Kweli CHADEMA Hawajui 'Global Economic Crisis' Ndo Imezifikia Nchi Zinazoendelea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli CHADEMA Hawajui 'Global Economic Crisis' Ndo Imezifikia Nchi Zinazoendelea?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LINCOLINMTZA, May 18, 2011.

 1. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ndugu Wanajamvi,
  Nilikuwa 'nachat' na mkenya mmoja akaniuliza "Hivi na nyie vitu vimepanda bei kama huku kwetu?". Nikamjibu "Ndiyo tena Chama Cha Upinzani, CHADEMA kinafanya maandamano nchi nzima ya kupinga hali hiyo". Jamaa mwingine wa Uganda akiniambia kuwa nao hali ni hivyo hivyo na kweli vyombo vya habari vinatujulisha.

  Bwana mmoja amenitonya kwamba taasisi nyingi zinazopata 'grants' hasa Vyuo Vikuu kule Ulaya na Marekani zimepunguza matumizi kwa kupunguza malipo na nafasi za tutorings kwa sababu 'grants' zimepunguza kwa idadi na kiasi.

  Nikafanya utafiti kidogo, nikaambiwa kwamba effects ya "Global Economic Crisis" ndo imeingia kwenye nchi na taasisi zote zilizokuwa zinapata 'grants' kutoka nchi zilizoendelea kwa sababu grants nyingi zimeisha muda wake na hizo nyingi hazikubali kutoa mikataba mipya na ile iliyoendelea, kiasi kimepunguza. Hii imepelekea hali mbaya sana kwa nchi na taasisi zilizokuwa tegemezi kwa kiasi kikubwa sana kwa misaada hiyo.

  Pamoja na matatizo yaliyopo serikalini, CHADEMA hawajawahi kuligusia hili katika mfumuko wa bei zaidi ya kuilaumu serikali iliyopo madarakani. Je, ndo kusema hawalijui hili?
   
 2. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nadhani umesahau walichokisema akina Mkulo na Professor Ndulu. Wote walisema kuwa mfumo wa uchumi kuanguka duniani hauwezi kutuathiri sisi watanzania kwani uchumi wetu utaendelea kuwa imara. Juzi juzi tu Gavana ndulu ametueleza pia kuwa Tanzania ndio yenye reserve kubwa ya foreign exchange kuliko nchi yoyote ya Afrika mashariki na kati....na uchumi unakua vizuri sana. Mkulo nae alikanusha kuwa serikali haijafirisika na inapakaa kubwa la fedha huku akitoa na takwimu .... Sasa unataka viongozi wa CHADEMA wayazungumze hayo uliyoyasikia kwa Waganda na Wakenya ili iweje na kwa ushahidi upi?

  Nafikiri mambo ya Waganda waachie wao na Wakenya waachie wao ila ya Watanzania yanatuhusu wote. By the way mimi naishi China na ninaona vitu vinavyopanda bei kila siku, Nilikuwa huko Marekani kama kwa miezi miwili hivi nimesikia story ni hizo hizo lakini nakuhakikishia kuwa bei za daladala hapa China hazijapanda, vyakula muhimu navyo havijapanda hata kidogo pamoja na mafuta kutoka Kuai 6 mpaka 8 kwa lita sasa hivi.

  Naomba uangalie vyema ulinganifu (comparison) wako. Kenya siyo Tanzania wala Uganda siyo China na Urusi siyo Marekani ila CDM wanachosema ni kuwa bei za bidhaa muhimu zinaweza kushushwa na kuwa nafuu mfano wa China.
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Rais ndio halijui hilo. maana aliwahi kuhojiwa kwa nini Tanzania ni maskini jibu lake akasema hata yeye hajui, kwahiyo nakushauri umweleze Rais Kikwete tatizo ni nini atakushukuru,
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  CCM haijui ufisadi ndio kansa inayoliangamiza taifa
   
 5. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Uliulizia rwanda,burundi,malawi na congo?
  Mwanauchumi wetu tuambie kwa nini bei ya petrol iliyopitia bandari ya Dar inauzwa bei nafuu kule kigali kuliko Dar?
   
 6. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Hiyo GCrisis imeanza tangu tupate uhuru au we mgeni hapa TZ?
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mfumko wa bei (inflation) ulianza tangu 2006 and since then umezidi kupanda. World financial crisis haikuwepo 2006. Pili uchumi wa Tanzania hauko so connnected na wa nchi za magharibi na hata wakati financial crisis inaanza Governor Ndullu na viongozi wengine walikiri hilo. Sana sana Tanzania walikuwa na hofu ya kushuka kwa Direct Foreign Investment (FDI). Sekta ya utalii nayo ilikuwa inategemewa kushughuka kiasi kwa sababu watalii wengi walishindwa kusafiri. Hata hivyo utalii sasa hivi ok.

