Kwanini wazungu wana historia na sisi Waafrika hatuna?

Wakorea wana historia yao toka mwanzo wataifa lao kuwepo kipindi cha devine Jumong, wazungu hivyo hivyo wana story zao, mbona sisi waafrika hatuna hadithi zetu za mwanzo, au baada wa wazungu kututawala walichukua hadithi zetu? au wazee wetu hawakuwa na sehemu ya kuweka kumbukumbu?

sisi hadithi tulizonazo ni kutawaliwa tu hapo wazungu kuna mambo wameyaficha, pindi tukijuwa historia yetu tutafanya revolution tutawala dunia

story zao mungu mweupe shetani mweusi, hatuna historia tupo tupo tu kama mtoto yatima, wametuletea magonjwa kibao ila bado tunadunda, sisi endapo tukijua Historia zetu tuta fanya mapinduzi
Hatukuwa na uwezo wa kuandika ,yaani hakuna maandishi yaliyobuniwa Africa,tulikuwa na mtindo wa kutunza historia vichwani na kusimulia Kwa mdomo,
Mzee wa story akifa basi inakuwa imeisha

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Historia yetu inatuaminisha sisi tulikuwa sokwe,ndio maana hata kipindi hiki kuna waafrika bado wanaishi porini
Kama tulikuwa Sokwe basi na wazungu, waarabu, wahindi wote sisi sote ni jamii ya sokwe.

Kisayansi binadamu wa kwanza alitoka Africa specifically Ngorongoro. Kadiri alivyotawanyika na miaka ikaenda na mazingira yakabadilika, hao sokwe wakapata evolution wakawa wanachukua sura mpya.

Kama kuumba kidini Mungu alimuumba Adam na Hawa na walikuwa Eden. Eden ipo Iraq hivyo binadamu wa kwanza tuseme ni muIraq basi. Ibrahim alisafiri toka Ur kuja nchi ya ahadi, alifikia Byblos na uchunguzi wa kisayansi na vitu halisi vinaonyesha wa Cannan walifikia pale. Ni historia ndefu ila unaweza ku Google Byblos and its history.
 
Labda wivu ambao hauna msingi, mtu anakufa na ujuzi wake, mf. Anaejua jani fulani lina dawa ya kuzuia wachawi, hataki kurithisha kwa kizazi chake, anakufa na siri yake. Kuna mambo mengi mababu zetu hawakupenda kuweka wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila wenzetu wako vizuri aseee angalia tu hii Royal family kwa kina Elizabeth watu wanaweza kutrace walitunza kumbukumbu mpaka Queen huwa wanasema ni Saxon japo hili kabila lilishapotea , Angalia mfalme wa Norway family tree yake wanayo mpaka kwa mfalme wa kwanza wa Norway Harlad Finehair , Pia kwao mtu maarufu au mtu mwenye mchango kwa taifa tangu kitambo hicho akifariki wanahakikisha hata anapozikwa kila mtu ataona au atajua imagine watu bado wana kaburi la Rais wa kwanza wa Marekan Mzee Washington , hivyo hivyo kwa wanasayansi wao ,

Pia kinachofanya historia zao zinafana watu wanafanya utafiti , Michezo ya runinga inatengenezwa , pia nahisi sisi kitu kilichotupa shida ni kutojua kusoma na kuandika labda !! Pia wale wafalme au viongozi wa zamani kwa upande wa Asia na Ulaya yaani mtu akitawala anataka asifiwe vizazi hadi vizazi kwamba alifanya kitu ! Watu watatunga mashairi , kulikua na watu maalum kabisa kwenye kasri kwa ajili ya kuandika watu watapaint picha na akizingua mfano kwenye vita akili yake kubwa na aibu anawaza kwa kizazi kitakachokuja watanisemaje kwamba nilikua mfalme mwoga !!
Haya yote yamefanya wawe na mkusanyiko mzuri wa historia japo kuna mahala una mapungufu ila wana kitu cha kusimulia !

Historia yetu inakufa kwa sababu naona hatuna utamaduni wa kupenda vya kwetu huenda tulisahaulishwa kutokana na shida tulizo nazo vizazi vya mwanzo vikaona hakuna umuhimu wa kutunza historia !
 
Back
Top Bottom