kweli elimu ya juu yafanywa ngumu!!!

Mushobozi

JF-Expert Member
Aug 20, 2007
543
225
hapa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam jana ya tarehe 16, vijana kadhaa kama 50 walipita maeneo ya Nkurumah na maktaba wakiimba Tunataka Boom. wakati huo tulikuwa ndani ya maktaba, na hivu kuanza kuogoka kama tutapona maana move hizi zikishaanza hata kama wewe sio mmoja wao unalazimika kuwa nao; ama kwa viboko au kufungiwa mpaka jioni pale unapokuwa.

mida ilikuwa saa nne. baada ya kuzunguka kama mara tatu, sikuelewa walipoishia, ila ilibidi nifuatilie ili kujua kulikoni. haya ndio majibu niliyopewa kutoka kwa wanafunzi;

st year students, wanalipiwa kwa grades, kuna wanaopata A, B, C na D

wanaopata A=100%, B=80%, C=60% na D=40% ya karo yote

ili upate hiyo meals lazima ujisajiri; na kujisajiri, lazima ulipie ile asilimia ambayo bodi haitakulipia kwenye account ya chuo. hivyo vijana wengi wameshindwa kujisajiri kwa hawamu. this is terrible, maana kuna watu hawajajisajiri na bado wansubiria huruma ya chuo iwasajiri ili watakapopata hiyo asilimia basi waweze kulipia.

baada ya chuo kuona hivyo tangazo la VC lililobandikwa kwenye otice Board limeextend muda wa kujisajiri hadi tarehe 30 October kama deadline, na shule imeanza tarehe 21 September, sasa mtu aliyefachelewa siku 39 ataweza kucoup kweli?

Pia kuna wale wanaoendelea, ambao hawajapata ela yao toka board. nao wako hapo.

nililazimika kwenda loan board TRDO leo asubuhi kujua kulikoni, nikaambiwa eti Chuo ndio kilaumiwe kwa kutopeleka taarifa za vijana wanaoendelea, na kutokubali kusajiri vijana wanaoanza ili wapewe ela zao za accommodations na meal

nilipoenda kwa Bursar kujua kulikoni, nimeanbiwa yeye sio msemaji ila ni mtekerezaji.

vijana eti wanaona tarehe 27 October ni mbali, siku ya mgomo usiokuwa na mwisho. jamani hali hii itakuwaje kama kila mtu anafanya kazi bila kujari Kanini za ubinadamu?

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,953
2,000
Duh yale yale ya UDOM.
Unajua ukisha weka viongozi wa kukalili na imla maofisini basi madhara yake ndo haya.
Kwa nini watoe grade ktk mikopo?Utakuta hiyo A wanapata watoto wa wenye nazo.
Mungu tusaidie.
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
46,493
2,000
bila mgomo chuo hakiendi jamani
!!!!!!!!!!!!!tusiogpoe kugoma nakaumbuka tumegoma sana na wakina zitto
mpaka leo hii wanalipwa hela ya afadhali perday!!
 

Tonga

Senior Member
Jul 8, 2008
175
0
Mbona vyuo vikuu Tanzania vinaendeshwa kienyeji namna hii? hii sasa inazidi halafu tunashangaa mbona tuna wasomi wasiwasi! kama wanatumia muda mrefu kufikiria jinsi ya kujikimu tunategemea matokeo yao yawe mazuri kweli? kweli inatia hasira kila ninaposoma mambo ya vyuo vya nyumbani; its unbearable can we change and work as Professionals? watu wana majina makubwa ila utendaji wao zero...
 
Last edited:

F2S

JF-Expert Member
Feb 16, 2008
216
225
Naguswa kuandika kuwa heri wakati mikopo ikiwa chini ya wizara kwani hii loan board ni kitengo ambacho kinaprove failure kila kukicha. Nimegraduate pale UDSM wakati mikopo ikiwa chini ya wizara mambo yalikuwa safi kweli pesa wanafunzi wote wanaingiziwa siku kadhaa kabla ya kuanza masomo bila kelele na mwaka wa kwanza wanaletewa chuoni kwani wanakuwa hawana account. Sasa baada ya hii body francly speaking nilikuwa napata pesa baada ya miezi miwili napo baada ya kuacha masomo na kufatilia kwa udi na uvumba tukiwa na wanafunzi wengine na uongozi wa daruso. Bahati mbaya hata viongozi wa daruso inabidi wasaidie kufatilia hiyo mikopo na kuacha masomo hivyo wengine kufeli baadhi ya masomo.

Baya zaidi ukienda bodi ya mikopo TIRDO unakuta watu kutoka maofisini ndio wanaingia na kuapply na kupewa mikopo hiyo. Mwana JF mwenye uwezo wa kupenya hapo bodi ajaribufatilia list ya waliopewa mikopo mbali na wale fresh from school amwage tuone namna mambo yalivyo hapo.

This is worse nafikiri tunakoenda hao wanafunzi wataitisha mgomo wa nchi nzima na kusababisha nguvu za dola kuingilia kati kitu ambacho singependa kitokee kabisa last time jamaa walitupiga mabomu na virungu sio mchezo.

