Kweli Chadema wameamua... Mikutano minne kwa siku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli Chadema wameamua... Mikutano minne kwa siku

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Feb 26, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  VIONGOZI wa juu na wabunge wa Chadema jana walitawanyika katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza na kufanya mikutano ya hadhara kuendelea kupinga kupanda kwa gharama za maisha, malipo kwa Kampuni ya Dowans na kupanda kwa gharama za umeme.

  Viongozi na wabunge hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na Katibu wake mkuu Dk Willbrod Slaa aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita Oktoba 31 mwaka 2010 walichagiza katika mikutano hiyo ya mtawanyiko.

  Mikutano hiyo ya hadhara ilikusanya maelfu ya wakazi wa mkoa wa Mwanza, huku mwenyekiti Mbowe akifanya mkutano wa hadhara wilayani Geita akiwa ameongozana na wabunge wanne wa chama hicho na Katibu wake Dk Slaa akiwa Kisiwani Ukerewe ambako naye aliambatana na mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli na wabunge wa viti maalum, Rebecca Mngodo na Grace Kiwelu.

  Freeman Mbowe
  Mbowe alifuatana na Joseph Mbilinyi ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini, Halima Mdee (Kawe), Paulina Gekul na Anna Mallaki (viti maalum) pamoja na Profesa Kulikoyela Kahigi wa Bukombe.

  Akihutubia katika mkutano huo Mbowe alisema wilaya ya Geita, ni masikini kupindukia kutokana na wananchi wake kuhujumiwa na viongozi wachache walioko serikali licha ya kuwa na mgodi mkubwa wa dhahabu.

  Mbowe aliyasema hayo katika uwanja wa magereza nje kidogo na mji wa Geita, katika mkutano ambao ulitanguliwa na maandamano yaliyoaongozwa naye, huku wafuasi wa chama hicho wakibeba mabango mbalimbali, moja likilosomeka,’’Dowans ikilipwa, mimi nitajiua. Mtanzania halali’.’

  Huku akikatishwa na kelele za wananchi Mbowe alisema kuwa mgodi huo ilikuwa umejitolea kutoa umeme katika mji wa Geita kwa kuunganisha kwenye gridi ya taifa, lakini viongozi wa CCM waligoma kwa vile wao hawana uchungu na mgao wa umeme na kwa vile wana majenereta nyumbani kwao.

  Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alirejea kauli yake kuwa kamwe Chadema hakitakubali ushirika na vyama vingine bungeni akidai kuwa vyama hivyo ni mawakala wa CCM, lakini akasema chama chake hakina ugomvi na wananchama wa vyama hivyo na kuwaomba radhi kuwa ugomvi uliopo ni kati ya chama hicho na viongozi wa vyama vingine vya upinzani hasa kile cha CUF.

  Dk Wilbroad Slaa
  Dk Slaa alifanya mkutano wake wilayani Ukerewe ambapo amemtaka Rais Jakaya Kikwete ajiuzulu kwa kile alichokiita uzembe wa serikali yake, kuendelea kusababisha maafa kwa wananchi pamoja na kauli yake ya kutowafaamu wamiliki wa kampuni ya kufua umeme ya Dowans.

  Alisema haiingi akilini kuwa Rais Kikwete ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri lililoidhinisha mkataba wa kampuni tata ya Richmond ambao umerisishwa kwa Dowans kudai kuwa hafahamu wamiliki wake ambapo aliongeza kuwa ikiwa ni kweli Kikwete hawafahamu wamiliki wa kampuni hiyo, basi huo ni uzembe na anatakiwa kujiuzulu pamoja na serikali yake.

  Dk Slaa alisema pia kwamba Chadema haitakubali Tanesco kuingia mkataba na Dowans kama Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba anavyoshauri, vinginevyo watatumia nguvu ya umma kupinga hilo .

  Akifafanua alisema kimsingi mitambo hiyo inastahili kutaifishwa na kuonya kuwa kitendo cha kutaka kuingia mkataba na kampuni ya kifisadi ni ya kushangaza, kwani Serikali ilitambua tatizo la umeme wa kutegemea mabwawa ya maji tangu mwaka 2001 na baadaye tatizo hilo likajitokeza mwaka 2003.

  "Serikali makini, ingenunua mitambo yake yenye uwezo wa kuzalisha nishati hiyo na siyo kuingia mikataba ya kifisadi kama ya Richmond na baadaye Dowans," alisema Dk Slaa.

  Katibu Mkuu huyo wa Chadema alisema kwamba ameshangazwa na mtu aliyejitokeza kuwa ndiye mmiliki wa Dowans (Suleiman Al- Adawi) kujitokeza sasa akitoa madai tofauti ikiwemo na kutaka kusamehe deni hilo, baada ya kubaini mpango wa Chadema wa kutaka kutumia umma kupinga utapeli huo.

  Mkutano wa Misungwi
  Katika Wilaya ya Misungwi mkoani humo mkutano wa hadhara wa Chadema uliongozwa na mbunge wake wa Ilemela, Highness Kiwia huku ikielezwa kuwa mkutano huo ulisababisha kuvunjika kwa mkutano wa hadhara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, George Mkuchika uliokuwa ufanyike wilayani humo.

  Katika mkutano huo Kiwia alifuatana na wabunge wa viti maalum wa Chadema Raya Ibrahim (Pemba) na Chiku Abwao (Iringa) ambapo alisema aliyekuwa mpinzani wake katika kuwania kiti cha ubunge Anthon Diallo amemfungulia kesi mahakamani akimtuhumu kwa kuiba kura katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2010.

  Kiwia alisema pamoja na kumshitaki akidai aliiba kura kura zilizompa ushindi ametuhumiwa pia kufanya kampeni za vitisho na kusababisha wananchi kuogopa kujitokeza kwenda kupiga kura, lakini akasema ana uhakika kuwa waliomuweka madarakani ni wananchi kwa ridhaa yao na kudai kuwa atawapigania katika kuleta maendeleo.

  Kuhusu Katiba Kiwia alisema Chadema haitapumzika hadi Serikali ifanye mabadiliko ya katiba ambayo itamuwezesha mtanzania kufanya uchaguzi wa haki na kweli bila ya kupigwa mabomu.
  Katika mkutano huo wananchi waliohudhuria walipaza sauti wakisema kuwa Rais Kikwete hana budi kujiuzulu wakidai ameshindwa kuindesha nchi hii.

  Mkutano wa Kwimba
  Ezekia Wenje alifanya mkutano wake wa hadhara katika wilaya ya Kwimba huku akitoboa siri ya yaliyomsibu wakati wa kampeni za kuwania ubunge wa jimbo hilo.

  Katika mkutano wake Wenje alifuatana na wabunge wenzake wa chama hicho ambao ni Rachel Mashishanga, Philip Maturano, Joyce Mukya pamoja na mkurugenzi wa fedha wa chama hicho Antony Komu.

  Wenje alidai kuwa katika uchaguzi uliopita alihongwa Sh300 milioni ili ampishe aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na mgombea ubunge wa CCM katika jimbo hilo Lawrence Masha ambapo pia alidai moja ya chama siyo Chadema kilitenga Sh2.5 bilioni kwa ajili ya kuwagawia wapiga kura ili wachague chama hicho, lakini wananchi wa jimbo hilo waligoma na kulinda kura zao.

  Viongozi hao wa Chadema na wabunge wao watafanya maandamo ya amani na baadaye mkutano wa hadhara leo katika mkoa wa Mara.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo maandamano hayo yataanza saa 5 asubuhi yakianzia eneo la Makutano na kuelekea katikati ya mji wa Musoma kwenye uwanja wa michezo wa Mkindo.

  Habari zinaeleza kuwa ujumbe wa maandamano na mkutano wao wa hadhara ni sawa na ule walioutoa mkoani Mwanza, kupinga kupanda kwa gharama za maisha, malipo kwa Kampuni ya Dowans na kupanda kwa gharama za umeme.

  Habari hii imeandaliwa na Sheila Sezzy, Misungwi, Frederick Katulanda, Kwimba na Jovita Kaijage, Ukerewe.
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kaaaazi kweli kweli
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kaka tunashukuru kwa mchanganuo mzuri wenye umakin wa hali ya juu, binafsi nafurahishwa na mwenendo wa CDM, nafurahishwa zaid kwa ubunifu wao ktk harakati zakufikisha ujumbe kwa wananchi, realy wanaitaji support ya wananchi, tz yapaswa kujua yanayojili ktk serikali ya sasa. NGUVU YA UMMA ITASHINDA!
   
 4. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tanga hawaji?
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Watazunguka nchi nzima...
   
 6. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kazi nzuri sana!Naamini wamejipanga vizuri na watafika kila kona ya taifa hili.Ninachowaomba wasisahau maeneo ya kusini(mtwara,lindi),na kule kwa wenzetu zanzibar.
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Hivi CUF hawajatangaza kuja huko au ruti yao waliyopangiwa ni BUGURUNI - KIDONGOCHEKUNDU maana sijawahi sikia wakiandamana nje ya hapo.
   
 8. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hii ni ziara ya nchi zima, japo tanga mnatuangusha naimani watafika pia japo nanyi mpate upako!
   
 9. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Asanteeeeee!!!!!!!1
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  ninyi wagosi mshafungwa makamba toka january na mzee aliyejivutia maji kivyake
   
 11. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Well done chama langu.
   
 12. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kiasi gani kinachotumika kwa kila mkutano ? yaani posho? malazi? vyakula? gharama za mikutano zingine ?
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Wewe zinakuwasha wapi.
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ungejua gharama zake ungelia machozi , CDM sio mkombozi wa mtanzania, ni mnyonyaji na mdumazaji wa mtanzania. Wajinga wali wao kweli
   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo mkombozi wa mtanzania ni nani.
   
 16. b

  bulunga JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  inaitwa MANDE
   
 17. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  GeniusBrain bwana! kwa hiyo wewe ulipenda tuwe na chama kimoja tu!!!!!!!, vingine; vinawaduwaza Watanzania ha ha ha hi hih hi hi aluuuuu!!!!!!!!:mullet::mullet::A S 13:
   
 18. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />

  Ngoja watumie ruzuku ya chama kuelimisha wananchi. CDM ktk hilo mi binafsi nawaunga mkono, nipo radhi kuchangia chochote, kodi yetu haitumiwi barabara na mambo si shwari kwa mwananchi wa kawaida. Songeni mbele
   
 19. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Umemgeuza binadamu kiwa chake wakiita makalio pua waiita goti lakini unaamini unaongea ukweli mtupu! mtu wa ajabu sana wewe!!
   
 20. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kusema kweli chadema wameshika penyewe. Kitaeleweka tu.
   
Loading...