Kwanza mwanafunzi asichapwe, pili akipata mimba arudi shuleni, tatu kama ana utovu wa nidhamu pia arudi shuleni. Waoneeni huruma walimu

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
3,361
5,808
Nyie wanasiasa waoneeni huruma hao walimu mnao wakabidhi watoto wa aina hiyo.

Wazo la kwanza kuwawekea mfumo wao lilikuwa zuri sana lakini hili la kuwachanganya na wanafunzi wengine katika mfumo rasmi hapana.

Nitajieni ni nchi gani Ulaya na Amerika ambayo inatumia mfumo huu unao letwa Tanzania.

Nadhani sasa tume halalisha mapenzi shuleni nadhani sheria za shule zirekebishwe swala la mapenzi na mimba lisiwe kosa tena si kwa mabint si kwa vijana.
 
Nitajie nchi moja Ulaya au Marekani au Australia au Canada ambako mwanafunzi anachapwa, anapimwa mimba na akipata mimba anafukuzwa shule. Nitajie hata nusu nchi. Hata robo nchi.

Amandla....
 
Taifa Linaenda kuwa na Mmomonyoko Wa Maadili na KUBOMOKA Zaidi kipindi hiki kuliko Kipindi chochote huko nyuma.

Haya Mambo ya Watu Wa Magharibi sio Lazima tuyaige yote.

Tusipoangalia hata Mapenzi Ya Jinsia moja tutambiwa ni Haki za Binadamu hivyo hatuna budi....Eeeeh Mola Tusaidie.

Hapa naongea Kwa Uchungu Sana liwalo na liwe.
 
Hayo maadili yamakusaidia nini wewe kilaza fukara kwa miaka 60?
Taifa Linaenda kuwa na Mmomonyoko Wa Maadili na KUBOMOKA Zaidi kipindi hiki kuliko Kipindi chochote huko nyuma...!
Haya Mambo ya Watu Wa Magharibi sio Lazima tuyaige yote....! Tusipoangalia hata Mapenzi Ya Jinsia moja tutambiwa ni Haki za Binadamu hivyo hatuna budi....Eeeeh Mola Tusaidie.
Hapa naongea Kwa Uchungu Sana liwalo na liwe....!
 
Uoga wako tu. Wewe unadhani kumomonyoka maadili ni watu kujamiana tu? Iwe jamii tofauti au jamii moja. Hauoni dhulma, ubakaji wa watu wazima na watoto, uuaji wa vikongwe, uuaji wa albino, unyang'aji, uvunjaji wa nyumba ( grili zinathibitisha hiyo), ufisadi, ubamizaji wa kutisha wa wake zetu na watoto wetu, rushwa iliyokithiri.

Kutiwa ndani kwa kuonewa, kupigwa na kuwekwa ndani kwa sababu una jog asubuhi au umevaa fulana fulani, kufa kwa sababu huna hela ya kuhonga, kufa kwa sababu hamna dawa hospitali, kufa kwa sababu umeshindwa kufika hospitali, kufa kwa sababu hospitali haina vifaa, baada ya kufa maiti yako kuzuiwa kwa sababu huna pesa, watu kuvunjiwa vibiashara vyao bila compesation na kadhalika na kadhalika. Watu mnatembea na vibameidi na mabinti wa kazi wenye miaka 13 na mnajiona mashujaa!

Wewe unaona tatizo kubwa ni binti kuruhusiwa kuendelea na masomo baada ya kupata mimba kutokana na kubakwa! Au watu wazima wa jinsia moja kujamiana kwa hiari yao? Kitu ambacho kipo miaka yote, hata kabla hao mabeberu kuanza kututembelea. Mnafik mkubwa wewe.

Amandla....
 
Nuneni, kasirikeni, fokeni, lakini mtoto wa kike lazima apate elimu bila ya ubaguzi wowote ule🤗🤗🤗

89a_.jpg
 
Nadhani nidhamu kwa hapa Tanzania ina maana tofauti na ile iliyozoeleka. Unahisi tumewazidi nidhamu mataifa ya Ulaya?! Ufisadi, Rushwa, Wizi, Mauaji, Matusi, Ukosefu Wa Heshima nk.

