Kweli hii ruhusa ya mikutano itatekelezeka?

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,602
5,569
Najaribu kuwaza tu kama hakutakuwa na msigano baina ya ruhusa na matamko

===================================
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhan Kailima amesema Tume imetoa kibali cha mikutano ya hadhara ya kampeni ndani ya kata zitakazofanya uchaguzi mdogo wa madiwani na si nje ya kata hizo.

Kailima ametoa ufafanuzi huo leo Jumatano Oktoba 25,2017 alipozungumzia maandalizi ya uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 utakaofanyika Novemba 26,2017.

Akihojiwa katika kipindi cha East Africa Breakfast kinachotangazwa na Redio East Africa amesema, “Ni kweli mikutano ya hadhara imezuiwa na sipendi kuzungumzia sana huko, lakini Tume inatoa kibali cha mikutano ya kampeni ya hadhara kwenye kata husika na si nje ya hizo.”

Kuhusu watakaoruhusiwa kufanya kampeni amesema, “Watakaoruhusiwa kwa mujibu wa sheria ni mgombea mwenyewe, wanachama, chama chake au mtu yeyote ambaye mgombea ataridhia kumnadi.”

Mkurugenzi huyo amesema mazungumzo yatakayoruhusiwa ni kuwashawishi wananchi kumpiga kura. “Kwa mazungumzo mengine kuna hatua zitakazofuata ambazo Tume itashughulikia,” amesema.

Oktoba 4,2017 Tume ilitangaza uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.

Alisema ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo inaanza Oktoba 26 kwa kufanya uteuzi wa wagombea wa udiwani na kampeni zitaanza Oktoba 27 na kumalizika Novemba 25.

Soma: NEC yatangaza uchaguzi kata 43, zikiwemo za madiwani waliojiuzulu.


mwananchi
 
Back
Top Bottom