Kwanini Zitto anafaa kuwa Rais 2015...

nice 2

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
747
520
Na Ezekiel Kamwaga | Raia Mwema Toleo la 272 | 12 Dec 2012


272_zitto.jpg


NINAAMINI kwamba makala haya yataniletea upinzani mkubwa sana kwa baadhi ya watu ambao hawataki kusikia mtu akisema Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Kabwe Zitto, anafaa kuwa rais.

Kwa bahati mbaya, wengi hawamfahamu vizuri au taarifa walizonazo zinatokana na wale wenye chuki binafsi naye.

Ni muhimu kwa taifa letu kuwa na mijadala mipana kuhusu watu wanaotaka kugombea nafasi kubwa na nyeti hapa nchini kama urais. Rais hawezi kuchaguliwa eti kwa vile ametoka katika chama fulani, dini fulani, ana mwonekano mzuri au kabila fulani.

Rais anachaguliwa kutokana na ajenda anazoleta mezani. Barack Obama alikuja na sera za mabadiliko (change) na atahukumiwa kwa hilo. Ni lazima tujiulize, wagombea wetu watakuja na hoja gani mezani?

Kwa nini Zitto Kabwe?
Katika mojawapo ya maandishi yake, mwanasiasa na mwandishi wa iliyokuwa Urusi, Leon Trotsky, alipata kusema kwamba kiongozi mzuri ni yule mwenye uwezo wa kuandika mawazo yake.

Kwamba ni hatari sana kwa taifa kuwa na kiongozi ambaye hawezi kueleza kwa maandishi ya walau kurasa tatu mawazo yake kuhusu mambo mbalimbali.

Trotsky alikuwa ni mwandishi mzuri na pengine aliandika hivi ili aonekane kama mbadala sahihi wa Vladmir Lenin kuliko Stalin.

Hata hivyo, ukiangalia mifano mbalimbali, utaona ukweli wa mawazo haya ya Trotsky. Julius Nyerere ameandika mara ngapi kuhusu masuala mbalimbali? Thomas Jefferson miongoni mwa marais mahiri kabisa wa Marekani alikuwa mwandishi mzuri.

Angalia maandiko ya Rais wa zamani wa Senegal, Leopord Sedar Senghor. Nilikuwa msomaji mzuri wa makala za Thabo Mbeki katika gazeti la chama cha ANC wakati alipokuwa Rais wa Afrika Kusini.

Na hadi sasa, huwa nafurahia sana kusoma makala za Yoweri Museveni kila anapoandika iwe katika vitabu au magazeti. Hata kama hukubaliani na kiongozi kwenye masuala fulani fulani, inasaidia kama unaona anawaza nini.

Miongoni mwa watu wanaotajwa kuwania urais wa Tanzania, ni Zitto Kabwe pekee ambaye anaandika mara kwa mara kwenye magazeti na mitandao mbalimbali.

Makala zake nyingi zina mwelekeo wa kiuchumi lakini huwezi kulaumu kwa sababu kitaaluma ni mchumi. Hata hivyo, ameandika pia mambo kuhusu mtazamo wake kisiasa na kijamii.

Natoa changamoto kwa wenzangu mniambie mmeona makala za akina nani wengine wanaotajwa kuwania urais zilizotoka katika magazeti au mtandaoni katika siku za karibuni.

Obama alikuwa hafahamiki sana lakini watu walimfahamu kwa kazi zake bungeni na za kiuandishi wakati alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Harvard. Alikuwa miongoni mwa waandishi wa jarida la chuo.

Unamchaguaje mtu ambaye hawezi kukaa chini na kutafakari kuhusu lolote na kutoa mchango wake kuhusu jambo analolifahamu? Huo ni uchoyo wa kitaaluma.

Zitto pia, pengine, ndiye mwanasiasa ambaye anaweza kufiti kwenye mazingira mengi ya kijamii kuliko wengi wa wanasiasa nchini.

Nimemuona kwenye mikutano au mijadala ya kisomi katika vyuo vikuu ambako alipokewa vizuri tu. Nimemuona katika mijadala ya asasi za kijamii ambapo alifiti vizuri tu (kabla ya kuingia kwenye siasa kindakindaki alifanya kazi za kiharakati).

Nimemuona akizungumza vijijini kwao mkoani Kigoma na ungemuona sawa tu na wananchi hao. Nimemuona mpirani akishabikia klabu ya Simba au timu ya taifa kama shabiki mwingine yeyote.

