Kweli huyu ni mtetezi wa wanyonge?

Aputwike

Senior Member
Aug 9, 2016
170
250
Alijinadi kila sehemu kuwa atakuwa kiongozi wa wanyonge. Alisema hatavumilia kuona masikini wakiteseka. Pale jangwani aliongea maneno mengi kuliko hata nywele nyeupe. Alijitanabaisha kwa kutengeneza ajira lukuki, kwa kufanya watumishi waishi vizuri n.k.

Alisema yeye hatakuwa wamichakato, yeyote atakaye sema yupo kwenye mchakato; atachakatia pembeni. Alisema wanafunzi hawatasumbuliwa mikopo.

Sasa najiuliza. Mbona ajira ulisitisha kwa miezi miwili, hatimaye ikawa zaidi. Leo hii huyu mama anasema mtaajiri walimu wa sayansi tu, tena kwa masharti ya kutuma vyeti hapo mkijua wengi wao hawatatuma kwani si watakuwa walijiunga shule za binasfi ili msiajiri wengi kupunguza mzigo. Sasa yale maneno mengi ya jangwani kumbe ni nini sasa?!!! Naona makada fulani wananeemeka tu kwa mishahara ya kodi zetu, nikuteuana tu.

Au siye maskini ndio tuliokuwa tunaishi kama malaika? Maana tunaishi kama mashetani sasa, tena zaidi ya mashetani, tunaishi kama mizimu.

Au siye masikini ndio tulikuwa wapiga dili? Maana tunaona heri ya jana.

Huyu mama bado simuamini, inamaana zile ajira 71,000 zilizokuwa zinatangazwa Mara kwa Mara sio kweli? Naamini zitamwagwa kwa mbwembwe na vifijo kama ilivyokuwa kwa baba Lidhi. Wanaosema eti kaya haina hela hapa ndio pakuwashika uongo wao, kwani zitamwagwa na watumishi kupandishiwa mishahara hadi wabaki midomo wazi.
 

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
5,067
2,000
Natamani nipate nafasi nimuulize mkuu una mkakati gani wa kupambana na umaskini ukiondoa msemo wa uchumi wa viwanda.
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Ukiishaona mtu mmoja tu ndiyo anajifanya ana akili kuliko wengine wote ujue huyo mtu ana tatizo kubwa sana, kwa sasa wenzake wanamuangalia tu
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom