Kwanini Zitto alitumia nembo ya Bunge kuandika barua binafsi kwa Benki ya Dunia? Kwangu mimi huko ni kuhalalisha 'kushughulikiwa' na Bunge

labda tuanzie hapa kwani kunakosa lipo hapo au ni sheria au kanuni ipi imevunjwa...!? tukumbuke pia ni mbunge halali aliyechaguliwa na wananchi na hapo pia alikua anawawakilisha wananchi wake kama mbunge hakua anaisemea familia yake. na ndio maana alianza kwa kujitambulisha wadhifa wake na kuweka dhumuni kuu la barua.
Majibu atayatoa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
 
Asije akalia na kusaka huruma ya wananchi!
Mkuu hapa umetumia maneno kama niliyo yasema usiku wa manane uliopita, tofauti ni lugha tu.
Tena nikaongezea kwamba anajua sheria na taratibu za mchezo aliojiingiza.
Mchezo wenyewe anachezea ktk mazingira ambayo mipaka ya sheria zake za vita kama hivi alivyo anzisha hazijulikani vizuri.
Asije kulia kachezewa faulo, hajatendewa haki wakati haki zenyewe hazija ainishwa vizuri kwenye vita hivi.
 
Sio nembo ya bunge tu, Zitto kanikosea hadi mm maana kwenye barua kaniongelea kwa niaba yangu kama Mtanzania wakati sijamtuma.

Ana uhalali gani kuniongelea wakati mm sio mkazi wa Kigoma mjini?
amemuongelea mama/dada yako mwenye mimba anayenyimwa haki ya kupata elimu. sasa ukitaka akuongelee na wewe kaitege wakufanye upate mimba huku unasoma.
 
Una kipimo gani objective, concrete, measurable na factual cha kuonesha maneno ya barua hii ni ya uwakilishi na ya barua hii ni ya mtu binafsi?

Huoni kwamba umeleta mambo ya opinion na speculation hapa?

Give us facts please, not speculations and opinion.

You are supposed to be a lawyer. You know about facts.

What are the facts?

Sent using Jamii Forums mobile app
.

Sent using OPPO Mobile Phone
 
Sasa wote wamekosa, wanafunzi waja wazito wachache na wengi wasio wajawazito, nani kafaidika?
hakuna aliyekosa "sisi" tunauwezo mkubwa ndio maana tunatoa elimu bure kuanzia darasa chekechea hadi sekondari.
"walevi" ndio wanaongeaga hivi,
 
View attachment 1342451

Kwanza niseme wazi kuwa hapa sizungumzii maudhui ya barua ya Zito Z. Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT-Wazalendo) kwa Benki ya Dunia kuhusu mkopo wa elimu wa benki hiyo kwa nchi yetu pendwa ya Tanzania.

Hapa nazungumza kwa kuuliza kwanini Zito atumie nembo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuandika barua yake binafsi kwa Benki ya Dunia. Katika barua hiyo(ambayo hata humu JF iliwekwa), Zito ametumia 'headed paper' ya Bunge ingawa barua ina maneno binafsi.

Kutumia nembo ya ofisi ni kutaka kuaminisha kuwa mwandishi anasema kwa niaba ya ofisi husika. Ni kuaminisha kuwa Bunge linaijua barua yake na hoja zake. Ni kuaminisha kuwa Bunge linayatamka yaliyo kwenye barua husika.

Kwangu mimi, kutumia nembo ya Bunge ni kulialika Bunge kwenye suala linalohusika na barua hiyo ya Zito. Ni kulipa Bunge uhalali wa 'kumshughulikia' Zito kadiri ya Katiba, Sheria, Kanuni, Miongozo na Mazoea yanayoliongoza Bunge hilo.

Asije akalia na kusaka huruma ya wananchi!
Zitto Zuberi Kabwe ameona kusua sua na kuyumba kwa CDM sasa kaamua kukuza harakati zake ili aje kuwa kinara wa upinzani pamoja na chama chake hapa TZ.

#Time will Tell
 
Hizi kelele za waloshika mimba kuzuiwa shule zimevaliwa njuga kwa hisia sana. Sio kwamba watu wana huruma na hao wasichana bali wamepata ka nguzo kakung'an'g'ania baada ya kubanwa wasiseme.
Kama hili jambo dogo limekuwa hivi, basi huko tuendako si salama. Vifua vimebeba chuki na maumivu wanatafuta pa kutolea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angetumia kuandika mazuri ya inchi au kuombea mkopo kwa ajili ya watanzania angekuwa amefanya sawa kutumia nembo ya bunge?
Hana mamlaka hayo bado lingekuwa ni kosa kama hakufuata taratibu ndahani labda hujui maana ya matumizi ya karatasi maalumu na matumizi yake.
 
Ole wenu Sasa mumguse zitto kitatokea Kama kilichomkuta makontena! Na hilo block huwa halitakati maisha! Na Kama una hela huko USA baby sahau kuzipata, mmewa beep weeeh mabeberu sasa wameamua kuwapigia! Pia more is coming washa ban visa ya lottery kwa wa tz wote! Other measure are on pipeline, haya tuone Dona kantry tunasemaje! Namsubiri Mzee aliyeokotwa jalalani.
 
Wewe utakua mbumbumbu au Maimuna tu... Huyo rafiki yako kwanza ametumia official seal ya bunge kuwakilisha maslahi yake binafsi na wala sio mambo aliyotumwa na wapiga kura wake maskini wa Kigoma. Pili ame-masquarade kama vile bunge halina tatizo na yeye ku-submit hio position WB akishirikiana na NGO uchwara, ndio maana akina Molel leo wametoa motion ya kumpatia adhabu huyo rafiki yako...
Tatizo lako hasa ni lipi mbunge akitumia letterhead ya bunge?



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom