Kwanini Zitto alitumia nembo ya Bunge kuandika barua binafsi kwa Benki ya Dunia? Kwangu mimi huko ni kuhalalisha 'kushughulikiwa' na Bunge

Ikiwa Zitto ataonekana na hatia kwa kutumia letterhead ya bunge basi nina hakika 100% wabunge wote watatiwa hatiani pia ikiwa hilo ni kosa la kisheria!
 
Utajua tu mchakato utakapoanza,nazi haiwezi shindana na jiwe hata siku moja

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata jiwe haliwezi kushindana na muda, ndiyo maana katika somo la jiografia kuna somo la weathering of rocks.

Zaidi, haya si mashindano ya nani anaweza kushindana na nani, ni uchambuzi wa vitu vyenye tija.

Unaweza kuwa unataka kupata kiungo kizuri cha chakula chenye ladha, halafu nazi ikashindanishwa na jiwe, nazi ikashinda kuwa kiungo bora zaidi ya jiwe.

Muktadha ni kitu cha muhimu. Tusirahisishe mambo kwa meaningless jingoism.
 
Huyu jamaa ni MSHAMBA FULANI TU. Linatafuta kick kwa mambo ya kipuuzi kabisa mitandaoni ili liuze jina wakati wenzake wanauza jina kwa UBORA wa practice zao. Mara nyingi humu anaanzisha mada ambazo uwezo wake haumudu kabisa kuzitawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama mada ipi? Punguza kuropoka. Hapa hatuzungumzii practice ya sheria ambayo wewe hauijui, tunazungumzia siasa.
 
Kuna mahali nimesema kuna sheria imevunjwa? Hebu soma tena
PETURO ESKIA MSELEWA WEWE NI MWANA SHERIA KANJANJA TUU PLUS NGUMBARU... HUNA ELIMU YOYOTE ZAIDI YA USAKA TONGE KWENYE SIASA. NDIO MAANA HUJUI HATA ENGLISH YA KUSEMA PLEASE GIVE ME SOME WATER
 
Vyovyote, angetumia nembo ya act au bunge au binafsi nadhani bado isingekua ndio sababu ya kushinikiza maamuzi ya benk ya Dunia.

Benki imesikiliza hoja na sio karatasi zilizotumika kuandika.

Kuna wanaharakati pia walienda na wengine waliandika barua, je mmeona barua zao na karatasi zilizotumika?

Hoja ni kua kuwanyima haki ya elimu watoto kisa tu wamepata mimba ni hoja ya hovyo sana. Elimu ni jambo la msingi la binadamu kama vile kuishi.

Huwezi kumnyima mtu haki ya kupata elimu kisa amepata mimba, hii ni hoja ya kivuta bangi.
acha kupotosha wewe.mtoto hajanyimwa haki ya kusoma.atasoma QIT na ataruhusiwa kufanya mtihani wa taifa.hivi kweli tukiacha ushabiki wa kijinga unataka kuhalalisha kuwa mtoto wa kike akipata mimba basi aende nyumbani akazae then akimwachisha mtoto ziwa arudi shule ile ile?common guys.ndiyo maana wazungu wanatuita nyani maana hatufikirii kama wanadamu wakaida.ebu kabla hamjashabikia upumbavu huu fanyeni utafiti huko kwa wazungu rate ya mimba za utotoni ikoje na compare na uchumi wa mataifa hayo na uchumi wetu.wao ni industrialized countries sisi ni developing poor countries.walifika katika hali ya kuwa industrialized country baada ya kuwa na wasomi wengi mno.acheni kutumia makalio kufikiri .i hate this
 
Kikatiba nafasi ya kuwa Mbunge ni Uwakilishi wa Wananchi katika Maeneo yake ,uwakilishi ni pamoja na yeye kama Mwananchi.Tatizo lipo wapi hapo !?
Hapa kuna mjadala kati ya watu wa aina mbili.

Watu wenye mtazamo wa kizamani, mtazamo wa Kikomunisti ulioshindwa na kuanguka Soviet Union.

Mtazamo unaosema kwamba Mbunge haruhusiwi kutumia letterhead ya bunge mpaka aombe idhini kwa maandishi ya barua ya triplicate nakala kwa katibu wa Bunge, Spika na Waziri Mkuu.

