Kweli hali ni mbaya kiasi hiki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli hali ni mbaya kiasi hiki?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 23, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Two Tanzanian stowaways to be deported

  January 22, 2008, 16:30

  Two young stowaways, who spent a harrowing eight days on a small ledge above a container ship's rudder from Kenya to Port Elizabeth, will be deported. The two youngsters, aged 18 and 16 years, are originally from Tanzania and said they fled poverty in their home country in search for greener pastures.

  Sadiki Ahmed and Saeed Abed left Tanzania for the port of Mombasa, Kenya, with the hope of boarding a ship to Europe.

  The Department of Home Affairs says it is busy with plans to deport them back to Tanzania, where they can apply for legal entry back into South Africa.

  My Take:

  Hivi kweli hali ni mbaya kiasi hiki maana wengine ndio tulikuwa tumeanza kufunga masanduku yetu ya mbao... kunarudika huko?
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hayakuanza leo hayo.... yapo miaka mingi sasa
   
 3. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2008
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tusiwe na kumbukmbu fupi. Tulishaambiwa humu JF, tena kwa ushawishi mkubwa sana kwamba mambo kama hayo yaliweza kutokea nyakati zile za hali numu ya maisha na kubanwa kwa watu wasisfiri kwa kunyimwa pasi.

  Waache hao ni mabaharia wa enzi mpya hizi. Wao hawatembei kwa miguu hadi Sudan; wanakodi meli nzima.
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hali inategemea una elimu na, kwa bahati mbaya, nasaba gani. Kuna watu wasio elimu wala nasaba, hata kipaji cha kubangaiza bongoflava nacho wanakosa.Wamezaliwa mjini na mambo ya kwenda shamba wanaona hawawezi, isitoshe wakiangalia watu wote wa shamba wanakuja kujazana mjini sasa wao wafanye nini? Ndiyo hivyo wengine wanaenda "Kiboko Msheli" wengine wanatafuta ndoto za Amba baharini na safari za kuzamia (so 80's!)

  Sasa mimi nafikiria mtu unazamia hujui hata unaishia wapi unaweza kutoka kurasini ukafunga safari mpaka Mogadishu halafu kuchukua meli itakayokurudisha kurasini baada ya dhahma kubwa, au kutupwa baharini na magiriki katili, au kuishia kwenye miamba iliyosahauliwa na mungu huko bahari ya pasifiki kama Tonga.

  Hali ni mbaya Mwanakijiji na ubaya ni kwamba wakati watu wanaagiza ma-Range Rover kwa ndege (ulimbwende gani huu!) wengine wanakosa kula milo miwili kwa siku, achilia mitatu.

  Kwa nini watoto wasitafute safari kwa nguvu.Hivi wale watoto wa Kitanzania waliokuja Marekani na Uskauti halafu wakaingia mitini hitch hiking the entire eastern seaboard waliishia wapi?
   
 5. M

  Mwendapole Old JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2008
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 249
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa hali hiyo, basi hawa ni wawakilishi wa kizazi cha wanaofanya hivyo kwa kukosa hela za kulipia pasi na usafiri halali, pamoja na kutokuwa na sababu halali za kuwapeleka wanakokwenda
  Walio na njaa hawajui bandari iko wapi; hata wale vijana wa ferry, wanaoishi kwa kuiba na kulala hapo ferry haijawahi kuwajia kufanya jambo hilo
  Wenye njaa wako vijijini, hata nauli ya kufika palipo bandari hawana
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2008
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Hivi karibuni nilisikia kunawengine walidakwa kule Walvis bay, Namibia na wakawa deported. Nitaitafuta story niiweke hapa. Nafikiri ilikuwa kwenye daily News au The Guardian. One of those TZ english papers!!!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jan 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  sasa pesa zote zilizopo Tanzania kweli bado kuna ulazima wa watu kuzamia au kudandia meli? Miaka ya themanini nilikuwa kwenye mpango huo, tukapata ratiba ya meli fulani ya Kigiriki ilikuwa kwenye gati la Raskazoni, tukailia mahesabu, tukatafuta yale mabiskuti magumu ya jeshi, na kujaribu kuzamia kutoka eneo la Raskazoni kule Tanga.

