Kweli Lowassa alikuwa smart Sana, hii serikali ya awamu ya tano imeanza kuwanyang'anya wananchi Mali zao Kwa ajili michango ya ujenzi wa shule.

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
2,050
3,658
Hapo vip!!
Leo nimekutana na wananchi wanaotokea wilaya ya Arumeru wakililamika migambo kuvamia katika Nyumba zao na kuchukua Mali, Kwa madai ya kushindwa kulipa michango ya ujenzi wa shule ya shillingi elfu 25.

Nakauli mbiu ya hao Migambo ni kwamba michango lazima, vinginevyo hata kitanda watakiuza.

Anyway, sipingani na mpango Wa kujenga shule lakini kwa serikali hii inayokusanya kodi Sana mbali na kodi kuna vyanzo vingi vya kupata pesa, Kwa nini inawafilisi wananchi wake. ..?

Isitoshe serikali hii imesababisha maisha magumu kwa wananchi, kuanzia katika maeneo ya biashara (hakuna mzunguko wa pesa), hakuna ajira n. K

Leo inamtaka huyu mwananchi aliyekosa ajira, mwananchi ambaye biashara yake imefilisika kutoka na kuyumba Kwa uchumi wa Nchi...alipe mchango tena Kwa lazima.

Hivi Lowassa aliwezaje kujenga shule za Kata pasipo, kuwavamia wananchi na kuwanyang'anya Mali zao..?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom