Kwann watu wanaidharau degree ya Open University?

Wadau ni kwann mhitimu wa degree kutoka OUT anadharaulika na kuonekana kama degree yake haipo sawa kama degree nyingine kutoka vyuo vingine?

Kihistoria, kupata digilii ilikuwa dili sana. Yaani mtu mwenye nayo angejulikana kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba kadhaa. Taasisi za umma zilikuwa zikigombea wenye nazo hata kabla hawakuhitimu. Haikuwa ajabu mhitimu kuwa na barua tatu nne za taasisi za umma zikimtaka akaripoti kwao.

Kupata digilii ilikuwa ni kwa wachache. Wilaya nzimanzima zilikuwa zinatoa wanafunzi wachache "waliopasi" kwenda sekondari. Huko sekondari, wachache zaidi walichaguliwa kwenda sekondari ya juu. Kutoka huko sekondari ya juu, ni wachache sana waliochaguliwa kwenda kusoma digilii "Chuo Kikuu".

Ndio. Haikuhitajika kutaja jina la chuo. "Msimuone vile, jamaa anasoma Chuo Kikuu!!1!" Mkuu wa nchi ndiye aliyekuwa Mkuu wa Chuo.

Vyuovyuo vingine vilivyotoa elimu ya juu havikuruhusiwa kutoa digilii. Vilitoa "Diploma ya Juu" ambayo wenyewe walisema "ni sawa tu na digilii". Lakini wenzetu wa Chuo Kikuu hawakuwa wanatambua hilo la usawa. Baadhi ya kozi ilikuwa ukienda na Diploma yako ya Juu, hukupokelewa kusoma digilii ya Mastaz. Salama yako ilikuwa ukasome nje ya nchi walikokuwa wakitambua Diploma za Juu.

Nafikiri umepata picha kuhusu digilii ilivyokuwa dili.

Sasa mning'inio wa mawazo ya hivyo bado uko. Mtu akisoma digilii ya chuo kingine ambacho siyo "Chuo Kikuu", huonekana kutiliwa shaka hiyo digilii yake. Ndio utaona wengine wanaviita baadhi ya vyuo kuwa ni "vya kata". Dhana nzima ya chuo kuwa "cha kata" ni ileile: ilikuwa dili sana kusoma sekondari, hasa "ya kupasi". Zamani hizo kwamba ulisoma sekondari "binafsi" ilikuwa ni ushahidi kwamba wewe "hukupasi", na kwa hiyo siyo wa "viwango" kama wale waliokuwa shule za "kupasi", yaani za serikali.

Zilipokuja shule za kata, yaani kila kata iwe na shule ya serikali "ya kupasi", wanafunzi wengi walipata fursa ya kupata elimu ya sekondari. Na hivyo ile kujitutumua kwamba "nimepasi" iliisha.

Kuibuka kwa vyuo vingine vingi vinavyotoa digilii kulisababisha kupungua kwa makali ya kusema "niko Chuo Kikuu", kwa vile sasa ulianza kuulizwa, "Chuo Kikuu Kipi?"

Ndipo kikaja Chuo Kikuu Huria. Huria kwenye jina la Chuo Kikuu haliko kwa urembo. Lina maana chuo kikuu ni huria -- mtu yeyote apendaye kujiunga nacho anakaribishwa. Bila kujali kasoma kiasi gani. Bila kujali ana cheti cha kidato cha nne au cha sita. Mradi tu awe na nia (na ada!) ya kusoma. Walau ndivyo vilivyo vyuo vikuu huria vingine duniani.

Zamani, ili ujulikane "umepasi" kwenda sekondari, mara nyingi ni kwa vile sasa utapanda basi kwenda shule ya kutwa au ya bweni... Mning'inio wa mawazo kama hayo upo kwamba, ili ujulikane unasoma "Chuo", inabidi uwe uko "kampasi" au umepanga "geto"; unachukua "bumu". Sasa digilii gani unaweza kuchukua bila kukaa kampasi? Nini sasa faida ya kwenda "chuo"?

Hata kama digilii za vyuo vya matofali nyingine baadhi ya wanafunzi ni wavivu na wazembe, waishiao kutumia "madesa" yaliyopitwa na wakati, hujiona ni bora kuliko wale wa huria ambao inabidi wasome kweli mpaka wapate digilii zao.

Ndugu yangu, kwa kifupi mawazo-mgando ndiyo sababu ya kudharaulika kwa digilii za Chuo Kikuu Huria.

Yapuuze.

Angalia:

Best comment

Pamoja na Uchambuzi wako wa kisomi nashangaa neno degree/digrii limekushinda kabisa

Btw uzi umeishia hapa, hakuna kilaza wa chuo chochote anayejiona bora ataendeleza mjadala
 
Nashukuru kwa mchango wako mzur sanaa naomba kuuliza kwa miaka hiyo kuna chuo tofauti na udsm kilichokuwa kinatoka degree hapa tz? Msaada mkuu.
 
Back
Top Bottom