Nimemuona akichanganya na wale wanaoitwa celebrities katika muziki na filamu na nikamuona amepokewa vizuri tu kiasi cha kuimba nao wimbo wa kumchangia msanii Sajuki aliyekuwa akiumwa.

Amekusanya pia wasanii wa mkoa wake na kutoa wimbo wa kuhamasisha maendeleo ya mkoa huo uitwao Leka Tutigite.
Kwenye hili, Zitto amefuata wosia wa mwanafalsafa Conficus aliyeasa kwamba kiongozi ni lazima awe karibu na jamii na asionekane amejitenga nayo.

Katika dunia hii iliyo kijiji, unahitaji rais anayefahamu mawazo na hisia za makundi mbalimbali ya kijamii. Unahitaji pia rais ambaye makundi mengi kadri iwezekanavyo yanaweza kujihusisha na harakati zake.

Majuzi hapa, katika gazeti hili hili, Zitto ameandika makala kuhusu namna Mkoa wa Lindi unavyoweza kuwa Sri Lanka ya Tanzania. Angeweza kuandika kuhusu Kigoma lakini akaandika kuhusu rasilimali za mkoa wa Lindi usio wake.

Hili lilionyesha namna anavyofikiri kama Mtanzania na si kama Mha. Lakini pia ameonyesha namna gani anafahamu matatizo ya Watanzania kiuchumi na utatuzi wake.

Tusisahau pia kwamba Zitto amejikita zaidi katika usomi wa masuala ya madini na nishati. Ninaamini kwamba huko tuendako tunahitaji rais mweledi katika masuala hayo. Huko tuendako, gesi na mafuta yatakuja kuwa rasilimali muhimu zaidi hapa nchini. Nani miongoni mwa wanaotajwa ana uelewa wa mambo haya kuliko Zitto?

Mimi pia ni miongoni mwa wale wanaoitwa romantics katika siasa. Kwamba Zitto ni mtoto wa mkulima. Hatokani na familia zile za "uchifu mamboleo" zinazoanza kujitengeneza hapa nchini.

Za mtoto wa rais mstaafu anayetaka urais. Za mke wa waziri ambaye ni mbunge wa viti maalumu. Bado wapo miongoni mwetu wanaotamani wanasiasa waliojitengeneza wenyewe. Tunaitwa romantics. Zitto anaangukia katika kundi hili la waliojitengeza wenyewe.

Katika umri wake, Zitto ametengeneza urafiki na kufahamiana na watu ambao wanasiasa wengine hata hawawajui. Tumeona mara ngapi Zitto akikutana na watu kama Mahathir Mohamed, yule mwanasiasa aliyeibadili Malaysia kutoka nchi masikini hadi tajiri?

Tumemuona akikutana na akina Keneth Kaunda. Ninafahamu ana mawasiliano ya karibu na Raila Odinga. Zitto anaaminika na karibu wakuu wote wa vyombo vya usalama nchini. Unahitaji mgombea anayeaminika na vyombo nyeti kama hivyo.

Ninafahamu kwamba kuna viongozi wa juu na waliomzidi umri Zitto hapa nchini ambao walikuwa hawafahamiani na viongozi mashuhuri wa kitaifa wa Tanzania na walikutanishwa nao kupitia kwa mwanasiasa huyu.

Watu wengi hawafahamu lakini Zitto ni mwanajumui wa Afrika (Pan Africanist). Huko nyuma ilikuwa miongoni mwa sifa muhimu za mtu kuwa kiongozi. Umujumui, pamoja na mambo mengine, unampa fahari mtu mweusi. Unampa fursa ya kufahamu mtu mweusi alikotoka.

Kwangu mimi, hii ni sifa nzuri kwa kiongozi wa nchi ya kiafrika. Tuliwapenda kina Nyerere na Nkrumah kwa sababu walikuwa wanajumui wazuri. Waliweza kuzungumza na wazungu na kueleza msimamo wao pasipo waoga.

Kama una rais mpenda uzunguni, anayetamani kuwa mzungu na asiyejua nini kilio cha mwafrika, unategemea nini kutoka kwake. Kwangu mimi, uanajumui unamfanya kiongozi kuwa mzuri.

Zaidi ya nusu ya Watanzania wana umri chini ya miaka 30. Itapendeza zaidi kama mtu mwenye maono, elimu, umri na kipawa cha Zitto akawa kiongozi wa taifa la namna hiyo badala ya kuwa na Rais ambaye anawakilisha asilimia 20 ya Watanzania kiumri.

