Kweli leo ni siku ya wajinga..........soma hii kutoka Habari Leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli leo ni siku ya wajinga..........soma hii kutoka Habari Leo

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Rutashubanyuma, Apr 1, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Babu wa Loliondo kutoa vikombe Jangwani

  Imeandikwa na Waandishi Wetu, Dar na Loliondo; Tarehe: 31st March 2011 @ 23:30 Imesomwa na watu: 253; Jumla ya maoni: 0
  MCHUNGAJI Ambilikile Mwaisapile ‘Babu’ ametua Dar es Salaam kutoa huduma yake ya tiba ya kikombe kwa muda akisubiri eneo lingine kubwa zaidi aliloahidiwa na Serikali.

  Babu aliwasili Alhamisi asubuhi kwa helikopta akitoka Loliondo ambako utoaji tiba umesimama kwa muda na Ijumaa atakuwa akitoa kikombe katika viwanja vya Jangwani ambako alisema nafasi ni pana zaidi.

  Tofauti na Loliondo, Jangwani Babu ameweka vituo vipatavyo 10 ambako hadi usiku wa kuamkia leo, askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakishirikiana na watumishi wa Chama cha Msalaba Mwekundu walikuwa wakiendelea kusimika mahema.

  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili jana alasiri, Babu alisema, amefarijika kwamba ataweza kusaidia hata ambao walikuwa hawana uwezo wa kufika Loliondo.

  “Nadhani nitawasaidia wengi ambao hawakuwa na uwezo wa kufika Loliondo, lakini bado nasema wagonjwa mahututi waendelee kubaki hospitalini na wenye Ukimwi waendelee na dawa walizopewa hasa ARVs,” aliasa Babu.

  Kwa muda mrefu Babu amekuwa akitoa huduma zake katika kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro, Arusha ambako umati wa watu na misururu ya magari yanayokwenda huko, uliharibu mazingira hasa katika kipindi hiki cha mvua za masika.

  Kuharibika huko kwa mazingira kulisababisha baadhi ya magari kukwama na mengine kupata ajali jambo lililochangia ongezeko la vifo vya wagonjwa wanaokwenda kupata dozi na kutishia uwezekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko na kuongezeka kwa vifo.

  Akizungumza jana na gazeti hili kuhusu masuala ya ulinzi na usalama wa eneo hilo leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema utakuwa imara na askari 200 wanatarajiwa kutumika kwa kazi hiyo na kuwataka wananchi wasiwe na wasiwasi.

  “Barabara zinazokwenda Loliondo kutoka Arusha kupitia Mto wa Mbu, Monduli na kwenye hifadhi ya Ngorongoro wakati wa mvua hazipitiki. Hata barabara zinazotoka kwenye maeneo ya Bunda na Mugumu kwenda katika mji huo pia hazipikiki wakati mvua,” alisema Msaidizi wa Babu ambaye alikataa kutajwa jina.

  Jana Babu na alisafirishwa kwa helikopta ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na leo atatoa huduma yake katika viwanja hivyo ili kutoa fursa kwa wagonjwa wengi kupata tiba hiyo bila kuharibu mazingira na miundombinu.

  Pia Serikali imezuia magari yote yanayokwenda katika kijiji hicho na sasa wametakiwa kwenda Dar es Salaam kupata huduma hizo na ili kupunguza idadi ya vifo, tayari Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeanza kujenga zahanati ya muda kusaidia wagonjwa watakaozidiwa.

  Hata hivyo uamuzi huo wa Babu umeshutumiwa na watu waliokuwa katika foleni kusubiri kikombe na wametishia kuandamana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kupinga uamuzi wa Serikali kumsaidia Babu kutoa huduma Jangwani.

  Lakini mmoja wa wasaidizi wa Babu ambaye alizungumza na gazeti hili alithibitisha kuwa uamuzi wa Mchungaji huyo kuhamishia huduma zake Dar es Salaam kwa muda ni kutokana na kuongezeka kwa maombi ya watu na Serikali.

