kweli kwa jeshi la polisi hii ni aibu mno!

mcrounmj

JF-Expert Member
Feb 26, 2016
380
889
waungwana wa jukwaa hili mu buheri wa afya?

Kama kawaida harakati za maisha natumai zinaendelea. Jukwaa hili limekuwa msaada mkubwa wa kufikisha kero zetu huku uraiani kwa viongozi wenye dhamana, na hivyo kupata utatuzi wa haraka.

Leo nazungumzia biashara haramu ya dada zetu kuuza miili yao, jina maarufu kama madada poa. Ni karibia maeneo yote ya nchi yenye miji mikubwa biashara hii imeshamiri, licha ya jeshi la polisi kuonyesha juhudi zake za kuzuia. Kumekuwa na matamko kutoka kwa viongozi wakuu wa nchi akiwemo waziri wa afya, Ummy Mwalim kuagiza jeshi la polisi kuhakikisha biashara hii ya machangudoa kujiuza inakomeshwa. Ukweli ni kwamba imeshindikana kwani muda umeshapita na bado kwenye miji yetu hawa madada poa wamejaa tele.

Sitaki kuwalaumu polisi pengine wanayo majukumu mazito ya kuyashughulikia ukiacha la madada poa. Ila lawama hii hawataikwepa jeshi la polisi mkoa wa Tanga! Biashara ya madada poa katika jiji la Tanga na viunga vyake, inafanyika maeneo matatu makuu, ila kunalo eneo moja panaitwa forodhani au jina jingine chichi. Kwa yeyote mwenyeji wa jiji hili la Tanga, hili eneo la forodhani ni maarufu sana, likiwa limezungukwa na Maktaba ya mkoa na jengo la wizara ya mambo ya ndani ya nchi, yaani ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi mkoa, RPC.

Ukipita mida ya saa mbili usiku utawaona madada poa wakiwa wamevalia nusu uchi wakifanya ukahaba, kando ya barabara mita pungufu ya kumi kutoka kwenye milingoti ya bendera ya taifa na bendera ya jeshi la polisi iliyo mbele ya jengo hilo, huu ni udhalilishwaji kwa jeshi letu la polisi. haiwezekani katika kituo kikuu cha polisi mkoa, kinacholindwa na polisi wa dolia tena wakiwa na siraha za moto kukafanyika upuuzi huo.

Na hii haijaanza leo wala jana ila ni muda mrefu, mamlaka husika chumkueni hatua kuwanusuru vijana wa Tanzania.
 
Niliwahi kupita Kaumba nikihisi naoita Sodoma au gomora
Pale hatari sana!
Na zile salon Barbershop zilizo pale karibu baada ya kunyoa, muda wa kuoshwa sasa...Dada zetu lazima wakuambie "kuna Biashara nyingine, Vipi unataka!?"
 
waungwana wa jukwaa hili mu buheri wa afya? kama kawaida harakati za maisha natumai zinaendelea.
Jukwaa hili limekuwa msaada mkubwa wa kufikisha kero zetu huku uraiani kwa viongozi wenye dhamana, na hivyo kupata utatuzi wa haraka.
Leo nazungumzia biashara haramu ya dada zetu kuuza miili yao, jina maarufu kama madada poa. Ni karibia maeneo yote ya nchi yenye miji mikubwa biashara hii imeshamiri, licha ya jeshi la polisi kuonyesha juhudi zake za kuzuia. Kumekuwa na matamko kutoka kwa viongozi wakuu wa nchi akiwemo waziri wa afya, Ummy Mwalim kuagiza jeshi la polisi kuhakikisha biashara hii ya machangudoa kujiuza inakomeshwa. Ukweli ni kwamba imeshindikana kwani muda umeshapita na bado kwenye miji yetu hawa madada poa wamejaa tele.
Sitaki kuwalaumu polisi pengine wanayo majukumu mazito ya kuyashughulikia ukiacha la madada poa. Ila lawama hii hawataikwepa jeshi la polisi mkoa wa Tanga! Biashara ya madada poa katika jiji la Tanga na viunga vyake, inafanyika maeneo matatu makuu, ila kunalo eneo moja panaitwa forodhani au jina jingine chichi. Kwa yeyote mwenyeji wa jiji hili la Tanga, hili eneo la forodhani ni maarufu sana, likiwa limezungukwa na Maktaba ya mkoa na jengo la wizara ya mambo ya ndani ya nchi, yaani ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi mkoa, RPC. Ukipita mida ya saa mbili usiku utawaona madada poa wakiwa wamevalia nusu uchi wakifanya ukahaba, kando ya barabara mita pungufu ya kumi kutoka kwenye milingoti ya bendera ya taifa na bendera ya jeshi la polisi iliyo mbele ya jengo hilo, huu ni udhalilishwaji kwa jeshi letu la polisi. haiwezekani katika kituo kikuu cha polisi mkoa, kinacholindwa na polisi wa dolia tena wakiwa na siraha za moto kukafanyika upuuzi huo. Na hii haijaanza leo wala jana ila ni muda mrefu, mamlaka husika chumkueni hatua kuwanusuru vijana wa Tanzania.
Taja sehemu 2 zilizo baki, wenyeji tunakazi nazo
 
Miaka ya 80 Mwalimu alishawahi kudokeza kwamba, biashara hii ni ngumu mno namna ya kuizuia...!! watu wawili kuuziana vipande vya miili yao, je unaanzaje kuwathibiti?
 
hayupo wa kuangamiza hii biashara isipokuwa mungu.

Wanatupunguzia stress za wake kutunyima kwa kisingizio cha hawajisikii au kuchoka. kumiliki mchepuko ni pasua kichwa kwa mizinga. Bora unaandaa elfu 3 kila wiki ya kupozea rungu
 
Back
Top Bottom