Kwanini zile karatasi za vipimo vya mgonjwa zahanati binafsi huwa hairuhusiwi kuondoka nazo? Ni utaratibu sahihi wa tiba au ni uhuni?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Moja ya haki ya mgonjwa ni kupewa taarifa za ugonjwa na kuzitafakali kwa makini!

Swali; Kwanini vipimo na maelezo yanayoandikwa kwenye karatasi ya mgonjwa katika zahanati binafsi huwa vinazuiwa kuondoka navyo mgonjwa? Je, ni utaratibu wa kitabibu au ni uhuni?

Wajuvi tujuzeni!
 
Swali; Kwanini vipimo na maelezo yanayoandikwa kwenye karatasi ya mgonjwa katika zahanati binafsi huwa vinazuiwa kuondoka navyo mgonjwa? Je ni utaratibu wa kitabibu au ni uhuni?

Wajuvi tujuzeni!

Nenda pale Muhimbili ukaombe kuondoka na file lako nyumbani.

File kubaki hispitali ni record management ili ukirudi next time ijulikane ulifanyiwa vipimo gani na kuandikiwa dawa gani, je tatizo la sasa linamahusiano na lile la mwanzo au ni tafauti? Kama unazihitaji sana piga photocopy au picha kwa siku yako.
 
Kwani hospitali za serikali unaruhusiwa kuondoka nazo?

Wengi mnapotoshwa na mawazo kuwa 'unazuiliwa' ili ununue dawa hapo hapo.

La hasha!
Kinachoandikwa pale sio dawa pekee, ni pamoja na taarifa za mgonjwa. Una haki ya kupewa taarifa, lakini huwezi kusoma mwenyewe ukaelewa.

Kama unahitaji omba utapatiwa, lakini hawawezi kuziachia wazi kwa kila mtu kwa maana haijulikani nani ni nani.

Hii ni kwa usalama/usiri wa taarifa zako.
 
Oooh kwahiyo ni siri yao siyo siri ya mgonjwa mwenyeww
 
Ni siri ya mgonjwa, wenye kuhitaji huwa wanafahamishwa... kumbuka walio wengi ni wapumbavu mno kiasi kwamba hata hawajui kila kitu kuwahusu.

Cheti kinaandikwa kwa codes za kitaalamu, raia hawezi kuelewa na hivyo hawezi kutunza cheti hicho... kikiangukia mikononi mwa watu wabaya wanaojua kutafsiri sio poa.

Jengeni tabia ya kuamini wataalamu wetu, worst comes to worst... hofu ya kupigwa sijui pesa hasara yake ni kubwa kuliko faida.
 
Ni hasara zipi kwa mfano doctor
 
Mi uwa napiga picha.

Ni kosa kubwa ufanyalo, unapiga picha na kutangazia watu taarifa zako... fikiria una gonjwa la aibu na limeandikwa hapo!

Hujui kilichoandikwa unapiga picha tu na kusambazia watu, ujinga ni mzigo sana.
 
Moja ya haki ya mgonjwa ni kupewa taarifa za ugonjwa na kuzitafakali kwa makini!

Swali; Kwanini vipimo na maelezo yanayoandikwa kwenye karatasi ya mgonjwa katika zahanati binafsi huwa vinazuiwa kuondoka navyo mgonjwa? Je, ni utaratibu wa kitabibu au ni uhuni?

Wajuvi tujuzeni!
Hakuna mgonjwa anaeruhusiwa kuondoka na file la matibabu
Iyo ni sheria
 
Ni hasara zipi kwa mfano doctor

Taarifa zako ni siri kati yako na mtaalamu wa afya aliyekuhudumia kwa mujibu wa kiapo, au na mtu mwingine ambaye utaridhia wewe ajue siri yako.

Ukipewa cheti uende nacho nyumbani, kama hujui hata kilichoandikwa haitakusaidia kitu... matokeo yake kitawafikia watu wengine na kuuza siri zako.

Fikiria hasara ya kujulikana maradhi yako kwa watu usioridhia, linganisha na hiyo buku tano unayohisi unalazimishwa kununua dawa hapo hapo.
 
Moja ya haki ya mgonjwa ni kupewa taarifa za ugonjwa na kuzitafakali kwa makini!

Swali; Kwanini vipimo na maelezo yanayoandikwa kwenye karatasi ya mgonjwa katika zahanati binafsi huwa vinazuiwa kuondoka navyo mgonjwa? Je, ni utaratibu wa kitabibu au ni uhuni?

Wajuvi tujuzeni!
draw match we unaondoka na Dawa na ugonjwa wako wao wanabaki na file na daktari wao sasa shida iko wapi?
 
Moja ya haki ya mgonjwa ni kupewa taarifa za ugonjwa na kuzitafakali kwa makini!

Swali; Kwanini vipimo na maelezo yanayoandikwa kwenye karatasi ya mgonjwa katika zahanati binafsi huwa vinazuiwa kuondoka navyo mgonjwa? Je, ni utaratibu wa kitabibu au ni uhuni?

Wajuvi tujuzeni!
ni mazingira ya kutunza taarifa za mgonjwa lakini pia ni sehemu ya marketing kwa kuwa mara nyingi wagonjwa hupenda kwenye hospitali waliotibiwa kwanza kwa kuamini wa histori za changamoto zao kiafya .
hivyo sio jambo baya usihofu.
 
Nenda pale Muhimbili ukaombe kuondoka na file lako nyumbani.

File kubaki hispitali ni record management ili ukirudi next time ijulikane ulifanyiwa vipimo gani na kuandikiwa dawa gani, je tatizo la sasa linamahusiano na lile la mwanzo au ni tafauti? Kama unazihitaji sana piga photocopy au picha kwa siku yako.
Anazungumzia karatasi iliyoandikwa dawa siyo file.
 
Kwani hospitali za serikali unaruhusiwa kuondoka nazo?

Wengi mnapotoshwa na mawazo kuwa 'unazuiliwa' ili ununue dawa hapo hapo.

La hasha!
Kinachoandikwa pale sio dawa pekee, ni pamoja na taarifa za mgonjwa. Una haki ya kupewa taarifa, lakini huwezi kusoma mwenyewe ukaelewa.

Kama unahitaji omba utapatiwa, lakini hawawezi kuziachia wazi kwa kila mtu kwa maana haijulikani nani ni nani.

Hii ni kwa usalama/usiri wa taarifa zako.
Ni uhuni tu huwa unafanyika. Hospitali wanatakiwq kuandika dawa walizotoa kwenye file na wewe ile karatasi ya dawa uende nayo. Na ile karatasi inakuwa na copy yake ya njano kww chini. Ukipewa dawa, unaacha ile ya njano na original unaenda nayo.

Dispensary wanakataa kutoa vyeti ili ununue dawa kwao na hii ishu inabidi kukemewa.
 
Unazoita dispensary pengine ni za magumashi, umesema lengo ununue dawa zao... au kama ni za serikali pengine ni utaratibu rasmi.

Hiyo unayoita karatasi ni 'prescription', wala sio kwajili yako... inaandikwa dawa na maelekezo ya matumizi.

Ile unaandikiwa ili ukachukue dawa FAMASI, sasa kama dawa umepata unaihitaji ya kazi gani?

Siku hizi mifumo imeboreshwa, hakuna cha karatasi ni electronics unapewa namba tu nenda famasi chukua dawa anza kutumia kwa kuzingatia maelekezo.

Utapewa uende nayo ikiwa tu dawa hazipatikani hapo hospitali, na inategemea na aina ya dawa.
 
Back
Top Bottom