Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,004
MPANGO APINGANA NA UGUMU WA MAISHA


Na JANETH MUSHI – ARUSHA


WAKATI idadi kubwa ya wananchi wakilalamikia ugumu wa maisha unaowakabili, Serikali imesema kwa kutumia vigezo vyote vya kitaifa na kimataifa, hali ya mwenendo wa uchumi nchini ni nzuri.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Arusha na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano wa 18 wa taasisi za fedha nchini.

Pamoja na hayo, Dk. Mpango alisema Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kimataifa.

“Tayari Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umasikini nchini (Repoa), imeshafanya utafiti wake na kuonyesha viashiria vinavyoonyesha mwenendo mzuri.

“Mbali na Repoa, zipo taasisi nyingine ambazo zinaendelea na uchambuzi wa mwenendo wa uchumi wa nchi.
“Nilishasema bungeni na narudia tena, kwamba kwa vigezo vyote vya kimataifa, tutaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwani hata Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), limetoka hapa nchini hata mwezi haujapita, nao wamechambua mwenendo wa uchumi wetu na kusema uchumi wa nchi yetu ni mzuri.

“Maneno yanayosemwa mitaani, kwamba hali ya uchumi ni mbaya na fedha zimepungua katika mzunguko yanaenezwa na wapiga dili.

“Katika hili, nawatoa hofu wananchi, kwamba hali ya uchumi iko imara na hayo maneno yanayosemwa si ya kweli bali tufanye kazi kwa bidii,” alisema Dk. Mpango.

Alisema pia kwamba deni la taifa na mauzo ya ndani na nje yanakwenda vizuri ingawa ukame unaonyemelea nchi, unaweza ukasababisha upungufu wa chakula katika baadhi ya mikoa.

Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, alizishauri benki na taasisi nyingine za fedha kuhakikisha zinawafikia Watanzania wengi kwa kuwashirikisha kutoa mchango wa kifedha.

CHANZO: Mtanzania
 
UKIMULIZA MPANGO SUKARI AU UNGA KG 1 NI SH NGAPI....SIJUI KAMA ANAJUA

OVA
 
Uchumi umekua....je hizo sh mil 50
kila kijiji ziko wapi? Dawa hospitali hakuna hela za kununulia ziko wapi wakati uchumi unakua, kulipa madai wa watumishi wa serikali, nyongeza za mishahara hakuna lakimi uchumi unakua!!
Ruzuku ya pembejeo inatolewa kwa asilimia 10% tu ya wakulima lakini uchumi unakua,.... I do not understand
 
Ndiyo wasomi watanzania hao, yeye kwa vile yupo vizuri mfukoni haoni wengine.
Yeye anavyofikiria ni sawa na apo Dar es salaam Tanzania watu wanavyokuwa na shida ya maji, umeme, mvua, na usafiri wanakuwa awakumbuki kama kuna watu wapo vijijini na izo taarifa kwao ni ndoto na awawezi kuzipata kwa iyo kilichopo apo ni kusubiria tuuu sindano na dawa ituingie vizuri
 
Tatizo la wasomi wetu wakiishi nje ya vyeo vya kisiasa maisha hayaendi vizuri wanabakiza kufundisha tu, wavivu wa kufanya tafiti na sio wabunifu wa kujiajiri,sasa huyu ukweli anaujua ila mukulu akikusikia tu unasema ukweli kwamba uchumi upo kwenye hali mbaya kesho yake anakutengua sasa wamebakiza unafiki uliokithiri ili kumfurahisha mkuu wa kaya.
 
Back
Top Bottom