Kweli Maandamano na Migomo ndiyo SULUHISHO ya matatizo yetu? Nini kifanyike?

FairPlayer

JF-Expert Member
Feb 27, 2006
4,145
716
Wakuu,

Ni muda sasa toka nianzishe mada yoyote hapa JF. Sababu zipo nyingi ila kubwa ni kukosa muda.

Hivi kweli migomo ya mara kwa mara ndio suluhisho la matatizo ya wafanyakazi au wanafunzi au wafanyabiashara? Kwanini kusiwepo na sehemu au taasisi inayojitegemea kwa ajili ya kupelekea malalamiko yako?

Maandamano ya vyama vya siasa. Maandamano hata yakiwa ya amani lazima kuna vibaka wanajichomeka mle ili mradi wapate riziki zao.
Hivi hakuwezi haki kupatikana bila maandamano?, kwanini kusiwepo chombo ambacho ukitaka kuandamana au kugoma unapeleka maombi yako kisha polisi wanaitwa mnapingana kwa HOJA kisha hicho chombo kinaamua kuwa muandamane au hapana?

Jamani naomba mawazo yenu ya nini tufanye. Kwa mwendo huu wa sasa tutaanza kupoteza maisha ya watu kwa mambo yanayotatulika.

Asanteni kwa kuchangia positively.
 
Naona wachangiaji hamna. Hatutaki suluhisho tunataka CCM iondoke madarakani bila kujali kama ni wazuri au watajirekebisha au la.
Hii ndo naita siasa uchwara.
Poleni Mbeya, Udsm na Arusha. Kwa speed hii hatutofika
 
Kikubwa sio taasisi au jukwaa la kusuluhisha,kwanini nasema hivi.. kwa hali ilipofikia Serikali haiko tayari au kwa makusudi au bila kujua kushughulika na matatizo ya raia wake katika sehemu kwa wakati muafaka na sidhani kama wanaoandamana wanakuwa hawajapitia hatua zote muhimu mpaka wakafikia kuamua hayo.
Suala je maandamano ni halali au sio halali? yawe ya kisiasa,kidini au kinamna yoyote ile? kama jibu ni ndiyo kwanini iwe ni haramu kwa kundi lolote lile linalotaka kuandamana kufanya hivyo na Jeshi la Polisi likatekeleza wajibu wake wa kulinda amani na usalama..Ni upotevu wa fedha na muda kama hiyo taasisi ikifia mahali ikaanzishwa bila kwanza watendaji wa serikali kuacha kujipendekeza na kuweka unafiki nyuma wakaacha sheria,kanuni na taratibu za nchi zichukue mkondo wake ama sivyo tutakuwa madikteta bila ya kujua na raia wanaweza kuamua vinginevyo..
 
Fair Player, maandamano ndio suluhisho!. Tuendelee kuandamana mpaka 2015. Yatatungiza hadi Ikulu kama Misri na Libya!.
 
Pasco,

Angalia niliandika hii mada November mwaka jana. Wiki mbili mpaka sasa madaktari wanagoma. Waziri husika anapiga danadana katibu mkuu wa wizara naye kama kalogwa. Waziri mkuu naye anakurupuka.

Hivi hii serikali imelogwa?

BTW: umeona jamaa wameanza kuigilizia style yetu ya makanisani? nao wameanza, yaani sio wabunifu kabisa. Halafu wanaleta picha mbaya....

mwingine naye akiibukia msikitini sitoshangaa.

Ama kweli ....
 
Maandamano na migomo si suluhisho la matatizo yetu BALI ni NJIA ya kuyafikisha kwa nguvu matatizo yetu ili yaanza kutafutiwa ufumbuzi. Ni njia sahihi kabisa ya kudrtaw attention kutoka serikalini au kwa watu husika hasa wasiokubali mazungumzo ya kidiplomasia
 
Inasikitisha na inauma kusema kuwa Tanzania hatuna viongozi bali watawala, tena watawala wenyewe ni kama wanyapara wa kikoloni. Wao wanafikiria kuwa ufumbuzi wa matatizo yetu ni kwa kuwanyamazisha watu midomo kwa vitisho, kufukuza watu kazi, kutumia nguvu za dola katika kunyamazisha watu kwa mtutu na maji ya kuwasha, kumjadili mtu badala ya kujadili tatizo na kulipatia ufumbuzi.

Tatizo zaidi ni kuwa hawajifunzi kutokana na uzoefu wa matukio ya nchi nyengine wala kwa nyakati tunazokwenda nazo. Inapofikia wakati ikawa wananchi hawana matumaini, hawana cha kupoteza zaidi ya maisha ambayo kwao hayana thamani tena, wanaweza kufanya lolote. Mnakumbuka mwanafunzi mhitimu wa Tunisia aliyejiripua baada ya polisi kumzuwia kufanya umachinga wakati alikuwa hana kazi yoyote ya kumpatia riziki? Mnakumbuka watoto wadogo wa Palestina wanaotumia mawe kupambana na mtutu wa bunduki za Israeli? Mnakumbuka vurugu za mwaka jana Uingereza, Italia, Ugiriki, Ufaransa, Occupy Wall Street?....yalitokea hayo na yataendelea kutokea kwa sababu viongozi badala ya kuwasikiliza wananchi, wanavisikiliza na kuvinufaisha vyombo vya fedha na wawekezaji na sio wananchi wao.

Utamwambia nani akuamini kuwa serikali haina pesa wakati wabunge wanaongezwa posho, viongozi wanasafiri kama masaburi yanawauma kukaa nchini kwao, wanatibiwa India na kwengineko wakati wananchi wanashindwa kupata huduma za msingi za afya...?

Ni kweli migomo na maandamano sio suluhisho la mwisho, lakini kwa kuwa hakuna suluhisho lolote, migomo na maandamano ndio suluhisho pekee.
 
Back
Top Bottom