Kweli Hawa ni wanawake mfano wa kuigwa Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli Hawa ni wanawake mfano wa kuigwa Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Mar 8, 2011.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  WAKATI leo ni kilele cha siku ya wanawake duniani, baadhi ya wanawake wameonekana kuwa ni mfano wa kuigwa.

  Wanawake waliobainishwa kwa mfano ni pamoja Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti na Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia; Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Sophia Simba.

  Wengine ni pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani; Waiziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka; Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Samia Suluhu; Waziri Ofisi ya Rais Mazingira, Dk. Terezya Luvisa; Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya; Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto, Umy Mwalimu na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.

  Wanawake ambao ni anaharakati maarufu ni pamoja na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi Habari Wanawake (TAMWA), Ananilea Nkya na Mkurugenzi wa TGNP, Ussu Malya.

  Wanawake wengine ambao ni mfano wa kuigwa ni pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee; Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela; Injinia Stella Manyanya na wengine wengi walioonesha ujasiri wao.

  Gazeti la Dar leo.

  I dont know much about others, but those in bold, I doubt and I think they dont really deserve to be role models, especially S.S.
  Those in red, I salute them.
   
 2. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  First lady si mfano wa kuigwa?, mbona hayuko kwenye hiyo list.
   
 3. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mama Nkya mbona hujamsalute wakati she is an exemplary citizen, good leader and has had a significant impact on the health of the nation through her work in morogoro. Wewe umekosea kabisa, unaangalia kichama zaidi. Ukweli ni kwamba nchi zetu hizi nafasi ya mwanamke bado haijawa inavyotakiwa.
   
 4. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mi Tibaijuka, Mdee, Buyogela na Mch Assumpta tu....hao wengine hawana jipya!!!
   
 5. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  simuoni hapo Miss Judith, wamemsahau nini? na mimi ni mfano wa kuigwa ati, hahah

  Glory to God
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Huyu ni waziri wa nini au mbunge wa jimbo gani?
   
 7. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  headingi imeuliza hivi "Kweli Hawa ni wanawake mfano wa kuigwa Tanzania?" sasa kama ingetaka mawaziri na wabunge pekee ingeuliza "kweli hawa ni wabnge/mawaziri mfano wa kuigwa TZ?" hapo nisingetia neno, lakini kama ni wanawake, na mimi nimo na ni mfano wa kuigwa ati  Glory to God
   
 8. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mh haya, Nimekubali!
   
 9. c

  carefree JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Na mimi nimeweza kumudu majukumu yangu kazini nyumbani na ujasiriamali kinamna niko juuuuu
  na nategemea kupigiwa kura next election if god wish n i hope nitashinda
   
 10. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Tatizo mwandishi ameangalia cheo cha mtu, bila kuangalia kazi zao, ye kawaona mawaziri ndo wakuigwa wakati wengine wamefanya madudu mengi tu twawajua, na pia wapo wasio na umaarufu wamefanya mazuri makubwa katika nchi hii wameachwa. Anyway mi my mother ni mfano wa kuigwa...
   
 11. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Akiwa mfano wa kuigwa basi na mie ntampendekeza mama yangu awe nae mfano wa kuigwa!
   
 12. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Michelle, FL1, Lizzy na Regia Mtema ni mfano wa kuigwa humu jamvini.
   
 13. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hawa waigwe kwa kitu gani? ama kwa uanachama bora wa kwenye kundi la wezi wa mali za umma????
   
 14. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono mkuu...
   
 15. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfano wa kuigwa katika nini? Nini cha kuiga kutoka kwa Hawa Ghasia kama sio ghasia tupu, Sophia Simba mipasho na kunyima uroda wanaume wasio iunga mkono CCM, Kombani naye utata mtupu mara serikali haina budget ya katiba mpya, mara yalikuwa maoni binafsi! Labda ni mfano wa kuigwa kwa kupewa uwaziri kwa upendeleo bila kuangalia merits zao!!!!
   
 16. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  100% correct.

  Glory to God
   
 17. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  So do mamangu pia... Huwezi nieleza ati Sophia Simba na Ghasia ni wa kuigwa, kivipi? Post zenyewe wanazipewa kila msimu afu sioni kipy zaidi ya kutumia muda wao mwingi kulumbana na watu nje na ndani ya chama. Mfano wa kuigwa mama Mphamvu bwana!
   
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Sijui kama mwandishi yuko makini. Lakini kutokana na list hiyo nataka kujiuliza, ina maana wanawake wa mfano ni wale waliongia kwenye siasa na kwenye nyadhifa za uongozi tuu? bila hata kujali tabia na maadili yao? mlinda mafisadi naye ni mfano wa kuigwa?

  Are we serious kuwa mafuska, wazugaji, wababaishaji ndio wanawake wa mfano Tanzania? What kind of nation will that be?

  What about mwanamama wa kijijini anayetunza familia kwenye mazingira magumu na kuleta kwenye jamii mchapakazi mwenye afya? What about Mama ntilie anyeweza kuwasaidia manamba kupata chakula kizuri kiasi kwa bei nafuu?

  What about manesi, walimu wanaofanya kazi kwenye mazingira ya vumbi na machafu kwa mishahara midogo, what about those who work so hard to protect children? Are they not wanwake wa mfano.

  Kwa maoni yangu wanwake wa Tanzania wanastahili heshima zaidi kuliko matusi ya kwenye makala hiyo.
   
 19. P

  PakavuNateleza JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 957
  Likes Received: 513
  Trophy Points: 180
  Kuna Carina Wangwe kwenye mambo ya IT,Lady jay dee kwenye mziki,Mama Tibaijuka,prof amandina lihamba ete etc
   
 20. M

  Marytina JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  well said hasa hapo red.Jaman hivi JK ni kilaza kiasi cha kuwaweka Hawa (utumishi)? na Sofia uwaziri?
   
Loading...