Kwaresma

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
740
Kuna mdau amenitumia hii nyepesinyepesi nikaona niibandike hapa.

Naye Lowassa akawaambia mawaziri wengine"

KESHENI mkiomba kwani hamjui siku wala saa atakayokuja Dr Mwakyembe.
Nami naenda mtaani kuwaandalia kijiwe ili nitakapokuwa nanyi muwepo.
Nanyi muonapo tume zaundwa basi mtambue muda wa mavuno ya MAFISADI umekaribia".
Kisha akakwea tena Ikulu kuomba Rais asimfilisi. Lakini RICHMOND akatokea na jeshi la Mwakyembe na kusema " Nitakayembusu huyo ndie....!".
Mara Chenge akatoa Upanga alani na kumkata mfuasi wa Mwakyembe(Anna Kilango) sikio.
Lowassa akamwambia Chenge "rudisha upanga wako alani, Kikombe nilichotupiwa na Kikwete Sina budi Kukinywa"

Moja kati wa mayahudi wale aitwaye Selelii hakuamini kama Lowasa Kajiuzuru, akatwaa mkuki akamchoma ubavuni na tazama...Ikatoka gas ya songosongo na nati ya mitambo ya umeme...
Siku ya tatu wakaenda pale ofisini kwake...
Lakini wakakuta wingu la Mvi limetanda na Suti ya mistarimistari pale kitini walipomweka..yule morani waliyemkuta getini akawaambia mnayemtafuta hayupo.....Ameshapaa kwenda Monduli na yupo kuume kwa Laiboni..Wakasema..."Hakika huyu alikuwa Fisadi.
 
du we mkali ndugu. Nimecheka hadi mbavu zinauma. Sikuwa kwenye good mood lakini after kicheko hiki niko fiti sasa mkuu.Thanks
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom