Mbarawa ni Engineer tena aliyebobea toka Majini mpaka Angani.

Hebu pia cambia za kuwa na dreamliner straight kutoka Detroit to Dar vs Boeing.

Tufike mahali tuwaamini watanzania wenzetu wafanye kazi tumeona nia yao.ni.nzuri.na kweli.wamekusudia kuinyanyua hii.nchi kiuchumi
Huwezi amini,ila baadae utaamini mambo yakianza changanyana.
 
sasa nyie mnatakaje? tatizo hamkuzoea mambo makubwa mlizoea tanzania iliyo shindwa kila kitu...unataka kuniambia serikali hawajui hayo? unadhani CEO wa ATCL hajui hilo....kwahiyo hasingenunua dreamliner unadhan bombardier wana ndege nyingine za masafa marefu kama boeing....kwahiyo tufanyeje tusilifufue shirika kisa gharama ni kubwa..husione vyaelea vyaundwa...ila katika vitu ambavyo magu hatutamsahau kama taifa ni kufufua ATCL.....ipo siku tutamkumbuka jamaa kafanya kazi kubwa mbona kikwete kwa miaka10 hata Q400 ilimshinda?
Kwani hujasoma anataka nini?Kwanini usianze kwa kuthibitisha serikali inajua na si kuja na maneno ya kufikirika kwa niaba ya serikali.hizi akili kwamba serikali inajua kila kitu ni akili ndogo sana,ndio maana hamna mchango kwa taifa.Serikali ingekuwa inafikiria na kujua kila kitu hii mizaha tunayoiona kila siku isingekuwa inatokea.
 
Barafu pamoja na kujaribu kufanya analysis yako ionekane ina mwelekeo, naona kama ina mambo mengi ya kujiuliza kuhusu hicho ulichokiita kachumbali. Rwanda Air wana boeing, Q400, na airbus, Ethiopia pia wana mchanganyiko huko huo. Air Tanzania wana Bombardier na wanategemea kuleta Boeing. Je nani ana fleet commonality? Biashara ya ndege imekuwa ikibadilika sana na kile kilichoaminiwa zamani sio lazima kuwa kwa mazingira ya kisasa kinaendelea kuwa ukweli. Kiukweli ushindani katika soko la usafiri wa anga kwa sasa linataliwa na uwezo wa ndege zako katika matumizi ya mafuta na uwezo wa injini . Ndio sababu kila mmoja anahama kutoka kabila moja ya ndege kwenda ingine kwa kuangalia ni ndege kabila ipi itampatia faida ya ushindani (competitive advantage). Swala la commonality katika mazingira ya sasa ni kama Lina kosa usahihi wenye uhakika na ndio sababu Ethiopia na Rwanda wamechanganya au wanakachumbali kubwa sana. Kwa ndege za mapanga zilizopo tanzania, Q400 imeonyesha kuwa na performance nzuri sana na hili si kwa Tanzania tu bali dunia ni kote. Hata hivyo ATcL lazima ajiulize ni soko lipi analolilenga na kama Q400 zitamwezesha kushindana. Jibu ni lazima afikiri nje ya Q400 kwa kutilia maanani kuwa kina Rwanda, Kenya, South Africa, na Ethiopia wako huko na wanatumia regional jet, boeing, airbus, embraer, nk. Hivyo ni lazima aliangalie soko kwa mtizamo huo pia. Kwa kigezo cha faida ya kiushindani Cseries inamfaa na sio Q400 maana ndio iko katika jamii ya regional jet! Angalia ni mashirika mangapi yameshawikika kununua cseries na sababu ni ipi. Commonality ameendelea nayo maana bado yuko kwenye familia moja ya bombardier tofauti ni aina ya ndege. Commonality sio kutumia Q400 tu bali mtengenezaji mmoja. Kwa kufuata kigezo cha commonality, ATCL angefikiria pia kupata wide body (ndege kubwa) kutoka bombardier ili aweze kuwa na uwezo wa kushindana beyond soko la regional jet. Kwa bahati mbaya bombardier hana wide body hivyo ni lazima aende airbus au boeing kama anataka ajitanue zaidi kiushindani. Kwa kigezo kile kile cha kupata faida ya ushindani ameona boeing 787 ni bora kuliko airbus 330 au 350!
Naomba mnisaidie kunionyosha iko wapi hiyo kachumbali. Je Ukimfananisha ATCL na Rwanda au Ethiopia nani ana kachumbali? Je, faida ya ushindani kwa kuwa na commonality bado ipo katika mazingira ya sasa ukiangalia swala la mafuta na engine performance? Nisaidieni kujibu.
Ndio maana mkuu NOD RwandAir mpaka sasa ndege zake zooote za Bombardier zipo chini ya Ethiopia kuanzia Marubani mpaka wahandisi,na wameingia mkataba wa miaka saba wa kuhudumiwa na Ethiopia kwenye wahandisi na marubani.Sasa kwa maana ya kubana matumizi kama sera ya JPM ilivyo,na sisi tukiingia kwenye mfumo huu kwenye dreamliner,ina maana dhana hiyo inakuwa haifanyi kazi.

