IKARAHANSI
JF-Expert Member
- Jul 30, 2019
- 398
- 479
Wakuu habari ya muda huu, ni matumaini yangu kuwa mpo salama mkiendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa. Kwa wale wenye matatizo ya hapa na pale nawaombea kwa MUNGU awafanyie wepesi ili mfanikiwe kwa usalama. Tuje kwenye hoja.
Tuliopita shuleni enzi hizo na tuliopo sasa, tumefundishwa kupitia hisitoria kuwa kuna vita nyingi sana zilipiganwa baina ya makabila, himaya, falme hadi na nchi moja dhidi ya nyingine yote hiyo ilikuwa ni kugombea maslahi na mipaka ya utawala baina ya himaya moja na nyingine.
Moja wapo ya vita hizo kuna vita kubwa mbili ambazo zilijumuisha mataifa mengi ambazo ziliitwa vita za dunia (Vita ya kwanza ya dunia na vita ya pili ya dunia), vita za dunia zote mbili zilihusisha mataifa makubwa ya ulaya enzi hizo yaani Wajerumani na Waingereza pamoja na makoloni yao wakisaidiwa na baadhi ya mataifa ya America (USA) na Asia (Japan).
Binafsi nilipokuwa shule enzi hizo nilikubaliana kuwa kweli ilikuwa ni vita za dunia, lakini kadri ninapoendelea kukua na kutafakari naona kuwa tulidanganywa hakukuwahi kuwa na vita ya dunia. maana kama ingekuwa vita ya dunia basi mataifa yote yaliyopo Duniani yangeshiriki.
Swali langu ni je, Kwanini ziitwe vita za Dunia wakati nchi kama Brazil, Agentina, Paraguay, Colombia, Peru, Uruguay kwa ujumla America ya kusini hazikushiriki katika vita hizo na wakati zipo Duniani? Ukija kwa upande wa Asia sikuwahi kusikia China, Campodia au Iran zikitajwa katika vita hizo mbili za dunia.
karibuni kwa michango!!!