  Labda niseme, wakati wa chaguzi zote mbili 2005 na 2010 tuliona matumizi makubwa sana , imports ilienda juu na kulikuwa na a lot of money in the circulation! kuna mtu aliongelea hili? pili, mabilioni ya JK kuna taasisi iliangalia hili (in relation of circulation). Nadhani uchumi wa Tanzania unaweza kutulia kama tutacha kuugemea zaidi kwenye 'green' policies.
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Yeah ndio Maana kodi ya Madini ni asilimia %3 ?

  Ndio Maana Mafisadi kila kona Serikalini ?

  Ndio Maana chama kimejaa Wafanya biashara walafi? wasiojali Nchi?

  Ndio Maana Rais anagawa Vyeo kutokana na Urafiki ili washibishe hayo Matumbo yasiyoshiba hata kama ni Makubwa?
   
 9. d

  dotto JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Global Crisis inatokana na mambo mengi. Kwa Tanzania JK alishasema hiyo haitatugusa kabisa katika siku za mwanzo. Na baadae kidogo tukaanza sikia mahoteli yanapunguza wafanyakazi wake sababu wageni wachache. TAtizo pia ni mafuta lakini tunahitaji pesa za kitanzania kiasi gani kwa pipa moja la mafuta kulingana na Exch.rate zetu za sasa hapa Tanzania. Kwani ni lazima Exch. RAte zifike huko. HAkuna Mwarobaini wa hilo. Mahela waliyokuwa wanamwaga wakati wa uchaguzi hawakuwa na ushauri toka kwa wana economics. Ni aibu kutawaliwa na mbayuwayuuuuu.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Serikali makini hata simu moja haiwezi kuacha bidhaa nyeti kama mkate , mafuta ya kupikia , nk kupanda bei then unasema ni dunia na mfumuko sijui wa ujinga gani . Kuna vitu kama beer bei ikipandahakuna kulalama waka kuandamana but not mahitaji muhimu ya maisha ya mtanzania no way .
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu unaposema Chadema hawajui una maana gani?...
  Hivi kweli wewe na usomi wako ama niseme kwa kuuliza kwako hiyo Global economic crisis ambayo ndio sababu ya mfumko wa bei za bidhaa unatokana na sababu kuwa hata Kenya na Uganda nao wanalia hivyo hivyo! hii imekuwa sababu ya kudai kwamba Chadema hawajui?

  Tuzungumze kisomi kwa sababu wewe ndiye unajua au sio?
  1. Ebu nambie kwa ufasaha zaidi hiyo mikopo unayozungumzia haitoki, kama tungepewa sisi ingeweza vipi kushusha bei ya bidhaa.. nambie mkopo unaopewa serikali kuendesha miradi ya maendeleo utaweza vipi kushusha bei ya sukari, mchele na mazao mengineyo.
  2. Nambie wewe kwa nini bei ya bidhaa zetu iwe sukari, mchele, saruji na mali nyinginezo ziwe bei ghali kuliko zile zinazoagizwa toka nje?.

  Nakumbuka serikali hii imekatiwa mikopo kwa sababu nje kabisa na hali ya kiuchumi duniani, kama sikosei tumeshindwa ku qualify kutokana na grand corruption ambapo fedha nyingi za mikopo zimetumika vibaya na tumeshindwa kuonyesha matunda ya fedha tulizokopeshwa kiasi kwamba imefikia serikali yetu kukopa fedha toka benki za ndani kuweza kuendesha.. Na kama serikali imefikia hatua hiyo ina maana fungu la fedha ambazo wangepewa wananchi ktk mzunguko wa kibiashara zimepungua au hazipo tena..

  Tatu, binafsi nashindwa kuelewa zaidi naposikia leo hii benki zinatoa mikopo kuliko wakati wowote ule kwa sababu wananchi wengi wamejiingiza ktk ujasiliamali bila kujali riba kubwa wanayotakiwa kulipa. Infact wananchi wengi wamepoteza nyumba na mashamba yao kwa mikopo hi ambayo waliwekeza ktk biashara za kuiga in imports kuliko ubunifu wa miradi ya ndani...

  Na hakika sababu hasa ya biashara nyingi za kuiga hasa ktk imports mali kutoka China na Dubai zimekwama kutokana na udogo wa middle class ambayo kila siku inazidi kupungua kutokana na kwamba tumejenga taifa la tabaka mbili - Matajiri na maskini. Hivyo Matajiri hawana sababu ya kununua mali feki toka China au Dubai na hata kama watazihitaji watakwenda wao wenyewe huku kundi la maskini wanashindwa hata kununua chakula..Mtajiri wananunua vyakula vyao supermarket Mlimani city na Shoprite na maduka ya kuagiza zaidi ya mali ya mkulima ambapo mfanyakaz mwenye mshahara mdogo pia hawezi kumudu bidhaa za ndani..

