Kwanini Zitto na ACT Wazalendo wanamtetea Prof. Assad? Ni maslahi binafsi au ya Taifa?

Mathayo Fungo

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
319
510
KWANINI ZITTO NA ACT YAKE WAMEKURUPUKA KUMTETEA ASSAD? NI MASLAHI BINAFSI AU YA TAIFA? MTAZAMO WA MWANASHERIA NGULI

Nimeyaona maoni ya wengi katika hili la CAG Prof. Mussa Assad kurithiwa na Mkaguzi Mwandamizi (Senior Certified Auditor) na Mwanasheria Msomi Bw. Charles Kicheere.

Lakini miongoni mwa maoni ya ambayo hayapaswi kuachwa yapite yatanajisi taaluma ya sheria ni yaliyotolewa na Chama cha ACT na Kiongozi wake Zitto Kabwe.

Kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi ya Taifa Na. 11 ya Mwaka 2008 kifungu cha 6(1) "basic tenure" ya CAG ni miaka mitano na sheria inasema anaweza (Shall) kutumikia vipindi viwili vya miaka mingine mitano.

CAG anaulinzi mkubwa kisheria na moja ya ulinzi wake ni kuwa hawezi kuondolewa hivi hivi bila masharti kadhaa kufuatwa hasa akiwa katikati ya tenure yake.

Maana yake katika hiyo miaka mitano yake kabla hajaimaliza, iwe ya pili au ile ya mwanzo, kumuondoa sio jambo rahisi lazima utumie masharti ya Ibara ya 144(3) ya Katiba au yeye mwenyewe achukue hatua under subsection 2 ya hiyo Sheria ya Ukaguzi niliyoitaja hapo juu. Lakini kwa ujumla anaweza kuondolewa, si ngumu. Nitaeleza.

Najua kitu kilichowakanganya wengi na ACT kuudanganya umma ni neno "Shall" lililotumika katika Sheria ya Ukaguzi kwenye kifungu cha 6 na ndicho ACT wamekivamia na kufasiri kwa tafsiri SISISI ya kisheria kuwa lazima CAG aongezewe kipindi cha pili.

Kwa heshima na taadhima, Sheria hapo haijakusudia hivyo na ndio maana sheria haifasiriwi kwa matakwa ya mtu bali sheria zenyewe zinavyokusudia kufasiriwa katika muktadha wa jambo husika na lengo la mtunga sheria.

Katika muradi wa sheria na taratibu za kiutawala (admimistrative law point of view) sheria zinajulikana kuwa zitajitafsiri zenyewe na msingi unaokubalika ni kuwa kika ambapo tenure inapomalizika na kuwepo kwa kanuni ya kuongezewa tena kipindi cha pili neno "Shall" halina maana kama ilivyo katika Sheria ya Kufasiri Sheria (The Interpretation of Laws Act), hapa maana huwa ya kimazingira zaidi (contextual meaning) na haiwi LAZIMA bali INAWEZA.

Na moja kwa moja maoni yangu hapa ni kuwa kuongezewa tenure ya pili Mtendaji yeyote mwenye tenure ya vipindi viwili na hata Rais mwenyewe sio "automatic" lazima kuwe "subject to good performance."

Na anayeamua akuongezee tenure ya pili, hiyo sheria haijambana, ni yule yule mwenye mamlaka ya kuteua na kukutengua.

Rais anapewa mamlaka hayo kwa CAG na watendaji wengine Serikali aliowateua kwa sheria yoyote kwa mamlaka aliuonayo katika Ibara ya 36. Tena 36(3) ndio inampa mamlaka ya jumla zaidi ya kudeal na tatizo lolote kwa nia ya kuweka utulivu katika utumishi kwa kuweza kumtengua mtu yeyote aliyemteua.

Ukifasiri neno "shall" katika Sheria ya Ukaguzi ili kumtetea CAG Assad kwamba ilikuwa lazima aendelee miaka mitano ya pili ni kuleta dhahama kubwa nchini inayoweza kushawishi hata Uchaguzi Mkuu wa Mwakani usifanyike. Najua utashangaa!!!

Ndio, tafsiri ya Zitto na wenzake ni ya hatari zaidi kwa nchi kwani ukisoma Ibara ya 40 ya Katiba inapozungumzia Rais aliyeko madarakani kwa kipindi cha miaka mitano ya mwanzo kuwa anaweza kuchaguliwa tena kwa miaka mingine mitano ya pili na ya mwisho neno lililotumika ni "shall."

Kama tafsiri SISISI na "shallow" ya ACT ni ya kufuatwa basi kwa muktadha wa neno "Shall" pia katika Ibara ya 40 ya Katiba, Rais Magufuli naye mwakani hakuna haja ya kupimwa utendaji wake kwa kurudi katika sanduku la kura, aendelee tu, kusiwe na uchaguzi, aapishwe moja kwa moja kuendelea na Urais maana "shall" ina maana ya LAZIMA.

Lakini hapana, muradi wa "shall" katika masuala ya utawala sio kama inavyotumika katika sheria za kawaida, hapa bado dhana ya mhusika kuwa "subjected to good performance" kwa kutazamwa utendaji wake kama unaridhisha mamlaka ya uteuzi (kwa kesi ya CAG) na kwa kurudi kuomba kura tena kwa wananchi (kwa kesi ya Rais) ndio utaratibu kabla ya kulamba awamu ya pili.

Maoni yangu ya kitaalamu ni kuwa CAG anayemaliza muda wake kesho hakuonewa na kama ni kuonewa au aliyemteua ana nia mbaya angeweza kuondolewa hata kabla hajamaliza miaka hii mitano.

Ibara ya 144(2) inampa madaraka Rais kumuondoa CAG kwa sababu ya utendaji mbovu, maradhi au sababu nyingine yoyote.

