Kweli Huu ni Uungwana? CV inang'ara, kiingereza kinavutia, kwenda kwenye interview aibu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli Huu ni Uungwana? CV inang'ara, kiingereza kinavutia, kwenda kwenye interview aibu...

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 1, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 30,761
  Likes Received: 4,131
  Trophy Points: 280
  HIVI KWELI HUU NI UUNGWANA? Umetuma maombi ya kazi na CV yako inawaka na kung'ara. Kiingereza chake safi na ujiko uliojipa unafanya CV isimame kati ya nyingi. Uliyemtumia anaona una "potential" anakuunganisha na taasisi ya kimataifa. Unaenda kwa interview Kiingereza kimevunjika vunjika kama sanamu ya udongo iliyoangushwa chini! Kumbe CV kakuandikia mama na kiingereza umeandikiwa. Huwezi kujieleza, kujitetea wala kujitutumua! Wakuu wanamfuata yule aliyekupigia debe "umetutumia kijana gani wewe"? Hivi kweli huu ni Uungwana? Unamfanya mtu na heshima zake kuonekana hamnazo!? Nimekomaaaa!

  Tunadhalilishana namna hii kwa kweli!
   
 2. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 11,351
  Likes Received: 2,761
  Trophy Points: 280
  Ni aibu. Ingawa pia ni fundisho kwako na watu kama wewe.
  Unapotoa recommendations kwa ajili ya mtu fulani ni vyema ukamfahamu fika. Ukafahamu uwezo na mapungufu yake. Ili kuepusha aibu kama uliyoipata.

  Umetoa recommendations za kumfit Wayne Rooney,kumbe ana kiwango cha John Boko!
   
 3. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ukimkuta Mbuzi mee yuko juu ya mti !
  Kapanda mwenyewe ?
  Haiwezekani !
  K a pa n d i s h w a.
   
 4. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,640
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280
  Pole sana,tatizo ulimwamini baada ya kuona CV zake bila kufanya uchunguzi.
   
 5. JS

  JS JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Pole Mkjj ndo binadamu tulivyo hatuna uungwana na tabia ya kusema ukweli au kuwa mkweli hasa sie Wafrika haipo kabisa mwishowe kutiana aibu tu. Ameharibia wengine ambao wangependa uwe reference yao.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 68,240
  Likes Received: 22,869
  Trophy Points: 280
  Mzee yamekukuta?
   
 7. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hehehe kama nakuona macho yalivokutoka,,ndo dunia hiyo.
   
 8. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,777
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji ngoja nikutumie cv yangu achana na huyo aliyekuaibisha..
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 30,761
  Likes Received: 4,131
  Trophy Points: 280
  Bangosha,karibu sana maana ulipotea kweli kweli. Unajua mara nyingi nasikia watu wanaulizia CV ya mtu na wakiiona imejaa vitu vingi basi kwao inakuwa "jamaa kichwa sana". Mimi si muumini sana wa CV lakini nilipoona ya huyu bwana mdogo wa miaka 20 hivi (imeambatanishwa na picha) nikajua this kid tunaweza kumuwahi mapema. Sasa jamaa yangu akajaribu kwenda kukutana naye na walipokaa kuzungumza hakuweza kutoa hata sentensi moja coherent ya Kiingereza.

  Napigiwa simu naulizwa "mzee huyu kijana mbona yupo yupo tu?"

  Well na miye ikabidi niruke futi nyingi tu!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 30,761
  Likes Received: 4,131
  Trophy Points: 280

  hahaha ah wapi! sidanganyiki tena; fool me once shame on you, fool me twice shame on me!
   
 11. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,603
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ulichokosea ni "kutominterview" wewe mwenyewe kwanza... Wala hapo hakuna wa kumbebesha lawama!
   
 12. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,603
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  ha ha ha .... Once beaten....,
   
 13. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,684
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mkjj, mi wala sikulaumu wewe, nailaumu society yetu ambayo imeondoa kabisa kujiamini kwa watu personally na badala yake imepandikiza mbegu ya kutaka 'kuonekana' bora hata Kama huo ubora si wako. Watu wanaiba au kufanyiwa mitihani, waalimu wanapasisha wanafunzi kwa rushwa, watu wanapeana nafasi za uongozi kwa kupendeleana bila kujali uwezo nk. Hayo ndo matokeo yake. Mpaka tukuone cha moto ndo tutaamka toka usingizini.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 30,761
  Likes Received: 4,131
  Trophy Points: 280
  sasa mimi ningeminterview kwanini; I was not looking to hire anybody au kufanya scouting kwa watu wengine!
   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,681
  Likes Received: 950
  Trophy Points: 280
  Sasa mbnona tunasengenyana humu!
   
 16. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #16
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,564
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hujajua vilaza wengi nguvu zao ziko kwenye CV??? Wao huwa wanamgojwa kubebwa tu
   
 17. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 8,714
  Likes Received: 1,632
  Trophy Points: 280
  sizani kama kingeleza ni kipimo cha kumuita yupoyupo,labda kama mlitafuta mtangazaji..wanasayansi kibao hawajui hiyo lugha,yaani watanzania wakishajua kingeleza tabu tupu kwa wenzao.
   
 18. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,513
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mzee hapo mzigo nakubebesha ww...
  hata hizo dk chache ulizopata kuwa nae hukuweza kuusoma uelewa wake???
  afu ndo ufananishe na hiyo cv??
  lazima ungekua na walakini...
  labda km hamkuongea kabisa...
  af ni wakike au wakiume.?
  ili tusihangaike sana.
   
 19. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #19
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 9,113
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  MM, Acha utani bana!
  Ina maana hujawahi kupigiwa simu na mwajiri fulani kwamba wewe ni refarii wa mtu ilhali mtu humfahamu na wala hajakupa taarifa kwamba kakuweka ni mmoja wa wadhamini wake katika wasifu wake (CV)?
  Same case scenario!
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 30,761
  Likes Received: 4,131
  Trophy Points: 280
  Nafasi ambayo alikuwa anaangaliwa kwayo ilihusiana sana na yeye kuzungumza Kiingereza na kwa jinsi alivyoandika ndivyo vilivyonivutia mimi.. Wakati mwingine wanaposema "the candidate should be proficient in spoken and written English" huwa ni kweli si utani..
   
Loading...