  Msaidizi huyo alisema watu wengi hawana uwezo wa kwenda Loliondo kutokana na wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kujitajirisha kwa kutoza nauli kubwa inayofikia Sh 200,000 kutoka Arusha jambo ambalo watu wengi hawana uwezo nalo.

  “Kama sasa hivi tu nauli iko aghali ina maana wakati wa masika itaongezeka zaidi, ndiyo maana tumeshauriwa kuhamishia huduma hii kwa muda Dar es Salaam,” alisema Msaidizi huyo.

  Habari za kuaminika kutoka serikalini, zilieleza kuwa mti ambao unatumika kama dawa utaendelea kuchimbwa eneo hilo la Samunge na kusafirishwa kwa helikopta za JWTZ hadi Dar es Salaam.

  “Serikali itatuma helikopta ambayo itatua Waso ambako kuna uwanja wa ndege ambao umekuwa ukitumiwa na viongozi wa kiserikali ambao wanaenda kutibiwa Samunge,” kilisema chanzo chetu cha habari.

  Mmoja wa wagonjwa ambao wanajiandaa kuonana na Babu leo alipotaka kujua zaidi kwa nini Mchungaji huyo amehamia Dar es Salaam ghafla, Msaidizi huyo wa Babu alimjibu : “Leo ni siku ya wajinga duniani”.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu magazeti ya serikali ....should stay away from this nonsense........................................
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Apr 1, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nadhani siyo magazeti ya serikali tu, magazeti serious yangeachana na hiyo 1st April fools day wayaachie yale ya udaku. Leo magazeti serious yamejaa udaku wa 1st April Fools days. Mara TP Mazembe haiendi dar kucheza na simba, mara Lionel Mess yupo Samunge akipata kikombe, nk. Huu utani si mzuri kwa magazeti serious
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  Serikali ya wajinga na waandishi wajinga wasiojua ethics unadhani watafanya nini zaidi ya ujinga? Thats why huwa sisomi Habari Leo
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hizi habari za siku ya wajinga zingefaa katika magazeti ya udaku!
   
 6. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  well said,,,bora ingekuwa yale ya udaku,,,too low
   
 7. G

  Gathii Senior Member

  #7
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nafikiri tunapaswa kujiuliza ni mantiki ya siku ya wajinga?
  Obviously ni kitu tulichokopi toka kwa wazungu,lakini kwani ni lazima tukopi kila kitu?-ni kweli kuna vingi vyenye manufaa hivyo na tuviige kwa maendeleo yetu,hii ya 1st April Fool's day sidhani kama ina lolote la kutusaidia.
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Apr 1, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hivi na hawa TBC na wao wanajiunga na ujinga huu wa siku ya wajinga kwa kuwadanganya watanzania kuwa TP Mazembe haileti timu Tanzania kupambana na Simba. Nilikuwa naiheshimu stesheni hii lakini sasa naanza kuidharau!
   
 9. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hata isiwe siku ya wajinga mie huwa siyaamini haya magazeti :disapointed::disapointed::disapointed:
   
 10. s

  sawabho JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Nimesikia kuptia Nipashe Redio One: SMZ imekodi ndege maalum kumpeleka Babu huko ZNZ kuanzia saa moja asbh hadi saa 3.30 ili atoe dawa muda huu. Nikjiuliza, huu si udaku!! Sasa inakuwaje vyombo vya habari makini navyo viingie kwenye udaku kama huu. Je, kama kukitokea jambo la kweli katika muda huu waatawanishaje wasikilizaji?
   
 11. wapalepale

  wapalepale JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 33
  Ni kweli kabisa yaan leo kila habari inanitia mashaka ila afadhari hao redio one maana mwishoni wakasema mwisho wa huduma ni saa 3.30 asubuhi, hivyo mtu akijiuliza kwa makin atagundua kitu
   
 12. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Walichikifanya leo ndio kinaonyesha kwamba wao ni mahiri wa kutunga story hata kama sio April Mosi.
  Ukisoma hiyo habari imepambwa utafikiri ni ya kweli, so disappointing really!
   
Loading...