Moreover uongozi wa chuo ndio wala haujihusishi wanadai wao sio kazi yao kama kwenda bodi ni kazi ya mwanafunzi muhusika na bodi yake ya mkopo. Mwisho wa siku wanakudisco si utafeli usiombe kusoma bila boom. Hawa jamaa ni wajanja wamejitoa ktk vimeo vyote ikiwepo accomodation na hii mikopo kwani last time wao ndio walikuwa wanafatilia pesa wizara na ilikuwa very efficient kama hujapata unatoa taarifa kwa uongzi wa chuo nao wanadeal na wizara kijana unakama boom.

Hekima itumike bodi na chuo wawe wanadili na mikopo kwa kushirikiana sio kulaumiana kusiko na msingi wakati mtoto wa mkulima anaumia.

Na hili swala la % ya mkopo ndio utata sijui ni kigezo gani utatumia kujua nani ana uwezo na nani hana kwani lasilimali tanzania haiwi registered tutawapa 100% wanaojiweza kwa kuwa watatoa rushwa na kuwanyima wasiojiweza kwa sababu hawana uwezo wa kutoa rushwa. Utendaji wa bodi upitiwe upya hawa ndio wanasababisha JK aahirishe hata kuwaona na kuongea na wananchi( mambo ya MB)
 

Calnde

JF-Expert Member
Oct 7, 2008
1,373
0
Hapa ndipo changamoto inapokuja.Viongozi wetu kila siku wanalia hatuna wataalamu halafu hawataki kuwaandaa.huu ni ujinga uliokithiri ambao haupaswi kuendekezwa.Fikiri kama waliweza kiilipa kampuni ya kifisadi sh 152m kwa siku wanashindwa nini kuwasomesha vijana wetu ambao ndio msingi wa Taifa.Fikiri kijana amesoma kwa taabu miaka minne,anapata dili la kwenda nje unamwambia abaki hapa kwa sababu ya uzalendo!Serikali lazima ifanye reform katika mfumo wa Elimu la sivyo tutapotea katiak ramani ya nchi zinazotoa angalau elimu ya msingi duniani.Maizingira ya kusomea hasa pale UD ni very discouraging.Wanaomba bil 100 wanapewa bil 2 na Serikali.SERIKALI IACHE HUU UJINGA
 

Tonga

Senior Member
Jul 8, 2008
175
0
Ubaya serikali ya Tanzania haipi elimu kipaumbele ndio maana tuko hapa tulipo. Kama serikali ingejua umuhimu wa elimu na kuacha ubabaishaji hata kwenye maamuzi muhimu yanayoathiri utendaji wa kazi na kuliingizia Taifa hasara kila wakati, tungekuwa mbali kidogo. Sijui ni lini tutaamka katika huu usingizi wa pono manake sioni dalili kwa uongozi wa kishkaji tulionao sasa, i hope hii hasara tuliojipa kwa 'uvivu wa kuchagua' haitadumu kwa miaka 10, sipati picha Tz itakuwaje 8 -10 yrs to come!
Poleni wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania, natamani ningeweza kuwasaidia.
 

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,501
2,000
Kunji liliishia wapi? Enzi zetu kunji then mzee. Sasa yote hayo hakuna!!! Ndiyo maana wanafunzi wananyanyaswa bila mpangilio. Revist the real power of kunji na mzee alivyokuwa anawaanika. Naona hadhi ya chuo inaelekea kuwa kama ka college fulani tu!!! Ni aibu sana kwa taifa.
 

Balingilaki

Member
Aug 2, 2008
77
0
Kunji liliishia wapi? Enzi zetu kunji then mzee. Sasa yote hayo hakuna!!! Ndiyo maana wanafunzi wananyanyaswa bila mpangilio. Revist the real power of kunji na mzee alivyokuwa anawaanika. Naona hadhi ya chuo inaelekea kuwa kama ka college fulani tu!!! Ni aibu sana kwa taifa.

sijui ukiongelea chuo alafu college una maanisha academic performance au achievement,tena ni mara mia tungekuwa na college kuliko kuwa na vile unavyoviita vyuo ili hali mambo hayaendi katika nchi 'tumekuwa na vyuo vya kufundisha kukwapua' na si kusaidia wananchi wanaohitaji msaada wa wasomi.
 

Balingilaki

Member
Aug 2, 2008
77
0
kweli swala la mikopo ya wanafunzi ni swala zito: mi nahisi hii ya mikopo na sera zinazoambatana nalo ni mbinu ya 'watu weupe ambao kikwete anawkumbatia kutualibia mfumo mzima wa elimu ili tuzidi kuwatengenezea ajira'
maana hawa viongozi wetu wanaotudanganya eti wanampango kabambe wa kuboresha elimu /watoto wao wanasoma ngambo'
mbona waziri uingerezaamejiuzulu kwa kudai elimu imepanda uku yeye asomeshi kwny za 'kata' za uko je maghembe anasubiri nini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom