Kwanini zamani wazazi walikuwa wakitukataza kuongea wakati wa kula?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,272
8,843
Siku hizi Utaratibu huu naona umepotea kabisa au labda umebaki kwa Familia chache sana.

Familia za sasa mkiwa Mezani mnakula ni mwendo wa kupepeta stori mpaka Msosi unaisha.

Kwanini zamani hii ilionekana kuwa tabia mbaya? Nini kimebadilika?
 
mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
9,168
17,056
Kwanza kuongea huku unakula kiafya sio sawa,
--kurusha mate kwenye chakula.
--kupaliwa na chakula wakati unaongea.

Ila siku hizi watoto wanakula huku wanaangalia TV.
Wakati zamani tuliambiwa tukila.tuangalie chini tunapokula.
 
Bangida

JF-Expert Member
Mar 20, 2022
1,319
4,617
Baba yamgu aliniambia, msingi wa tabia kwa mtoto unaanzia mezani. Ukufanikiwa kuhakikisha table manners, ni rahisi mtoto kua na tabia nzuri.

Pamoja na hili nafkiri ilikua kwa ajili ya kutunza siri za familia maana watoto hawana breki, wanaeza sema mabo ya shombo mbele ya kadamnasi.

Na zamani sehem ambapo kulikua na kadamnasi ni mezani coz nje ya hapo watoto hawaruhusiwi kuwepo kwenye maongezi ya watu wazima.
 
Hank_31

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
845
2,041
Kwanza kuongea huku unakula kiafya sio sawa,
--kurusha mate kwenye chakula.
--kupaliwa na chakula wakati unaongea.
Kwa kuongezea hapo pia, kiroho inasaidia sana maana inamfanya mtu ku-concentrate na chakula hivyo ni kama moja ya Energy meditation.
 
Unforgettable

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
4,429
9,642
Kwanza kuongea huku unakula kiafya sio sawa,
--kurusha mate kwenye chakula.
--kupaliwa na chakula wakati unaongea.

Ila siku hizi watoto wanakula huku wanaangalia TV.
Wakati zamani tuliambiwa tukila.tuangalie chini tunapokula.
tena tv inazimwa mnakula kwa pamoja ndomana watu wa zamani upendo upo ila sikuizi watoto wanalia vyumbani tena kwa mda anaotaka huku anachat na kuongea na simu
 
Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,272
8,843
Baba yamgu aliniambia, msingi wa tabia kwa mtoto unaanzia mezani. Ukufanikiwa kuhakikisha table manners, ni rahisi mtoto kua na tabia nzuri.

Pamoja na hili nafkiri ilikua kwa ajili ya kutunza siri za familia maana watoto hawana breki, wanaeza sema mabo ya shombo mbele ya kadamnasi.

Na zamani sehem ambapo kulikua na kadamnasi ni mezani coz nje ya hapo watoto hawaruhusiwi kuwepo kwenye maongezi ya watu wazima.
Hili jambo la Msingi sana. Mtoto anaweza kukuaibisha bila kutarajia na ukakosa hata la kujitetea😂😂😂
 
Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,272
8,843
tena tv inazimwa mnakula kwa pamoja ndomana watu wa zamani upendo upo ila sikuizi watoto wanalia vyumbani tena kwa mda anaotaka huku anachat na kuongea na simu
Hapa unadhani kosa ni la nani? Kwanini Mtoto alie Chakula Chumbani tena kwa wakati wake? Anayeosha Vyombo kila baada ya dk anakuta Sink lina chombo kichafu
 
Mr Gadaffi

JF-Expert Member
Nov 14, 2022
1,214
1,751
Tena mimi nyumbani kwetu muda wa chakula unatandikwa mkeke mkubwa wote mnakaa chini, mze peke yake ndo anakalia kiti , marufuku kuongea hata punje!
 
saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
754
831
Siku hizi Utaratibu huu naona umepotea kabisa au labda umebaki kwa Familia chache sana.

Familia za sasa mkiwa Mezani mnakula ni mwendo wa kupepeta stori mpaka Msosi unaisha.

Kwanini zamani hii ilionekana kuwa tabia mbaya? Nini kimebadilika?
Labda huko kwenu mmeshindwa malezi. Huku kwetu hyo tabia hairuhusiwi
 
chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,528
15,037
siku hizi wazazi wanawakataza watoto kushika simu wakati wanakula
 
Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
96,103
99,883
Umbea wa zamani ni mzito wa siku hizi ni mwepesi sana ndiyo maana...
 
4 Reactions
Reply
Top Bottom