Kweli dunia tunapita. Huwezi amini enzi za Polepole, Makonda na Bashiru zimepita kama umande

Cha kujifunza ni kwamba ukitaka kutamba, kuwa kama Mo au Bakhresa; usitambie vyeo vya kupewa
 
Yaaah binadamu TUNAPITA...
Yaah vyeo VINAPITA....

ILA......

Nchi HAIPITI....
Taifa HALIPITI...

"Punda" AFE ,nchi ibaki SALAMA....

#SiempreTanzania
#VivaTanzania
Leo umekula biriani unatema madini
 
Mleta uzi idea anayoijadili ni kua humble duniani tunapita na cheo ni dhamana. Ili kuthibitisha idea yake ametumia mifano ya hao watu
Hata yeye atapita tu kama haamini aangalie kitambi chake kama kilikuwepo miaka 10 iliyopita.
 
Hakika dunia tunapita
Nikimkumbuka Polepole anayepigia Wakuu Wa Wilaya, Mikoa mpaka IGP simu usiku Leo hii ni bureee kabisa Hana lolote .

Polepole aliwahi kutamba kwamba ana koneksheni kubwa dah maisha haya.

Makonda akiwa kileleni baba Keagan aliwahi kusema yeye ndio mtu anayepata raha kuliko watu wote duniani astaghafilulaaah.

Bashiru kwa majigambo anampigia simu waziri Fulani anamwambia ilifanya hivi na vile kazi huuuna khaaa.

Kuna la kujifunza.

Maisha haya tunapita tu jameni.
Magufuli leo kalala peke yake ule msururu wa makomando umemuacha daaah.
Dah!...hivi Polepole akiamua kuendeleza kile kipindi, je hao mawaziri watagoma kupokea simu?
 
Mtoa mada ajue kuwa cheo na utu havikai chungu kimoja. Cheo kinadeal na taratibu na kanuni za kazi, lakini utu unadeal na taratibu na kanuni za tamaduni na dini husika. Kuwajibika na kuwajibisha watu kadri cheo kinavyotaka huo ni uwajibikaji katika cheo! Na ikumbukwe kila mwenye cheo anajua hatodumu na cheo milele. Otherwise unalenga kuleta fikra potofu kuwa utendaji wa majukumu ya serikali ni ya maridhiano na hayapaswi kuchukuliana hatua, Jambo ambalo linaturudisha enzi za uzembe ktk ofisi za umma!! Siku zote watu waliokosa nafsi za utii kwa mamlaka za kidunia huishia kulalamika watendaji wanapotimiza majukumu yao!
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom