Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 14,706
- 42,612
Hello !
Mwanzoni mwa mwezi May 2024 mke wangu aliniambia kuwa kadi za CCM zinefika, mjumbe kaandika jina lako hivyo twende ukachukue kadi yako.
Nilitafakari, inakuwaje mjumbe aandike jina langu kwenye orodha ya wanaohitaji kadi za CCM bila ridhaa yangu.
Kwakuwa nilikuwa free nikaona nisigombane na wife au mjumbe tukaambatana mpaka mahali zilipokuwa zikitolewa kadi za CCM.
Nilimkuta mwenyekiti wa serikali ya mtaa wetu nikamsalimia akafurahi. Akanisifia kwa hili na lile na kunitaka nijipange kugombea udiwani wa kata yetu , nikajua tu ni janja tu za kukaribia uchaguzi wa serikali za mtaa.
Zoezi la kugawa kadi llhuku likiendelea niliona vijana wenye nguvu wakiwa na bashasha kupokea kadi za CCM. Mimi Kadi yangu nilikuta iko tayari licha ya kutoa sababu zangu kuwa Mimi sipaswi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini wakanisihi tu nichukue kadi, kauli za hata IGP ana kadi ya CCM, CDF ana kadi ya CCM zilisikika. Nikachukua kupooza mvuke yakaisha. Aisee huu mtaa wetu sio wamama wala vijana. Kadi zilichukuliwa kwa kasi mno.
Nikamuuliza wife ambaye naye ni katibu msaidizi wa wamama wa CCM, je, hawa vijana, mabinti na wamama wengi kiasi hichi ni nini kimewasukuma kuchukua kadi za CCM?
Akasema si kila mwana CCM yuko CCM, watu wanafuata vipesa vya hapa na pale. Hata wife si mwana CCM halisi.
Vijana mavyuoni , sekondari na mtaani wanajiunga CCM.
Iwe kwa unafiki au kwa moyo hii hali inaogopesha.
CCM imeshindwa kutumia rasilimali zenye thamani ya ma quadrillions badala yake inabudi kodi haramu kila mwaka.
Badala yake inajisifu kukopa na kupokea misaada.