Kweli bwana Masako; tutoke kwenye mfumo dume na kwenda mfumo wa kutokuwa na dini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli bwana Masako; tutoke kwenye mfumo dume na kwenda mfumo wa kutokuwa na dini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngekewa, Apr 2, 2011.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nimeangalia kipindi cha Kipima joto cha ITV na mwisho wa kipindi hiki nilipata ujumbe uliokusudiwa na mtayarishaji Bwana Masako.
  Mada ya kipindi hicho ilikuwa mchakato wa sheria ya urithi. Walioshiriki wote walikuwa na mawazo mamoja ya kupinga sheria za mila na za dini.
  Kwa mawanzo yangu mambo mawili yalikuwa si sahihi.
  1.Mtayarishaji kutowa nafasi kwa watu wa aina moja tu ( kwani kwa bahati mbaya washiriki wanne wote walikuwa Wakristo) na kuacha kusikia maoni ya pande mbili (dini na mila) haikuwa sahihi. Tuna uzoefu wa kuona mila fulani kuwa potofu na kupigwa vita jee na dini nayo tusemeje?

  2. Watowa mada walikazania kifungu cha haki za binaadamu na kusahau kuwa katiba hiyohiyo ndiyo inayotambuwa uhuru wa kuabudu, sasa hawaoni haja ya vitu viwili hivi vikaenda sambamba kama vinavyokwenda sasa?
  Namjuvya Bwana Masako kuwa kulikuwa na mfumo dume na ukapigwa vita lakini kwa namna alivyochaguwa watu wa kutowa mada nahofu kuwa anapalillia kile Waslamu wanachosema Mfumo wa Kikiristo.
  Sipendi kumpaka mtu jambo ambalo pengine hakulikusudia lakini napenda kumtahadharisha tu kuwa mambo haya tunayoyaona madogo ndio msingi wa mmngonyoko wa umoja wa jamii.
   
 2. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hongera kwa kuisoma kwani naamini itamfikia mwenyewe! Pengine atajisahihisha siku nyengine!
   
 3. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Hata mi skuwa satisfied na wachangiaji jinsi walivyokuwa na upeo finyu wa dhana tofauti kuhusu mirathi, kiasi kwamba waliniboa! Kwani dhana ya urithi na ukristo ikoje?(sory cna mtizamo wa kidini)
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Mi sioni tofauti kati ya mila na dini kwani zote ni dini, naona wachangiaji wengi munaelekea kusema kuwa sheria zote niza kikristo- wenye muono huu nawapa pole: to me hakuna tofauti kati ya ukristo, uhindu, ubudha, usabato, ubaptist, uothodox, uislam na upagani: mfumo unaoweza kuwa sahihi ni ule usioegemea upande wowote yaani mfumo wa sheria za nchi na si makundi mengine.
   
 5. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwa nini vita na uhalifu
  vimezagaa kila mahali bila
  sababu za msingi ?
  BIBLIA INAJIBU HIVI:
  "Kisha aliwaambia, Taifa
  ...litaondoka kupigana na taifa,
  na
  ufalme kupigana na ufalme".
  Luka 21:10.
   
Loading...