Kweli CCM is in dis array, sijasikia Kinana wala Makamba akiongea lolote

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,171
Toka mwisho wa February mwaka huu 2921, Tanzania imepitia msukosuko liasi wa kisiasa na kiserikali kutokana na kutooneka, kufariki, na maziko ya Rais wa nchi Mh. John Pombe Magufuli.

Muda wote huu CCM imekuwa kama kungwi, akifanya kazi huku kajigubika kaniki.

Cha kushangaza zaidi ni makada wake maarufu kukaa kimya utafikiri hawapo kabisa.

Abdulrahman Kinana na mwenziweYussufu Makamba waliowahi kuwa Makatibu Wakuu wa CCM, wako kimya kabisa.

Aidha wazee hawa walikerwa na uendeshaji wa chama au lile sakata la kutaka kuwabambika kesi za kijinga ziliwakatisha tamaa na chama.

Mimi nawahimiza warudi kwenye mstari wa mbele chamani, Kikwete peke yake itamwia vigumu.

Popote mlipo wazee wetu.
 
Mliwadhalilisha wazee wa watu na wakawaachia lichama lenu; mtu anayeweza kuwashawishi kwa mfano kinana ni mzee mangulla peke yake! Mzee makamba ana hasira na umri nao umekwenda hawezi kukubali kurudi hata kwa kufungwa kamba!
 
Ni kweli walidhalilishwa lakini hilo lilifanywa na Mwendazake kwa kuwatumia kina Kilaba wa TCRA, ku tape sauti za viongozi(which is criminal).

Lakini sasa hivi chama kina wahitaji sana for continuity maana tunafahamu hata mzee Mangula alipata matatizo ya kulishwa nafikiri sumu lakini bado anatetea chama.
 
CCM ilishauwawa kama chama na mwendazake.
Waliingizwa wapiga porojo kama Polepole na waliokuwa wapinzani kama Bashiru aliyekuwa CUF.

CCM is no longer a political pointer.
 
CCM ilishauwawa kama chama na mwendazake.
Waliingizwa wapiga porojo kama Polepole na waliokuwa wapinzani kama Bashiru aliyekuwa CUF.

CCM is no longer a political pointer.
Kweli kabisa CCM sasa hivi is like a headless chicken.
Haina mwenyekiti wala katibu mkuu.
 
Back
Top Bottom