Ethiopia wana Bombadia na Boeing tu za kawaida,kwa maana ya B737,B738,B767,B757 na B777...,hii Dreamliner ni ETOPS,ndio maana hata wao wana uhaba wa mainjinia na marubani licha ya utabe wao ktk soko la usafiri wa anga.Sisi tungeweza kuanza na B737,B738 kabla ya kufika kwenye Dreamliner.Kumbuka rating ya dremliner sio ya kitoto mkuu

Note:Namuunga mkono JPM na suala lake la kuifufua ATCL,mjadala huu si nia ya kuikatisha tamaa ATCL,ni mawazo tu ktk kuchangia mjadala juu ya ufufuaji wa ATCL...
 
HELA YA KUNUNUNILIA NDEGE NI kodi yetu sote waTZ, watakaopanda ni wachache sana, je siingekua muhimu kushughulikia matatizo ya maji huko vijijini na hata hapa Dar, maeneo mengi sana hayana maji safi na salama kuliko kununua hizo ndege. ATCL ingeuza mali zake nyingi zilizo nchi nzima kama maofisi na majumba mengine ili kupata mtaji wa kununulia ndege au wakakope kuliko kutumia kodi zetu wote kwa ajili ya wachache, haya ni maamuzi ya nani? au Mtu mmoja tuu, kwa ajili ya sifa za kushindana na Rwanda na Kenya?
 
Maelezo yako yamejikita zaidi kwenye gharama za uendeshaji wa ATCL hasa kwenye "Employees remuneration ,Training cost" na "Maintenance and repair" kwa jinsi nilivyokuelewa.

Aina ya mfumo unaosema (fleet communality) kweli unasaidia kupunguza "costs" za uendeshaji lakini pia lazima uangalie pia uwezekano wake wa kuzalisha "Cash and cash equivalent over a long run","competitiveness" na "risks" za kutegemea mfumo moja mi nafikiri "diversification is the best option " kwenye kupunguza "risks" ,kupanua ujuzi wa kutoa huduma ya Anga kikamilifu na kuwa "competitive" .

Lazima gharama za uzalishaji ziwe juu tuu kwa ATCL kwenye hizi hatua za Mwanzoni za "Restructuring" hata kama ingekuwa inatumia "fleet communality", Mimi naamini costs hizi ( "Employees remuneration ,Training cost" na "Maintenance and repair" ) zitaendelea kushuka kwa jinsi kampuni litakavyokuwa likiongeza upanuzi wa huduma zake kwa "pricing policy" ambayo ni "competitive" kwa kutumia "competitive advantages" ilizokuwa nazo na kuiwezesha ATCL kuwa miongozo mwa makampuni ya umma litalochangia kwa kiasi kikubwa kipato cha Taifa katika miaka ijayo.

Article.
Hasa kwenye *pricing policy*, mfano ATCL from Mwanza to Dsm kama ukitaka kusafiri January unatakiwa ulipe 180000 lakini mshindani wake mkuu ni 120000, so automatically hapo kwa mtu asiye wa serikali ambaye anajilipia sio kulipiwa na serikali lazima atachoose low cost.....So yanaweza jirudia yaleyale na ndoto ya JPM ikashindwa kukamilika kwa kulipia ticket sh 70000....
 
Back
Top Bottom