Hebu tumchambue Zitto Kabwe wakti ungalipo. Lakini, kama atawania urais mwaka 2015, na kama Allah atanijalia uzima, kwa chama chochote au kama mgombea binafsi, ana uhakika wa kura yangu.
Nimefungua mjadala
 
Na unaweza leta uzi wa January Makamba pia sababu wanashabiana kwa sifa.
 
Mkuu naona unautafuta urais kwa njia zote!tulia kwani muda ukifika utapata na kama imeandikwa kwenye vitabu vya Mwenyenzi Mungu kuwa utakuwa rais basi utakuwa lakini kama ni tofauti na hapo basi ndo hivyo tena.
 
By Zitto May 2009

Nimezungumza na Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima ndugu Kibanda kuhusu suala hili na tumeelewana. Pale ambapo wao wana makosa ya kihariri wamekiri na pale ambapo mimi nina makosa nimekiri. Kwa upande wangu suala hili limekwisha, nimepiga mstari na kuganga yajayo. Ninaamini siku za usoni Tanzania Daima watakuwa makini na habari zao hasa zile zinazoweza kuleta migongano ndani ya chama.

Kuna mambo mengi ya kutuunganisha ndani ya chama kuliko kutugawa.
Nimemhakikishia kuwa mie simo kwenye mbio za Urais maana kwa maoni yangu hili ndilo jambo ambalo linatumika sana kutugawa wana chadema. Wakati utakapofika ambapo chama kitatangaza wanachama wake wajitokeze kuomba kuwa wagombea na hatimaye mgombea kupatikana kwa njia ya kidemokrasia, nitamwunga mkono mgombea huyo wa chama changu.

Suala la Rais Kikwete kusema atapenda Rais ajaye awe wa kizazi kingine cha vijana zaidi, nimewaeleza halikusema kwa siri au kunong'ona. Chief Kibanda pia alinikumbusha kuwa Rais alishawahi kusema hili miaka ya nyuma. Ni maoni tu ya Rais. Na kwamba vijana wenye uwezo, maadili na wazalendo wapo na wale wanaotimiza vigezo vya umri wasisite kujitokeza.

Kwa upande wangu suala hili limekwisha. Natawatakia kila la kheri
 
Urais si sawa na kutafuta uchumba ambapo lazima ujibaraguze kwa mwanamke na kumpa ahadi hewa nyingi ili tu umpate. Tofauti yna kutaka mchumba rais anatakiwa apendekezwe na watu na si ajipendekeze na kujibaraguza kwenye vyombo vya habari. Watu ndio wenye uwezo wa kusema wanataka nini?
 
Kwa faida ya wengine, who is ezeke..kamwaga


NIMEFURAHISHWA SANA NA KITENDO CHA MWANA JF KUHOJI KUHUSU KUONDOKA KWA MWANDISHI EZEKIEL KAMWAGA WA MWANAHALISI, INGAWAJE NIKO NJE YA NCHI NAOMBA NIWAONJESHE KIDOGO KUHUSU HUYU KAMWAGA ALIVYOANZA KUTUMIWA NA CCM NILIWAHI KUTUMIWA MAKALA HII NA RAFIKI YANGU AMBAYE YUKO TANZANIA ALIANDIKA MAKALA KWENDA MWANAHALISI LAKINI HAIKUCHAPWA, SASA KUBENEA ATWAMBIE KWANINI HAKUCHAPA MAKALA HII? NA EZEKIEL KAMWAGA YUPO SIMBA SASA HATUTAMWONA TENA MWANAHALISI!
Saed_Kubenea.jpg



EZEKIEL KAMWAGA MWANAHALISI SIO UWANJA WA POROJO NA PROPAGANDA

Katika gazeti la Mwanahalisi la jumatano,Machi30-Aprili5,2011 mwandishi Ezekiel Kamwaga aliandika makala yenye kichwa cha habari Msilale, CCM hawajaanza kugombana leo, nimeisoma mara tano makala hii ila nimeshindwa kuelewa iwapo makala hii kweli ilipaswa ichapwe kwenye gazeti la Mwanahalisi au Rai la Rostam Aziz?