Yote hayo yanafanywa na nani kama sio hao tuliowachapa mashuleni?! Viboko sio solution la kurekebisha nidhani wala maadili vinaleta usugu yu kwa muadhibiwa.
 
Nitajie nchi moja Ulaya au Marekani au Australia au Canada ambako mwanafunzi anachapwa, anapimwa mimba na akipata mimba anafukuzwa shule. Nitajie hata nusu nchi. Hata robo nchi.

Amandla....
Usipende kutajiwa ulie zoea school feeding.

kaangalie states za Marekani ngapi zinaruhusu fimbo.
 
akili yako mleta mada, ina uwanda mdogo sana wa kufikiri, unasubiri jambo lifanywe na mataifa ya magharibi ndio uone ni faafu kwetu? mwisho umetahadharisha juu ya ujio wa ushoga mbona mataifa ya magharibi wenyewe wamehalalisha na haujataka tuige mfano, badala yake unapinga hili la mimba kisa tu hawajahalalisha.

hapo jukumu litabaki kwa mzazi kumfunza mtoto wake kuwa na maadili. na ukizingatia kuwa vyote vinavyozuiliwa bado vinafanyika, ni vyema kupunguza uharibifu unaotokana na matokeo ya utendaji wa makatazo yote kwa kuanza na kuwajali mabinti wanaopata ujauzito shuleni.

mzazi.
 
Ni sawa tu, wacha warudi shule itasaidia wenzao kujifunza kutokana na makosa yao. Huwezi amini ni kazi ngumu kwa mtoto kukubali kurudia darasa kuliko kufukuzwa shule kabisa.

Ni swqla la kisaikolojia tu, watajilinda tofauti na zamani. Hawa ni watoto akili zao zipo tofauti sana. Akiwaza kurudia darasa ataona ni bonge la adhabu.

Tatizo umewqza kiutu uzima sana jaribu kuwaza kitoto utamuelewa mama, au jaribu kuuliza wanafunzi lipi bora kwao utabaki kushangaa mawazo yao
 
Kuchapa viboko sio njia sahihi ya kumjenga mtoto, mtoto ajengwi kwa adhabu hata kidogo.. Wale walio kulia kwenye misingi hiyo ndio hao mnawaona madarakani
 
Nyie wanasiasa waoneeni huruma hao walimu mnao wakabidhi watoto wa aina hiyo

Mama samia unanasa kwenye mitego inayo haribu taifa kimaadili na kwa vile umenasa kwenye hayo basi la ushoga lipo njiani

Wazo la kwanza kuwawekea mfumo wao lilikuwa zuri sana lakini hili la kuwachanganya na wanafunzi wengine katika mfumo rasmi hapana

Nitajieni ni nchi gani ulaya na Amerika ambayo inatumia mfumo huu unao letwa tanzania.

Nadhani sasa tume halalisha mapenzi shuleni nadhani sheria za shule zirekebishwe swala la mapenzi na mimba lisiwe kosa tena si kwa mabint si kwa vijana.
Sisi ni wa africa elimu kwetu nikitu kimekuja sasa tunapochukua elim yetu iwe kama ya ulaya na marekani walimu watashindwa na mwisho hili taifa litashuhudia mmomonjoko mkubwa wa maadili. God have a mercy on us.
 
Jiulize ni nchi yako tu yenye walimu?!
Walimu wa nchi zingine wanafanyaje?! Au watoto wa huko kote hawana nidhamu ila wetu tu?!
Mfano: Japan labda…
 
Nyie wanasiasa waoneeni huruma hao walimu mnao wakabidhi watoto wa aina hiyo

Mama samia unanasa kwenye mitego inayo haribu taifa kimaadili na kwa vile umenasa kwenye hayo basi la ushoga lipo njiani

Wazo la kwanza kuwawekea mfumo wao lilikuwa zuri sana lakini hili la kuwachanganya na wanafunzi wengine katika mfumo rasmi hapana

Nitajieni ni nchi gani ulaya na Amerika ambayo inatumia mfumo huu unao letwa tanzania.

Nadhani sasa tume halalisha mapenzi shuleni nadhani sheria za shule zirekebishwe swala la mapenzi na mimba lisiwe kosa tena si kwa mabint si kwa vijana.
Tuwaonee huruma walimu????? Watoto wengi hupewa mimba na walimu
 
Back
Top Bottom