Nimeona wengi wanasema Rais hawezi kufanya hivyo mpaka aunde Tume, si kweli. Watanzania tuachane na kasumba ya kutosoma kwa umakini.

Tuzisome sheria vyema na tunaposhindwa kuelewa tuwatafute wataalamu sio wanasiasa.

Katika Ibara ya 144(3) Rais ataunda Tume (If) kwa maana ya "kama" ataona kuchunguza sababu hizo za kumuondoa CAG kunafaa kuchunguzwa. Maana yake akijiridhisha hana haja ya kuunda Tume.

Kisheria na Kikatiba, namsifu sana JPM na wataalamu wake wa sheria, hakika ni wabobezi, wanazisoma sheria zetu kwa utulivu na kuzifasiri kwa mujibu wa viapo vyao.

Naamini Rais hakuwa na jambo baya la kutaka kumfukuza CAG isipokuwa "subject to good performance" anahitaji kasi zaidi katika eneo hilo na utulivu zaidi na kuaminika zaidi kwa kiongozi wa muhimili huo ambako Assad alishafeli kwa kufikia hatua ya kugombana na mhimili wa Bunge.

Kwa uchambuzi huu kudai Rais kavunja Sheria ni uchochezi mkubwa usiofaa kufumbiwa macho.

Imeandikwa Na,
Grayson K, Wakili wa Kujitegemea.
 
Rais anapewa mamlaka hayo kwa CAG na watendaji wengine Serikali aliowateua kwa sheria yoyote kwa mamlaka aliuonayo katika Ibara ya 36. Tena 36(3) ndio inampa mamlaka ya jumla zaidi ya kudeal na tatizo lolote kwa nia ya kuweka utulivu katika utumishi kwa kuweza kumtengua mtu yeyote aliyemteua.

Ukifasiri neno "shall" katika Sheria ya Ukaguzi ili kumtetea CAG Assad kwamba ilikuwa lazima aendelee miaka mitano ya pili ni kuleta dhahama kubwa nchini inayoweza kushawishi hata Uchaguzi Mkuu wa Mwakani usifanyike. Najua utashangaa!!!

Ndio, tafsiri ya Zitto na wenzake ni ya hatari zaidi kwa nchi kwani ukisoma Ibara ya 40 ya Katiba inapozungumzia Rais aliyeko madarakani kwa kipindi cha miaka mitano ya mwanzo kuwa anaweza kuchaguliwa tena kwa miaka mingine mitano ya pili na ya mwisho neno lililotumika ni "shall."

Kama tafsiri SISISI na "shallow" ya ACT ni ya kufuatwa basi kwa muktadha wa neno "Shall" pia katika Ibara ya 40 ya Katiba, Rais Magufuli naye mwakani hakuna haja ya kupimwa utendaji wake kwa kurudi katika sanduku la kura, aendelee tu, kusiwe na uchaguzi, aapishwe moja kwa moja kuendelea na Urais maana "shall" ina maana ya LAZIMA.

Lakini hapana, muradi wa "shall" katika masuala ya utawala sio kama inavyotumika katika sheria za kawaida, hapa bado dhana ya mhusika kuwa "subjected to good performance" kwa kutazamwa utendaji wake kama unaridhisha mamlaka ya uteuzi (kwa kesi ya CAG) na kwa kurudi kuomba kura tena kwa wananchi (kwa kesi ya Rais) ndio utaratibu kabla ya kulamba awamu ya pili.

Maoni yangu ya kitaalamu ni kuwa CAG anayemaliza muda wake kesho hakuonewa na kama ni kuonewa au aliyemteua ana nia mbaya angeweza kuondolewa hata kabla hajamaliza miaka hii mitano.

Ibara ya 144(2) inampa madaraka Rais kumuondoa CAG kwa sababu ya utendaji mbovu, maradhi au sababu nyingine yoyote.

Nimeona wengi wanasema Rais hawezi kufanya hivyo mpaka aunde Tume, si kweli. Watanzania tuachane na kasumba ya kutosoma kwa umakini.

Tuzisome sheria vyema na tunaposhindwa kuelewa tuwatafute wataalamu sio wanasiasa.

Nimependa sana mafungu haya ya maneno.
 
Zito Kabwe ni mpiga dili, H.Polepole alishasema harudi Bungeni 2020 hata kwa mbinde, sasa ana haha, muda siyo mrefu atahamia kwenye udini.
Kwisha habari yake!
Kweli mkuu zito kila tawi analodandia linakwanyuka
 
Asad ameondoshwa bila ya kupewa taarifa,hii peke yake inaonesha mataga mlikuwa na bifu nae kwa vile kafichua ujinga wenu na ufisadi mliokuwa mnaufanya.
 
Inasemekana kuwa Assad alikuwa mpambe kwenye harusi ya Zitto, kwa hiyo wanajuana. Inawezekana Zitto alikuwa na influence katika matamko unprofessional ya Assad.
 
Inasemekana kuwa Assad alikuwa mpambe kwenye harusi ya Zitto, kwa hiyo wanajuana. Inawezekana Zitto alikuwa na influence katika matamko unprofessional ya Assad.
Huo ndio ukweli pigia mstari kunakipindi nilidhani kuwa asad na zito ni ndugu
 
Okay na Hii?
Screenshot_20191104_025212_com.instagram.android.jpeg
 
Mwanasheria Msomi
Mimi nina swali hapa tu.

1. Kwanini wanasheria huwa wanajitambulisha kwa kuanza na maneno "Mwanasheria Msomi" ?

2. Je wakijitambulisha au kujiarifisha kwa kusema "Mwanasheria fulani" kuna tatizo gani ?
 
Back
Top Bottom