Kwanini zabuni ya kuonesha Ligi Kuu Tanzania Bara haikutangazwa, kapewa Azam moja kwa moja?

Mars 12

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
221
349
TFF na AZAM TV zimeingia mkataba wa kudhamini ligi ya soka Tanzania Bara bila ya kutangaza Tenda na Pia hakuna mikataba mirefu kama huubwa miaka kumi.Huu ni ukiukwaji wa utaratibu wa kuonyesha mechi za mpira wa miguu nchini.

Duniani kote Tenda zinatangazwa na kila kampuni inatoa ofa lakini haipewi kuonyesha mechi zote.Mfano ligi kuu ya Uingereza ofa ni kubwa mno kila timu kubwa na ndogo zinafaidika.

Wapo skysports, Bsports na Amazon. Ligi hii ya premier ya England ina thamani ya paundi za Uingereza Bilioni 6 na mkataba na Barclays bank mnono. Sasa hapa kwetu TFF itaingiaje mkataba wa miaka 10 na kampuni moja? Ama kweli fumbo mfumbie Mjinga,mwerevu hungamua.

WIZARA YA HABARI NA MICHEZO IINGILIE KATI MKATABA HUU KWA SABABU KUU TATU; 1)Tenda itangazwe na makampuni mengi ya utangazaji yatatoa ofa ambazo zitasaidia hata timu ndogo(2) TV moja isepewe asilimia 100 kama ilivyo sasa,zigawanywe kutokana na pesa wanazo ofa(3)Mkataba uwe wa miaka 3 mitatu tu na siyo 10.Kwa wengi na kwa sasa mabillioni wanayaona mengi lakini kwa miaka 10 ni pesa ndogo sana.

Hapa pana mambo ambayo inabidi yaangaliwe.TFF wasitufanye Watanzania wajinga na mbumbumbu. HAKUNA MIKATABA YA KUONYESHA MIPIRA KWA TELEVISION MOJA KWA MIAKA KUMI TENA KWA KIASI KIDOGO CHA PESA. TFF VUNJENI MKATABA NA AZAM TANGAZENI TENDA, TV NYINGI ZITAKUJA NA OFA , TIMU ZOTE ZITAFAIDIKA ZENYE UWEZO NA AMBAZO HAZINA. WIZARA YA HABARI, MICHEZO, BMT AMKENI.
 
Hahaha mkuu, kuna vingene uko sawa ila nakusihi sana kabla ya kuandika uzi hapa jf tafadhali fanya uchuzi hata kidogo. Nitakurekebisha mambo mawili tu afu ukafanye uchunguzi mwenyewe....

1: TFF walitangaza kumalizika kwa mkataba na tenda ilitangazwa kwenye vyombo vya habari ( wewe hukusikia).

2: Mwenye haki ya kuonyesha ligi ya EPL ni sky sports tu, wengine wote wanunua matangazo kutoka kwake.

Vipo vingi vya kukurekebisha ila jaribu kuviangalia mwenyewe.....
 
Ni matakwa ya procurement act

Sheria inataka tenda itangazwe bila ya kujali wapo wangapi nk

Screenshot_20210525-165657_WhatsApp.jpg
 
Hahaha mkuu, kuna vingene uko sawa ila nakusihi sana kabla ya kuandika uzi hapa jf tafadhali fanya uchuzi hata kidogo. Nitakurekebisha mambo mawili tu afu ukafanye uchunguzi mwenyewe....

1: TFF walitangaza kumalizika kwa mkataba na tenda ilitangazwa kwenye vyombo vya habari ( wewe hukusikia).

2: Mwenye haki ya kuonyesha ligi ya EPL ni sky sports tu, wengine wote wanunua matangazo kutoka kwake.

Vipo vingi vya kukurekebisha ila jaribu kuviangalia mwenyewe.....
Mtoa mada kisa hakusikia anahisi havikufanyika.
 
Tender ilitangazwa na kampuni zili bid, wakati wa kufungua technical proposals zao ulifanyika kwa uwazi tena kwenye Tv last month na kipindi kilikuwa live. Ni vyema ungeuliza kuliko kuhitimisha kwa vitu ambavyo huna ufahamu navyo.

Pili, Je tenda hii ya Azam ina faida kwa mpira wetu wa Tz, jibu ni ndio, sponsor mkuu Vodacom anatoa 3bn kwa mwaka saivi wakati Azam yeye ni broadcasting right tu amekubali kutoa 22bn kwa mwaka, kabla Azam alikuwa anatoa 23bn kwa miaka mitano ( 4.5bn kwa mwaka) hivyo kupanda hadi 22bn kwa mwaka ni ongezeko kubwa hata clubs zenyewe hazikutegemea, tujifunze kushukuru.

Je, kwa nini TFF na Bodi ya ligi wamekubali mkataba wa miaka 10 badala ya mkataba mfupi, mazingira ya Tz ni tofauti na nchi zilizoendelea, huku viwanja vyetu camera sio plug and play, kuna uwezekazaji mkubwa inabidi ufanyike ili viwanja vyetu vyote uweze kuona camera kwa angles zote, mtu hawezi kuwekeza pesa nyingi halafu mkataba unaisha kabla hata hajamaliza kurudisha pesa yote.
 
Back
Top Bottom