  Kwa Tanzania mkuu wangu hatuna sababu za kiuchumi ktk kufikia hali hii isipokuwa ni matumizi mabaya ya uwekezaji toka serikalini hadi wananchi kwa sababu kama mazao yetu yamekosa soko ulaya na yameshuka bei (hali halisi) iweje leo bei hizo zipande nyumbani?.. maanake nijuavyo mimi global crisis imesababisha malighafi zetu zishuke bei kutokana na hizo nchi za Ulaya kubana matumizi yao na moja ya vitu vilivyoathirika ni mazao yetu, hivyo kiuchumi malighafi yetu inapokosa soko na kushuka bei ndio inaathiri uchumi wetu kwa ujumla (exports) wakati huo huo mali tunazoagiza toka nje (imports in finished product) zimepanda bei..

  Sasa mkuu wangu ebu wewe nambie, sisi waafrika ni lini tutaelewa kwamba ktk makuzi ya maendeleo kuna hatua.. Hatuwezi kufikiria kuendelea ikiwa tutabakia ktk hatua ya uzalishaji malighafi wakati Ulaya na nchi zote zilizoendelea ndizo zenye viwanda aama wamepiga hatua nyingine baada ya viwanda..Wao wana kina sababu ya kuepeleka viwanda vyao China, India na Vietnam ambako hawapeleki malighafi..Na kibaya zaidi leo hii tuta deal na China na India kuwa wanunuzi wa malighafi zetu badala ya nchi za Ulaya na kibaya zaidi ni kwamba tunashindwa hata kushindana na nchi zinazoendelea...

  Toka tumepata Uhuru hakuna nchi ya kiafrika ambayo inajiandaa kiuchumi ipate kuendelea isipokuwa kwa kuomba Mungu wavumbue mafuta..Ni sawa na maskini kina sisi tunaoomba Mungu kila siku tushinde bahati nasibu (Lotto) hatuna tumaini jingine wakati wenzetu wameweza kupiga hatua toka umaskini hadi hapo walipo kwa ubunifu wa miradi ya maendeleo. Haikuwa bahati ya Mungu kujaliwa nahata kama sisi tutajaliwa bado hatukujiandaa kuendesha miradi hiyo. Tazama tuna dhahabu, gas na madini chungu nzima yote hii inaendeshwa na mashrika kutoka nje... Hatukujiandaa kabisa kuzalisha mali hizi ingawa tulijua utajiri huu miaka 50 iliyopita..
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkandara kijana mtupu ama anajifunza kuandika na kujenga hoja . Tuna ushahidi baada ya TZ kushindwa kuonyesha ilivyo tumia pesa ilizopewa na wahisani wakubwa kama Holland n Uswiss wamekataa kuwapa pesa kabisa kabisa na sasa Mkullo na CCM wanajiandaa kulitangazia Taifa kwamba misaada imekatwa kwa sababu ya uchumi umeyumba duniai lakini watu wale wale wanawapa Kenya , Uganda, Burundi na Rwanda pesa kwa nini iwe kwa Tanzania pekee ?
   
 13. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  ungekuwa na akili ungeuliza bei za bidhaa za tz na kenya miaka 2 iliypota halafu ulinganishe na bei za leo na mabadiliko ya kiasilimia, achana na uganda huyo ni mfu
   
 14. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kweli kichaa huwaona watu wengine wote ndo vichaa na mjinga hufikiria watu wote ni wajinga bila kujijua yeye ndo mjinga. Niulize kama unaswali lakini siyo kuhukumu uwezo wa akili yangu. Ulitaka niandike yote nilichat naye. Hii ni summary tu.
   
 15. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Hilo ndilo tatizo la watawala wetu - wana mawazo kama yako ya kutafuta visingizio.

  Kiongozi bora ni yule mwenye "VISION", anaweza kuona yaliyo mbele na KUCHUKUA HATUA kabla hayatokea. JK alinukuliwa akisema "Tunasubiri huo mtikisiko wa uchumi ukitufikia tuone tutafanyaje". Waziri wake wa fedha (kumbuka NSSF ilimshinda hadi akastaafishwa kwa manufaa ya umma!) nae alituambia kuwa hakuna madhara yatakayotufika. Ni kweli kuna matatizo ya uchumi duniani, swali la msingi: Serikali INAFANYA NINI kukabiliana na hali hiyo.

  Wewe na Chama Cha Magamba mnanikumbusha hadithi ya bwana mmoja aliedaiwa nguo ya sikukuu na mwanae. Mzee kujitetea akasema: Sina pesa mwanangu, sikukuu hii imekuja ghafla.
   
Loading...