  Mimi na jamaa wengine watatu tukaweza kuingia kwenye ile meli na kujibanza kule injini room (kuna jamaa alituunganisha). Mara tukasikia meli inapiga honi zake tukajua tumedandia meli. Kwa siku saba tukawa ndani ya meli ikisafiri.

  Mara tukasikia meli imetia nanga na sisi tukaamua kuchomoka tukitarajia tutakuwa mitaa fulani fulani hivi ya mbali. Tuliibuka mapema alfajiri na tulikuwa tunafurahi kuwa "na sisi tumezamia".

  Kulipopambuza tulipoibuka na kutokea kwenye moja ya majengo pale Bandarini tukakuta ni Jengo la Nasaco! Kumbe meli ilitoka gatini tu na kuja bandarini! Ndipo nikajua mimi si mzamiaji..

  Lakini wakati huo ilikuwa ni wakati wa njaa ya 80s, mambo yote Duka la Kaya, RTC, vibali jumapili, n.k!

  Sasa kweli hali bado iko hivyo au kama walivyosema wengine hawa watoto ni kutotaka kujishughuulisha tu..?
   
 8. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2008
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na tena 'Biskuti' hizo ngumu zilipatikana kwa kuweka foleni kwenye duka la RCT, ya siku nzima pale Mkwakwani, kwenye barabara ya njia nne.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jan 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  kabisa.. si pale pana ule "mwenge wa Amani" sijui kama upo, karibu na Majestic Cinema...
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mimi nakumbuka wakati wa nyerere watu kama hawa (wazamiaji), walitoswa na kapteni wa kigiriki huko somalia (hafun) na hapo nasikia kuna papa ajabu, kuna waliopoteza maisha katika hao na kuna waliobahatika kusalimika na janga hilo. Mmmoja kati yao nadhani alikuwa mcheza mpira maarufu wa enzi hizo kutokea kule Tanga, jina sikumbuki (sijui ni Abdallah Luo) kama si huyo mtanisamehe ndio maana nimeweka kwenye mabano.

  Sasa sijui na hilo tuli-connect na hali ngumu ya wakati ule? duuh, uki-compare sasa na wakati wa foleni za vibiriti na unga wa njano sijui kama kuna hali ngumu sasa hivi.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jan 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  mbona hata baada ya Nyerere kuondoka na kufa watu bado walikuwa wanatoswa? sidhani kama kutoswa watu baharini kulikuwa kunahusiana na Nyerere.. but Nyerere anahusishwa na ufisadi mwingi na udikteta mwingi kwa hiyo I'll take your word for it.
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  si ndio maana yake, kama kuzamia wakati wa hali ngumu, wakati wa nyerere, hakuhusiani na hali ngumu, basi na hili la vijana hawa usihusishe na hali ngumu, Jee hali ngumu ya sasa na ile ya wakati wa nyerere, ipi zaidi?. The point siyo kutoswa the point ni kuhusisha kwako wazamiaji na hali ngumu.
   
 13. T

  TAIKUBWA Senior Member

  #13
  Jan 23, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huku Si Utani Hali Ni Ngumu Kabisaaa Kabisaaaa Mekuuuuuu Kama Umefunga Hilo Sanduku Meku Lifunguee Kabisaaaa Ama Ukubali Ubalali Utaishi Maisha Mazuri Tu Hali Ukija Na Cheti Chako Wakuu,,,,,
   
 14. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hii ndiyo dhana halisi ya "Maisha Bora kwa kila Mtanzania" Vijana wamesubiri kuona ndoto za maisha bora wakaona hawaoni kitu kikiendelea wakaamua kutimkia huko.
   
Loading...