Kwanini Zitto na Lipumba wanajitenga na suala la Katiba Mpya?

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
549
785
Habari za asubuhi Wakuu.

Mimi nina maswali mengi yasiyo na majibu kuhusu vita inayoendelea ya Katiba Mpya.

Nimeshangaa sana kuona Zitto na Lipumba wamejitenga kabisa na hii Movement as if wao sio waathirika kabisa wa Katiba iliyopo.

Zitto amekuwa na hii Historia ya Undumilakuwili na usaliti kwenye harakati ila hata katika hili anakosa aibu kidogo hata ya kupaza sauti wenzie wasikamatwe?

Nimemsikia Mbatia kidoogo angalau na yeye aliongea kitu ila Zitto na Lipumba kimya.

Kama ndiyo aina ya Wanasiasa tulionao kweli tuna safari ndefu sana.
 
Nani aliyekwambia katiba ndo suruhisho ya matatizo Tanzania ? Tanzania ni moja ya nchi yenye katiba bora kabisa Africa tatizo lipo kwenye kutekeleza hyo katiba mnaweza kuwa na katiba mpya then viongozi hawataki kuitekeleza uoni kwamba utakuwa ni ujinga?

Mtanzania anataka maendeleo si katiba kwa maana katiba hii hii ndo imetupitisha ktk kipindi kigumu na tumekipita tena kwa amani kabisa na utulivu mnataka nn sasa??
 
Hapa ndo umekuja kumwaga pumba na uharo moja matata sana.
😂😂😂 Naona ndo mmeamka haya kavue Gwanda maana sasa imekuwa night dress Kamtoeni Kamanda wenu Mbowe kama Mwenyekiti ni Gaidi bhasi lazima taasisi itakuwa ya kigaidi tu.
 
Watu wenye akili kama Zitto na Lipumba hawawezi kujiingiza kwenye ma movement ya kijinga kama haya yanayo ratibiwa na CHADEMA! Wao baada ya kuona Magufuli kafariki na Rais Samia anaongea kistaarabu basi wakajua hapa ni mchekea.

Mbowe na wajinga wenzie wapigwe ndani hata mwaka mzima ili wapate akili.
 
Najitahidi kutunza kumbukumbu za hizi mambo.

Inasemwa,viongozi wapambanaji wa kisiasa mara nyingi huwa wanadondokea kwenye ufaulu na kushika hatamu, hebu tutunze hii kama mapambano ya kina mbowe yatazaa kile tunachokitaja sana.
 
Nani aliyekwambia katiba ndo suruhisho ya matatizo Tanzania ? Tanzania ni moja ya nchi yenye katiba bora kabisa Africa tatizo lipo kwenye kutekeleza hyo katiba mnaweza kuwa na katiba mpya then viongozi hawataki kuitekeleza uoni kwamba utakuwa ni ujinga?

Mtanzania anataka maendeleo si katiba kwa maana katiba hii hii ndo imetupitisha ktk kipindi kigumu na tumekipita tena kwa amani kabisa na utulivu mnataka nn sasa??
Lione kule
 
Siku utakapodhurika wewe na ukoo wako na KATIBA hii ndio utajua kama ni nzuri au Laa lakini utakuwa amefanya hivi sikushangai
20210716_160047.jpg

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Nani aliyekwambia katiba ndo suruhisho ya matatizo Tanzania ? Tanzania ni moja ya nchi yenye katiba bora kabisa Africa tatizo lipo kwenye kutekeleza hyo katiba mnaweza kuwa na katiba mpya then viongozi hawataki kuitekeleza uoni kwamba utakuwa ni ujinga?

Mtanzania anataka maendeleo si katiba kwa maana katiba hii hii ndo imetupitisha ktk kipindi kigumu na tumekipita tena kwa amani kabisa na utulivu mnataka nn sasa??

Mkuu wala usiwaombe kudai katiba mpya maana wataona wanahitajika, siku wakiitaka wataidai. Hao ukiwaambia wataishia kubeba ajenda za kuvurugana. Kila mtu aidai kivyake.
 
Nani aliyekwambia katiba ndo suruhisho ya matatizo Tanzania ? Tanzania ni moja ya nchi yenye katiba bora kabisa Africa tatizo lipo kwenye kutekeleza hyo katiba mnaweza kuwa na katiba mpya then viongozi hawataki kuitekeleza uoni kwamba utakuwa ni ujinga?

Mtanzania anataka maendeleo si katiba kwa maana katiba hii hii ndo imetupitisha ktk kipindi kigumu na tumekipita tena kwa amani kabisa na utulivu mnataka nn sasa??
Mojawapo ya Katiba bora Afrika?
Miaka 60 bado mnataka maendeleo chini ya Katiba hiyo bora. Miaka 60 bado tunajengewa vyoo na mabeberu. Miaka 60 bado maji ni shida kwa wananchi wengi. Miaka 60 bado shule zetu nyingi ni za matope na kwengine watoto wanasomea chini ya mti. Miaka 60 bado ni mtihani kupata dawa katika baadhi ya hospitali zetu. Miaka 60 bado mahabusu wanajisaidia kwenye ndoo na wanalala sakafuni. Miaka 60 bado tunahangaika kupeleka umeme kwenye vijiji vyetu. Miaka 60 bado tunapambana na utapia mlo.

Kama hali ni hivi chini ya hii Katiba bora basi wakati umefika wa kuiangalia upya.

Amandla...
 
Habari za asubuhi Wakuu.

Mimi nina maswali mengi yasiyo na majibu kuhusu vita inayoendelea ya Katiba Mpya.

Nimeshangaa sana kuona Zitto na Lipumba wamejitenga kabisa na hii Movement as if wao sio waathirika kabisa wa Katiba iliyopo.

Zitto amekuwa na hii Historia ya Undumilakuwili na usaliti kwenye harakati ila hata katika hili anakosa aibu kidogo hata ya kupaza sauti wenzie wasikamatwe?

Nimemsikia Mbatia kidoogo angalau na yeye aliongea kitu ila Zitto na Lipumba kimya.

Kama ndiyo aina ya Wanasiasa tulionao kweli tuna safari ndefu sana.
Yaani wewe unataka kila mtu afuate fikra za Mbowe? Kila siku mnasema nyie ndiyo wapinzani wa kweli mnaomba tena msaada kutoka kwao pambaneni kila mmoja ashinde mechi zake.
 
Back
Top Bottom