Kwanini? Why? 4 ladies only | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini? Why? 4 ladies only

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kilema, Dec 2, 2009.

 1. kilema

  kilema Member

  #1
  Dec 2, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hivi kwa nini wanawake wakiolewa katika familia fulani wao ndio chanzo cha kusamatika kwa upendo uliokuwepo katika familia hiyo.

  Kwetu tumezaliwa wanaume wawili na wanawake sita. toka tumekuwa tulikuwa tunapendana sana. Kasheshe ilianza baada ya kaka yangu kuoa. mkewe akawa hatutaki ndugu kabisa? bahati nzuri kaka yangu ndie anayejiweza kiuwezo kwa hiyo tukifika kwake tunaonekana kama vile tumekuja kuomba omba hata kam ni jambo lingine limetufikisha hapo. Hakuna ugomvi wala nini na mama huyu lakini anatengeneza bifu juu yetu kiasi cha kumfanya kaka asiwe tena karibu na sisi.Huyu mama mwenyewe kwao masikini hohe hahe.Hamjui dunia duara kesho ikiwa vinginevyo uso utauweka wapi?
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  huyo mke wa kakaako ana matatizo yake ya asili na si wanawake wote kama ulivyosema
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Dec 2, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni tabia ya mwanamke binafsi na sio wanawake wote wakiolewa inakuwa hivyo. Kuna wengine wakiolewa na upendo ndio unaongezeka katika familia na ukoo kwa ujumla.
  By the way ningeshauri hii post iende kwenye jukwaa la mahusiano pale kuna wazoefu wa mambo haya, na wanaweza wakakosa muda wa kupita jukwaa hili, ndugu yetu akakosa ushauri mzuri.
   
 4. w

  wakumbuli Senior Member

  #4
  Dec 2, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwani lazima kwenda hme kwa bro au namind na menu,kaonane naye ofisini
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahaha swalo lako la kizushi sana wakumbuli
   
 6. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Halafu utakuta mwanamke mwenyewe amepatikana kwa bro kupitia mimi yaani kaka alikuwa ananituma kupeleka vibarua au kumwita kwa ajili ya mapenzi yao baada ya bro kukolea na kutia ndani kimwana basi limwanamke linakuana kenge kinyesi mkubwa
   
 7. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kwanini uonane ofisini na kaka yako ?kisa shemeji yako, wakati yeye shemeji wakuja, mke unaweza kuachana nae lakini ndugu ama wazazi huwezi kuachana nao milele yote na katika maisha yote. elewa damu zito kuliko maji
   
 8. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,767
  Trophy Points: 280
  Uachane na mkeo ukazae na nduguyo..??? Cha msingi ni kukaa na kaka na kumweleza ukweli ili kama vipi akaseme na mkewe. Kukutana ofisi na kaka yenu siyo busara, san sana huyo mke akigundua basi itaongeza uhasama..
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280

  lakini wanawake wana sumu kali sana.
  Wanawake (mawifi) ndio wanaovunja ndoa pamoja na mama mkwe.
  Mashemeji na baba mkwe wala hawana tym ya kuingilia mahusiano ya mtu.
   
 10. kilema

  kilema Member

  #10
  Dec 2, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Inaonyesha tatizo hili liko kwa wengi. Mbona walengwa hawasemi
   
 11. _ BABA _

  _ BABA _ JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2009
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...hahaha mkuu hapo nimepakubali yani kusema amesahau kabisa fadhila za kipindi cha mawindo.....lol....
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hahaaa mkuu na experience the same thing yaani we acha tuu, sie tupo wa 5 wawili wa kike wa 3 wa kiume mmoja alifariki, tumebaki wa kiume 2 tu wa kike wameolewa tayari huyo bro wetu wa kwanza sasa hivi ni mbogo, kwake ukienda km umekwenda ugenini, yule shemeji yetu ana wadogo zake wanne wanamtegemea bro pale, watatu wa kiume wawili wa kike, ila wa kike mmoja kaolewa so anajitegemea, hawa watatu wa kiume na huyo mmoja wa kike ndo wapo pale.Juzi wifi yetu kaenda morogoro semina kakaa wiki tatu hata kuwapiia wifi zake wapo pale Morogoro, walipokutana naye kwa bahati mbaya tu akadai eti amesahau kwa ma wifi zake so kwenda mpaka kaka yetu ampeleke. mkuu hii kitu nimeiona sehemu nyingi sana tuuu
   
 13. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Kweli Mkuu umenena sawia. You can choose friends/wife/husband but not relatives.
   
 14. M

  Matarese JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  You are very right Chimunguru, baadhi (inawezekana kabisa idadi ikawa inaongezeka kwa sasa)ya wanawake wakishaolewa wanajaribu sana kuhakikisha mume na ndugu zake hawapo pamoja, yaani yeye ataleta sababu yoyote ile na kufanya chochote kile ili mradi ndugu wa mume wakikanyage hapo nyumbani. Kibaya zaidi, wengine wanafikia hata kuwakosanisha mume na ndugu zake. Naona tatizo kubwa ni UBINAFSI ULIOKITHIRI! Hivyo ni wajibu wa mume kutumia akili na busara ili kuzuia hili.
   
 15. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #15
  Dec 2, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hivi FL1, hujangundua kama huyu jamaa anayeanzisha hizi thread ana matatizo? Especially na shemeji zake. soma thread zake zote aloanzisha leo then tafakari. kwa ufupi nilivyomtathmini naona ana bifu na wanawake kama sio mashemeji zake, soma maneno fulani anayoyatumia kwenye thread zake zote, (mke wa kaka yake katoka familia maskini), so what? kwani kutoka familia maskini ni dhambi? Kwenye thread ingine kasema kaka yake kwa sasa kafukuzwa kazi mkewe anamnyanyasa, jamaa hadi kaamua kufundisha sunday school, sasa huku anasema kaka yake ana uwezo . I dont get it. Grow up man na ujue kaka yako kaoa, ana familia yake, give them space, na wewe tafuta vyako, tafuta familia yako. who knows may be yako itakuwa mbaya kushinda yake.
  Halafu usidharau watu kisa wametoka familia maskini, unaweza toka familia maskini ukawa tajiri na ulietoka familia ya kitajiri ukaishia kuwa maskini. so i would advice uondoe huo msamiati kwenye sentensi zako, you never know what tommorow holds.
   
 16. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Hichi kitu kweli kipo kwa baadhi yetu sisi wanawake, ila na nyie ndugu wa kiumeni mnakuwa mnazidisha. Utakuta mtaka kwenda kujazana kwa ndugu yenu hadi kero, mama wa watu anashindwa hata kupanga bajeti............nafuu basi muende tu kusalimia na kuondoka. Sasa nyie mnataka kujenga kibanda kabisa kwa ndugu yenu.
  Maisha yenyewe ya sasa kila mtu anaangalia familia yake, hatukatai kwenda kusalimia ni jambo zuri lakini msipende kukaaa hapo hapo hadi umfanye mwanamke wa watu kuona kero.
   
Loading...