Yani mfumo huu utakutaka kuandika barua kuomba ruhusa ya kuandika barua.

Huu ni mfumo wa kizamani, una ukiritimba, unaondoa maana ya uhuru wa mbunge, unamfanya mbunge kama mtoto.

Wengine tunahoji ujinga huo.

Tunasema, mbunge mpaka kuchaguliwa na wananchi ni mtu aliyekubalika.

Kuanza kumpangia habari za kuomba ruhusa ya kuandika barua ili kutumia letterhead ya bunge, wakati anafanya shughuli za uwakilishi wa watu kama mbunge, ni kumnyanyapaa, ni kuwatukana wale waliomchagua kwamba wamemchagua mtoto anayehitaji idhini hata kuandika barua, ni kuendekeza ukiritimba na dhana ya "police state", ni kumnyima mbunge uhuru wake wa kikatiba kama mwananchi na zaidi uhuru pekee wa kibunge.

Kweli mpaka leo kuna watu wanataka tuongozwe kwa ukiritimba wa Kisoviet Union ambao wao wenyewe wa Soviet waliangushwa nao wakaamua kuuacha?
 
Hivi Zito ananguvu hivyo kumzidi hata waziri wa fedha yaani ombi la Zitto limeshughulikiwa na world Bank kuliko ombi la waziri au serikali

mwanabhonga
 
mnaopotosha kuhusu wasichana waliotiwa mimba someni hii

PROGRAMU ELIMU YA SEKONDARI NJE YA MFUMO RASMI KWA NJIA YA MAFUNZO YA JIONI MKOMBOZI KWA WALIOKOSA ELIMU YA SEKONDARI
 
Kuna mahali nimesema kuna sheria imevunjwa? Hebu soma tena
Hujasema hivyo ila kwa kuwa wewe ni mtalaamu wa sheria alitaka pia uliangalie suala hili kisheria.

Kwa mfano mtu akikutwa kavaa sare za jeshi wakati yeye si mwanajeshi atakuwa kavunja sheria. Au mtu aka 'impersonate' kuwa fulani (eg TISS) wakati si kweli atakuwa kavunja sheria.

Zitto katumia headed paper za bunge la JMT ili alichokiandika humo kionekane kuwa kimetoka kwenye bunge la JMT wakati si kweli, atakuwa kweli hajavunja sheria fulani ya nchi inayofanana na mifano hiyo niliyoitaja? Si jinai kubwa kweli?.
Hebu basi jaribu kudadavua suala hili kisheria zaidi.

Au mtu yo yote anaweza kutumia headed paper hizo za bunge au za taasisi nyingine nyingine ye yote na akawa hajavunja sheria? Kama ni kweli mtu ye yote au mbunge ye yote anaruhusiwa kutumia headed paper hizo za bunge kwa mtindo huo basi tutegemee barua nyingi za namna hiyo kutoka kwa wabunge wetu. Heshima ya bunge letu hatapotea? Tunavyojua kwenye tasisi ye yote any official corespondent inayotumia nembo ya tasisi hiyo hufanywa kwa niaba ya mkuu wa tasisi husika na tasisi ya bunge la JMT mkuu wake ni spika wa bunge. Kwa hili Zitto Kabwe alilolifanya hakuna kitakacho mu exonerate from conviction of a criminal offence. Ngoja tusubiri tuone. Tayari AG analifanyia kazi suala hili.
 
Kuna mahali nimesema kuna sheria imevunjwa? Hebu soma tena
Impliedly...ndio. Mh. Mselewa angalia paragraph yako ya mwisho halafu zingatia hitimisho lako. Impliedly unalenga kuaminisha wasomaji kuwa Zitto amekiuka sheria fulani, ama kifungu fulani cha katiba , ama muongozo fulani ama mazoea fulani. Ndio maana umemhukumu impliedly kwenye mstari wako wa hitimisho. Hivyo usikatae. Ingelitosha ungebakia objective kwa kuuliza swali lako kama ulivyoanza pasipo kuingiza kwenye hitimisho lako kuhusu kumuonea huruma ...ama sijui...asijetafuta huruma za wananchi. What if..kwa kutumia headed paper hajakosea kisheria ama kikatiba ama kimuongozo wowote????
 
Back
Top Bottom