Makala hiyo ya Ezekiel Kamwaga imetushangaza watu wengi hasa kwa jinsi ilivyoshindwa kuzama kwenye hoja za msingi kwanini CCM sasa inayumba kuliko wakati wowote katika historia ya chama hiko? Mimi nilitegemea Kamwaga atwambie kiundani je CCM ilipokumbwa na migogoro ilikuwa chini ya uwenyekiti wa nani? Chukulia mfano wa vuta nikuvute ya Nyerere na Kambona au kina Kassela Bantu, ikumbukwe kuwa wakati ule CCM ilikuwa chini ya Mwalimu Nyerere na hata ulimwengu mzima unamfahamu Nyerere ni nani katika unguli wa siasa za Afrika. Sasa Kamwaga anapodai tena kwa maneno rahisi tu kuwa kwa vile kipindi kile CCM au TANU ilipita salama basi hata awamu hii itapita salama! Hapa anatudanganya kwa maana anataka kumlinganisha Nyerere na Kikwete kiuongozi kitu aambacho hakiwezi kutuingia akilini hata kidogo.

Labda tuchukulie mfano rahisi tu utamlinganisha vipi Kikwete ambaye anadanganywa kila siku kiasi cha watu kumchakachulia mafuta ya gari na Nyerere ambaye hakutaka mzaha hata kidogo? Hapa ni dhahiri kuwa Nyerere na Kikwete hawana kinachowakutanisha kiuongozi hata kimoja kama Nyerere ni 70 basi Kikwete ni hasi (-)70 na hapa Kamwaga anapaswa kutambua kuwa uongozi huo uwe wa kitaifa au chama cha CCM.
Historia ipo wazi kuwa Kikwete hajapitia shida, hajui changamoto zozote ndio maana hata zinapoibuka hawezi kuzitatua, ndio maana kwa udhaifu wake huo ameshindwa kujipambanua yuko kwa wapinga ufisadi kina Mwakyembe na Sitta au kwa Lowassa na Rostam Aziz, huyu ndio Kikwete ambaye CCM inazidi kumfia mikononi mwake, huyu ndiyo Jakaya Kikwete aliyeshindwa kufanya kampeni kwa kutumia makada wa CCM badala yake akafannya kampeni za BMW yaani Baba, Mama na Watoto, au basi Kamwaga anataka kutuchekesha kwa kulinganisha uongozi wa Philipo Mangula na Makamba.

Lakini kuna la zaidi katika makala ile ya Ezekiel Kamwaga ambayo nathubutu kuiita ni ya kipuuzi tu kwa maana inaonyesha jinsi gani mwandishi anatoa hoja mfu ambazo hata kama kuna ufufuko siku ya mwisho basi haziwezi kufufuka, lakini mimi kama mtu mwenye uzoefu na wanahabari wa taifa hili ambao ninawafahamu vizuri halafu na uzoefu na watu wa propaganda wa CCM na michezo yao michafu huku wakijijigamba kuwa hakuna chombo cha habari Tanzania kisichokuwa na bei kwa maana kuwa wanaweza kumhonga mwandishi huyu au yule nitumie fursa hii kuweka wazi kuwa Ezekiel Kamwaga ameingia kwenye mtego huu na yeye amenaswa sasa sijui kwa shilingi ngapi? Kwa maana kwa mwandishi kijana wa aina yake nilimtegemea hata kama kweli analenga kuandika makala ya mtindo ule basi angeandika hoja za msingi kuliko kujaza kurasa za gazeti kwa manenno ya kutumwa na Yusuph Makamba au Hizza Tambwe.

Jinsi makala ya Kamwaga ilivyokuwa ya kusifia uimara wa CCM ambao kiuhalisia kwa hivi sasa haupo tena mimi nilidhani iimeandikwa na Ridhiwan Kikwete au Miraj Kikwete au hata Mama Salma Kikwete ambao wanakila sababu ya kutetea hata yale yasiyokuwepo kwavile tu CCM ndio inawapa kula si baba yao Kikwete ndio mwenyekiti? Sasa yeye Kamwaga amepewa nini mpaka afanye kazi isiyomhusu?
Nichukue fursa hii pia kumkubusha kuwa anachofanya anajiharibia mwenyewe na katu hawezi kuliharibu Mwanahalisi kama ametumwa kufanya hivyo, watanzania wanafahamu kuwa Saed Kubenea ni mtetezi wao, wanajua kuwa kina Mwangulumbi, Mbaga, Assenga na Ndimara Tegambwage ni watu makini sana. Watanzania wanakumbuka kuwa umaarufu wa Mwanahalisi haujaja kwa kujipendekeza kwa CCM bali kwa jasho na damu ya Kubenea na Tegambwage ,nani asiyekumbuka jinsi wanaharakati hawa walivyopigwa mapanga na kumwagiwa tindikali? Hivyo anapotokea mpuuzi kama Ezekiel Kamwaga ambaye ametumwa na wapuuzi fulanifulani ambao ikibidi tutawataja wanaotaka kutuharibia gazeti hili sisi ni lazima tuseme kwa maana tunajua fika kuwa bila Mwanahalisi au Raia Mwema tusingekuwa hapa tulipo, tusingekuwa na uwezo wa kumhoji Rostam au Lowassa, mchango wa magazeti haya mawili ni mkubwa sana katika kuelekea mageuzi ya kweli nchini hivyo hatuwezi kufungia macho kadudumtu yoyote anayeleta porojo na propaganda chafu kwenye gazeti hili la Mwanahalisi mtetezi wa wanyonge wa taifa hili.


Kwanza kwa taarifa yake Kamwaga asidhani kuwa hao walioumtuma huwa hawasomi Mwanahalisi, aache upuuzi kwa taarifa yake kila jumatano Salva Rweyemamu lazima anunue gazeti la Mwanahalisi na Raia Mwema na ampelekee huyo Kikwete, amini usiamini hata Ridhiwan, Miraj, Salma, Makamba, Tambwe na wabunge wote wakitoa tamko tu lazima wakimbilie kuona waandishi makini wa Mwanahalisi na Raia Mwema wameandika au kuchambua vipi hicho walichozungumza na mara nyingi wamekuwa wakibadili mienendo yao kwa kweli Mwanahalisi sio chombo cha kubeza hapa hakuna porojo kuna uchambuzi , hakuna propaganda kuna habari za kitafiti sasa iweje Ezekiel Kamwaga afanyie kazi ya Hizza Tambwe kwenye gazeti hili? Haiwezekani!


Najua kwavile huyu Ezekiel Kamwaga ameshalambishwa asali ya pesa mpya za benki kuu ataibuka harakaharaka na kunijibu lakini hii haina maana kama atashindwa kuweka bayana kwanini ameanza kuandika makala zisizofanana na Mwanahalisi au zilizo chini ya kiwango tena hali hii imejitokeza ghafla? Najua haya hawezi kujibu kwasababu anaujua ukweli, labda mimi naona kuliko kulumbana na ukweli ninaomwambia ni bora akahama Mwanahalisi kisha aende Mtanzania, Uhuru au Mzalendo huko na imani kuwa atafanya kazi yake vizuri lakini sio humu, akifanyia humu hatutamvumilia kwa maana porojo na propaganda hazitakiwi humu Mwanahalisi.


Halikadhalika labda nimpe siri moja Ezekiel Kamwaga ambayo itamsaidia kama kweli anataka kufanikiwa huko kwenye jukwaa lake jipya la CCM , kwa kawaida ukiwa bongo lala kama wewe wa kusifia tu watakudharau huko CCM hata wenyewe sikuhizi wanataka watu wenye uwezo wa kuhoji na kutoa changamoto hivyo jijengee utamaduni wa kuwa huru kimawazo ndio watakuheshimu huko CCM vinginevyo kwa jinsi upeo wako na maandiko yako yalivyo ya kishabiki bila shaka na wewe utaonekana gamba tu halafu watakuvua kwasababu huna faida kwao.
Hivi wewe Kamwaga unadhani kwa mwendo unaokwenda nao utadumu humu Mwanahalisi? Au unadhani kina Saed Kubenea watakuvumilia kupotosha umma? Bila shaka haiwezekani tayari maandishi yameshaandikwa ukutani siku zako za kukaa humu Mwanahalisi zinahesabika, na hata wakikutetea hatutakubali tutahoji na ikibidi tutajitokeza waziwazi hata kwenye TV kama umoja wa wasomaji wa Mwanahalisi na kuweka wazi kuwa HATUKUTAKI!

Fanya toba , omba msamaha anza upya vinginevyo utaangamia kwenye anga la habari za kiuchambuzi, mwishowe nitoe angalizo kuwa uchambuzi wangu umetawaliwa na hoja hivyo hata ikibidi kujibiwa iwe kwa misingi ya hoja hivohivyo lakini pia wakati ukijiandaa kujibu tuhuma hizi Bwana Ezekiel Kamwaga kumbuka kuwa hoja sio wewe kutetea CCM bali ni kwanini unafanya kazi ya Hizza Tambwe na Yusuph Makamba kwenye gazeti makini la Mwanahalisi?....Tafakari!


