Kweli Huu ni Uungwana? CV inang'ara, kiingereza kinavutia, kwenda kwenye interview aibu...

mzee hapo mzigo nakubebesha ww...
hata hizo dk chache ulizopata kuwa nae hukuweza kuusoma uelewa wake???
afu ndo ufananishe na hiyo cv??
lazima ungekua na walakini...
labda km hamkuongea kabisa...
af ni wakike au wakiume.?
ili tusihangaike sana.

Sikuwa naye ni email tu!
 
kuna wtu hawajui kuitwa kwenye interview tu ni jambo kubwa sana .wanachukulia tu rahisi maana kaunganishiwa.kuna mtu nilishamuunganishia mahali kiukweli yule binti ni mrembo lakini alivovaa tu siku iyo kama anaenda sokoni.nikamuuliza kwani vp hv na unazo nguo kibao? bahati nzuri akatoswa toka siku iyo kuunganishia watu nimekoma
interview ni zaidi ya kupata kazi watu hawajui.hamna kitu naogopa kama interview.kumbuka ile ndo inaamua maisha yako ndo inakufanya uwe mahali flani.ndo inakutoa ulipo ikuweke pale.toka unavoingia kwenye chumba cha interview haijalishi umefika vp pale lazima uhakikishe umewaridhisha wale ,mapanelist
mimi nilishawai kufanya interview shirika moja mwanza huko bahati nzuri baada ya kule nilifanya tena dsm nikapata kazi zote kule mwanza nikawaambia hao wazungu sitoenda yaani aliniandikia mail kibao akinibembeleza.reason ni tu nilivofanya nao ile interview sio lazima ujue kila kitu.kuna watu wanaboa toka anavojitambulisha.na dhani hii issue ya umoja wa africa mashariki itatuathirio sana watz sijui tutatoka vp
pole mwanakijiji
 
Ndio matokeo ya elimu yetu hayo kijana anatoka University of Dar Es Salaam , BA Journalism ame graduate na grade nzuri lakini masikini hata kuandika sentensi moja au kuongea kizungu sentensi mbili hajui. Unajiuliza alimaliza vp chuo?? na hiyo HGL alisoma vp?
 
Pole sana mmjj,ndio elimu zetu kibongo bongo na style ya kubebena ndio imeshika kasi kwan huku maofinin kuna watu wengine mpaka unajiuliza wamepataje hizi position!!

Ninachosikitika ni kwamba huyo mtu keshawaharibia na wengine ambao labda kwa namna moja au nyingine wangehitaji msaada wako na wanajiweza hasa,lkn kutokana na hilo hutokuwa tayari kuwasaidia tena!
 
inawezekana ajua fresh tu kimombo, ila siku hiyo hakupiga valuu wala konyagi ndo maana kikampotea kidogo kutokana na panic yakutoamini kuitwa kwenye international organization.
 
Hiyo ni kweli saaana. Wanawaharibia wale wenye potentials za ukweli.

Je huyu ambaye amekwenda kwenye interview na akaonyesha kuwa anafaa na akapewa siku ya kuanza kazi. Anakuja mtu mwingine ana anza kutoa masifa mabaya ya uongo juu ya mwenzie alie pata hiyo nafasi. Jamaa anakwenda kuanza kazi, ana ambiwa; Tutakupigia simu. Usiwe na wasi wasi. Huku unamona mwenzio kakaa kwenye kiti chake. Hana la kufanya ila kuondoka na kuhuzunika.

Vyote hivi vipo na vinavunja moral za wenye uwezo na unakuta wana ajiriwa watu ambao not compitant.
 
Hichi kisa kimenigusa sana kwani ndivyo inavyotokea mara nyingi.
Na hii inatokana na kutaka kwetu "bora elimu" kuliko "elimu bora".
Kila mwaka wazazi na wanafunzi wanalalamika kufutiwa mitihani
kumbe wanakopia mpaka nambari ya "Candidates Number". Kuna
rafiki yangu mmoja aliniambia alimsaidia mwanafunzi F6 kujibu swali
la "Ufahamu" kwenye "paper" ya Kiswahili; akamwandikia katika
kimemo "the answer is at paragraph three lines 4-7". Yule
mwanafunzi kakopia sentensi ileile kujibu swali la Kiswahili.

Visa kama hivyo Mkuu ni vingi tu. Mtu anadai kazi fulani yeye
ni mtaalamu na unaweza amini kwa CV yake, ukimwambia alete
vyeti halisi anaingia mitini.

Kwa mtindo huu, kama hatukubadilika kwanza "kiutamaduni" na
baadaye kubadilisha sera na mfumo wetu wa "bora elimu",
Watanzania wengi hatitafaa popote, bora tubakie nyumbani
tutendeleze majungu yetu, na wala sio EAC, AU au katika
mashirika ya kimataifa.
 
kingereza bila ujuzi ni porojo
st kayumba twende wapi?

Wa hapa hapa.
Na kuchoma sindano napo kingereza?
Kupima deep/strike napo kingereza?

Basi china wamebahatisha!
 
Huwa hata mimi nashangaa..wewe pitiapitia hata humu Jf uone baadhi ya watu tena wenye degree wanavyopangalia sentensi zao,hata kwa kiswahili tu ni balaa,na si mara moja au mbili.....halafu unajiuliza hivi kama kiswahili ni hivi je "kidhungu"?

Lakini usishangae anakuwa "supervisor" kwenye kampuni fulani..hata kuandika ripoti hajui.Nimewahi kuwa na rafiki yangu mmoja ambaye anafanya kazi kama mshauri mwelekezi (consultant) kwenye baadhi ya mashirika...hilo ni la kawaida,lakini la kustusha ni kwamba kazi nyingine inayomuingizia kipato ni kuwaaandikia wanafunzi wa masters degree dessertation na course work.Amini usiamini kwa wiki anafanya kazi za dessertation kama 3.

Sasa jiulize anafanya analysis saa ngapi? kama sio na yeye kukopi kazi za wengine kwenye internet?

Hapa ndipo tulipofika!!
 
Back
Top Bottom