barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Hii imeendelea kuleta mkanganyiko katika kusimamia sheria na taratibu wanaoziweka na kuamua kuzitekeleza.
Ikiwa imepita siku kadhaa mkutano mkubwa wa Chadema Wilayani Kahama kuzuiliwa na watu kupigwa mabomu,na huko Dsm Kongamano la ndani la Chama cha ACT-Wazalendo kuzuiliwa kwa nguvu kubwa,Huko Iramba Waziri mteule wa Mambo ya Ndani ameendelea kufanya mikutano ya kisiasa na mikusanyiko mikubwa mikubwa yenye lengo la "kuwashukuru" wananchi kwa kumchagua na hatimaye kushinda ubunge.
Haya ya huko Iramba yanatokea huku Jeshi la Polisi likiwa limepiga marufuku mkusanyiko wa kisiasa wa aina yoyote!Na hii imedhihirika baada ya leo kiongozi wa Upinzani Bungeni na viongozi wengine wa chama kushikiliwa kwa muda na polisi.
Jamani hii nchi ya wote,Epukeni "Double Standard" zitakazoleta utengano badala ya umoja!