Mwandishi wa makala haya ni Ilunga Msekela , ni msomaji mkererketwa wa Mwanahalisi, aliwahi kusoma chuo kikuu Makerere cha nchini Uganda na ni mwanahabari katika moja ya mshirika ya kimataifa nchini ,anapatikana kwa anwani ya barua pepe; mpambanaji@live.com
 
hivi ni yule kamwaga w sport Kizaazaa?Kule kuna vichwa maji wengi sana.wanaongea vitu vya kupata palepale ktk mjadala.Na si vitu mtu alivyojiandaa kuja visema na alivyowahi vifanyia kazi.
 
EZEKIEL nilimtumia msg juzi.kuwa nae tofauti katka hoja zake,nilikubaliana na baadhi ya hoja,ila na kataa hoja moja ZITTO hanA SIFA ya kua RAIS..mimi nafanya kazi kigoma kaskazini ,kuna matatizo mengi sisi wananchi hatujui mfuko wa jimbo unafanyaje kazi,maji,barabara baadh ya vijiji ni tatizo,usafiri,nauli ni kubwa kuliko uhalisia mfano kutoka mkigo mpaka mjini kigoma nauli elfu nne mpaka elfu tano na nikilometa 35,wakati kutoka mtwara mpaka LIND nauliI 3500 ,na nizaid ya kilometa 78;na nimemwambia mara nyingi ktk mitandao ya kijamii,kuna wale wanao ishi pemben ya ziwa,MWAMGONGO sijasikia anasema chochote,yeye anatafuta ishu ambayo TAIFA ZIMA IMEITOLEAMACHO NDO ANAZUNGUMZA.kamwaga njoo kigoma kask sanasana njoo KIJIJI CHA NYARUBANDA
 
Sifa moja ya huyu dogo ni ubishi.....
Kijana alikataa katakata kwenda chuo baada ya kumaliza form six, akadai atanyoosha maisha yake hivyohivyo!!!
Hii ndio matatizo yake..kajaa hoja za kitoto!!!
 
Ukweli Zitto anaweza kua anafaa kua Rais kwan mm sjawah kuona kashfa dhidi yake inayothibitishika zaid ya udaku tu na zaid mambo mengi ya kizalendo nimeona akiyafanya.

Ila hawa ambao tunajua kabisa kua n wanafiki wanapojiingiza kumtajataja Zito na Urais na kujifanya kumpigia debe ndio wanaonza kumtia madoa. Mana unapopigiwa debe na mnafiki unafanya watu waanze kukutilia shaka naww.

Binafsi naomba kama kweli wanadhan Zitto anafaa uraisi wake kimya mana kujiingiza kumnad ni kumapaka shombo kijana wa watu...labla kama wanafanya kwa nia ya kuigawa CDM then hiyo kwao ina faida bas kina Zitto wasikae kimya.
 
Heshima kwenu great thinkers, mnajadili hoja au mnamjadili mtu?
 
Huwa namsikiliza sana Dr Slaa kwa busara na uzalendo wake nafurahishwa sana. Enzi nikiwa mwanafunzi pale providence, usa nilikuwa nafurahishwa sana na mwalimu mmoja maana kila alichokuwa akikifundisha kinaeleweka na kinamwingia mwanafunzi na wanafunzi tulikuwa tukimsifu. Sasa kati ya walimu wote 5 waliwokuwa wakinifundisha ni huyo tuu pekee nilimwelewa na kufaulu somo lake vizuri sana. Hapa napenda kumfananisha Dr Slaa na huyo mwalimu kwamba wanasiasa wote hakuna anayenivutia kama Slaa kwa uzalendo na ujasiri wake kwa watz.
 
Na Ezekiel Kamwaga | Raia Mwema Toleo la 272 | 12 Dec 2012


272_zitto.jpg


Hebu tumchambue Zitto Kabwe wakti ungalipo. Lakini, kama atawania urais mwaka 2015, na kama Allah atanijalia uzima, kwa chama chochote au kama mgombea binafsi, ana uhakika wa kura yangu.
Nimefungua mjadala

Heshima kwenu great thinkers, mnajadili hoja au mnamjadili mtu?

Kwa sababu hukuweka YOUR TAKE: Ulichokiuliza kwenye hiyo post yako ya pili kwenye uzi huu ni sawa na kushidwa kujisoma.
 
Back
Top Bottom