Kweli huyu mpenzi wangu ananipenda kwa dhati?

kagarara

Senior Member
Nov 23, 2010
118
9
Mm nina mpenzi wangu ambaye kwa kweli nampenda sana, yeye mwenyewe ameshanitambulisha kwa ndugu zake wote na anasema ananipenda, je ndugu zangu nitumie kipimo gani kujua kama ananipenda kweli?
 
kuwa nae karibu kila wakati ukimaliza kazi ofisini, week end n.k ukifanikiwa kwa hilo angalia simu yake kama iko muted, au anazima au hapokei simu zingine nk.

ila umenishangaza kuonyesha kama humwamini
 
Jitahidi kufanya uchunguzi wako, ili uridhike na maneno yake. Mapenzi ni ya watu wawili, na hatujui amekupendea nini; na wewe pia umempendea nini!!!
Take time!! mapenzi si ya siku moja hasa kwa ambaye unataKA awe mwandani wako milele... BE CAREFUL IN LOVE
 
omg,,,,u have to trust her the way she loves u ndo maana mapenzi ya sasa hua hayadumu wallah si kwa wakike wala wakiume only thing u have to do for both of u to trust each other no way out,,,nawaombea mapenzi ya kheyr na yenye barka,,,
 
Muamini mwenzio kaka. Wala haina haja ya kumchunguza chunguza. Bata ukimchunguza sana..?
 
kwa vigezo vile unavyotumia kuona anakupenda sasa vigeuze (Negate) halafu uvifanyie utafiti
 
omg,,,,u have to trust her the way she loves u ndo maana mapenzi ya sasa hua hayadumu wallah si kwa wakike wala wakiume only thing u have to do for both of u to trust each other no way out,,,nawaombea mapenzi ya kheyr na yenye barka,,,

akhsante sana, na ninashukuru kwa sala zako.
 
omg,,,,u have to trust her the way she loves u ndo maana mapenzi ya sasa hua hayadumu wallah si kwa wakike wala wakiume only thing u have to do for both of u to trust each other no way out,,,nawaombea mapenzi ya kheyr na yenye barka,,,

nashukuru sana mpendwa kwa sala zako na mwenyezi Mungu akujalie
 
Muamini mwenzio kaka. Wala haina haja ya kumchunguza chunguza. Bata ukimchunguza sana..?

Najua ndugu bata ukimchunguza humli lkn huoni kwamba nisipochunguza zaid mtu ambaye nategemea kumuona nitakujalia?
 
kuwa nae karibu kila wakati ukimaliza kazi ofisini, week end n.k ukifanikiwa kwa hilo angalia simu yake kama iko muted, au anazima au hapokei simu zingine nk.

ila umenishangaza kuonyesha kama humwamini
Ikiwa unampenda na yeye kasema anakupenda INATOSHA. Hilo la kuwa pamoja naye litazidisha mapenzi yenu, lakini tafadhali, jaribu kumwamini bila ya kumchunguzachunguza, si katika simu yake, mkoba wake wala emails zake. Kumbuka kuwa "atafutaye hakosi" na wewe kama utaanza kumtafutafuta hutakosa kasoro zake, lakini yoyote utakayoyaona yatatokana zaidi na kutomwamini kwako kuliko ukweli wenyewe. Kumbuka kuwa kutoaminiana na wivu ni adui wa mwanzo wa mapenzi. Kadiri atakavyohisi kuwa unamwamini ndipo atazidi kukupenda kuliko kuanza na mguu mbaya tangu mwanzo kwa wivu na upekuzi wa kipuuzi. Mwachie uhuru wake ili kulinda uhuru wako na nyote lindeni mapenzi yenu.
 
Najua ndugu bata ukimchunguza humli lkn huoni kwamba nisipochunguza zaid mtu ambaye nategemea kumuona nitakujalia?

hakuna aliyekamilika. Lazima utakuta ka weakness kaka. Mpe uhuru bwana huku ukimsisitizia kuwa makini. Unaweza ukamchunguza kwa mapenzi mwenzio akaona kero. Kama unataka kuchunguza chunguza pale unapoona kuna tofauti sio mambo yapo shwari we unafukunyua tu. Mabinti hatupendi hizo, utakosa mke bure.
 
Back
Top Bottom