Kwanini Zitto alitumia nembo ya Bunge kuandika barua binafsi kwa Benki ya Dunia? Kwangu mimi huko ni kuhalalisha 'kushughulikiwa' na Bunge

Kwahiyo kama unakiri hakuna sheria iliyovunjwa,unadhani Ndugai na CCM wenzake watamshugulikia kwa sheria ipi wakati hata wewe mwandishi unakiri hakuna sheria iliyovunjwa?

Kwahiyo unakiri ni mwendelezo wa vitisho na kelele zenye lengo la kuwanyamanzisha wanaounga mkono maoni ya Zitto

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapi nilipokiri kuwa hakuna sheria iliyovunjwa?
 
Zitto ni mbunge na bunge ni ofisini kwake unless kama sheria za bunge zinakataza wabunge wasitumie nembo yake kitu ambacho hakipo maana hata gari zao wanapeperusha bendera ya bunge lenye nembo.

Kwa kifupi anayo haki kutumia nembo ya bunge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu mwisho wao kuona mambo unaishia keshokutwa. Watu makini huyaona mambo hata mbele ya miaka 50.

Mataifa yote (simaanishi vinchi - kwa lugha ya Mwalimu Nyerere) yanajua kila kitu kinachoendelea Tanzania. Mataifa haya hayahitaji kuambiwa na Zito au wanaharakati ili kuyajua yanayoendelea hapa kwetu.

Maamuzi yalikwishafikiwa juu ya ombi la mkopo wetu WB.

Lakini pia, maamuzi yamefanyika kuhusu uvurugwaji wa aina yoyote ile utakaojitokeza kwenye uchaguzi mkuu 2020.

Wanachokihitaji ni ule uhalali tu wa kuchukua hatua. Hakimu anaweza kumwona mtu anaiba, anaweza kujua kuwa mtu fulani anadhulumiwa lakini hawezi kuchukua hatua za kumfunga au kumpiga faini mhalifu bila ya kuwepo anayelalamika.

Zito na wanaharakati wamehalalisha tu maamuzi yaliyofikiwa. Sasa wanasubiriwa wengine wahalalishe hatua za kuchukua baada ya uchaguzi wa 2020. Ndiyo maana niliwahi kusema kuwa kosa dogo kwenye uchaguzi wa 2020, sote tutajutia.

Tusimwangalie Zito wala wanaharakati, bali kama Taifa tuangalie zaidi makosa tuliyoyafanya. Kumbukeni kuwa, siku zote, madhara makubwa, kwanza hutanguliwa na madhara madogo ambayo huwa yanapuuzwa. Hili la sasa ni dogo sana. Kwa bahati mbaya tunataka kulishughulikia kwa kuharibu zaidi badala ya kurekebisha.

Mwenye kupuuza afanye hivyo na mwenye kuzingatia, ajaliwe zaidi hekima.
 
Kuna mahali nimesema kuna sheria imevunjwa? Hebu soma tena
Unajichanganya sana!
kwenye andiko lako umehoji kama sheria imevunjwa....
lkn kwenye hitimisho lako umesha conclude uhalali wa Bunge kumshunghulikia Zito ....
bila kwenda zaidi kuonyesha kanuni na sheria
zilizokuwa offended....????
next time try to be brief and precisely....
otherwise unapoteza point nyingi sana....
 
HAO NDIO WANASHERIA WETU , HATA KAMA UNA KESI YA KUSINGIZIWA KUIBA KUKU JITETEE MWENYEWE
 
Naamini wewe ni mwanasheria ila unanishangaza sana unapokuwa unaandika kama mtu aliyesoma Political Science.

Kabla ya kuongea au kaundika fanya utafiti kwanza halafu uje na legal issues kwa kuonesha wapi sheria imevunjwa na legal implication yake ni nini.

Ahsante sana.
Nimeshakquestion mara nyingi kuhusu huyu mwanasheria wetu .... something clearly does not add up!!
 
Kwanza niseme wazi kuwa hapa sizungumzii maudhui ya barua ya Zito Z. Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT-Wazalendo) kwa Benki ya Dunia kuhusu mkopo wa elimu wa benki hiyo kwa nchi yetu pendwa ya Tanzania.

Hapa nazungumza kwa kuuliza kwanini Zito atumie nembo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuandika barua yake binafsi kwa Benki ya Dunia. Katika barua hiyo(ambayo hata humu JF iliwekwa), Zito ametumia 'headed paper' ya Bunge ingawa barua ina maneno binafsi.

Kutumia nembo ya ofisi ni kutaka kuaminisha kuwa mwandishi anasema kwa niaba ya ofisi husika. Ni kuaminisha kuwa Bunge linaijua barua yake na hoja zake. Ni kuaminisha kuwa Bunge linayatamka yaliyo kwenye barua husika.

Kwangu mimi, kutumia nembo ya Bunge ni kulialika Bunge kwenye suala linalohusika na barua hiyo ya Zito. Ni kulipa Bunge uhalali wa 'kumshughulikia' Zito kadiri ya Katiba, Sheria, Kanuni, Miongozo na Mazoea yanayoliongoza Bunge hilo.

Asije akalia na kusaka huruma ya wananchi!
kumtaja Zitto kama "Zito" haina tofauti na Zitto kutumia nembo ya bunge.

wanaojua hesabu wamenielewa!
 
Atleaat angekuja na quotation ya sheria gani zimevunjwa ili kuitia uzito hoja yake. Hapa ndipo wanasheria wa tz wanafeli
Naamini wewe ni mwanasheria ila unanishangaza sana unapokuwa unaandika kama mtu aliyesoma Political Science.

Kabla ya kuongea au kaundika fanya utafiti kwanza halafu uje na legal issues kwa kuonesha wapi sheria imevunjwa na legal implication yake ni nini.

Ahsante sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom