Kwanini wazungu wana historia na sisi Waafrika hatuna?

APPROXIMATELY

JF-Expert Member
Aug 10, 2021
2,035
2,682
Wakorea wana historia yao toka mwanzo wataifa lao kuwepo kipindi cha devine Jumong, wazungu hivyo hivyo wana story zao, mbona sisi Waafrika hatuna hadithi zetu za mwanzo, au baada wa wazungu kututawala walichukua hadithi zetu? au wazee wetu hawakuwa na sehemu ya kuweka kumbukumbu?

Sisi hadithi tulizonazo ni kutawaliwa tu hapo wazungu kuna mambo wameyaficha, pindi tukijuwa historia yetu tutafanya revolution tutawala dunia

Story zao Mungu mweupe shetani mweusi, hatuna historia tupo tupo tu kama mtoto yatima, wametuletea magonjwa kibao ila bado tunadunda, sisi endapo tukijua Historia zetu tuta fanya mapinduzi.
 
... unlike jamii za Ulaya na Far & Middle East ambao wamekuwa na permanent settlements for centuries, jamii nyingi za kiafrika zimekuwa zikihamahama until the recent past ndio angalau zime-settle permanently. Katika mazingira ya kuhamahama ni vigumu sana kutunza historia!

Kwa mfano, Roma ilijengwa mwaka 740 K.K. means the Romans by then (2761 years ago) walishakuwa na permanent settlements wakati leo hii Afrika bado kuna jamii zinahamahama maporini huko! Hivi maporini unatunza wapi historia?
 
Iraq ina historia kuanzia 5000 BC na hata huyo mzee Ibrahim alitokea huko Ur kwenye bonde kati ya Tigris na Euprates. Je huyu alikuwa ni mzungu. Waliweza kuandika na kuchonga na kuumba vitu ambavyo mpaka sasa vipo.

Sisi ukikuta chombo alichotumia babu mzaa babu yako unakichoma na ndo maana hatuna historia. Miti iliyotumika kuabudia na kutolea sadaka ilishakatwa na hakuna kumbukumbu ya wapi tuliabudu.

Angalia magofu yaliyopo Kilwa baada ya miaka 100 yawezekana hayatakuwepo na tutasema tulitawaliwa na wazungu wakati mwarabu kaingia hapa kalne ya 10.

Hadithi za mapokeo tulizokuwa tunasimuliwa na wazee wakati wa jioni tukikoka moto au wakati wa mvua, siku hizi hakuna sababu wazazi wapo bize na smati foni.

Waafrika hatukuwa na maandishi ila michoro. Waafrika ambao walikuwa na maandishi ni wahabeshi, wamisri ingawa wao walitumia michoro zaidi ya herufi. Sisi ilikuwa ni michoro ambayo hatukuweza kurithishwa hivyo haikuwekwa kwenye mapokeo.
Anza wewe, tulia na wanao kila jioni uwasimulie hadithi ulizorithishwa na wazazi wako au hata hekaya za Abunuasi.
 
Mtumwa hana historia. Usemi huu unaakisiwa kwa namna nyingi.

Nitaanza na utambulisho wa mtu katika jamii yake.

Huwezi kwenda mfano Ujerumani ukakuta mtu asiye Mmakonde akawa na jina la Chakumwenda Chipumbu. Utakuta wajerumani wana majina yao asilia. Cha ajabu ukienda Songea utakutana na Mgoni anaitwa Otto Reinhardt.

Twende visiwa vya Karibian huko Jaimaica. Utakutana na kina Campbell kibao ilhali wao ni weusi titii hawana jina la Mandingo. Ukiwachunguza utabaini kina Campbell wa Jamaica walikuwa watumwa wa bwana Campbell mscotishi yaliyekuwa na mashamba makubwa ya miwa kisiwani Jamaica. Na kila aliponunua watumwa aliwapa jina la ubini la Campbell kwa lazima ili watambulike ni mali ya bwana mkubwa Campbell.

Sisi huku Afrika ambao tulibahatika babu zetu kutokamatwa na kupeleka utumwani, tumekubali kupoteza majina yetu ya kama Chibiriti, Chingolo au Malecela n.k kujitambulisha koo zetu na sehemu zetu za asili bila kucharazwa bakora wala kuwa chini ya utumwa.

Tumekubali kupoteza asili, majina ya ukoo, simulizi za mdomo, majina ya mashujaa, majina ya watabiri wa jadi, tiba-asilia, elimu jadi ya utunzaji ardhi/ kilimo/ mifugo / misitu /uvuvi, dini za asili , tamaduni, stadi za kuishi ktk mazingira yetu n.k kwa kuaminishwa kuwa lazima tuingie katika dini za kuja kwa majahazi na merikebu toka mbali.

Inasikitisha leo hii hatujui majina ya wahenga wetu, miti tuliyokuwa tunakwenda kuweka kafara zetu za jadi, Mahoka, Masika Zolelanga, Mulungu n.k Tunakaririsha Miungu na Mitume ya mbali na kwetu iliyotumika katika mazingira na historia tofauti na ya mababu zetu.

Sifa moja ya mtumwa ni kukosa historia ya asili yake katika kila hali, huku tukidanganyana kuwa mkataa kwao ni mtumwa wakati kiukweli sisi sote tumeshakataa 'kwetu' ingawa tunadanganyana kuwa tuna kwetu na huwa tunajitahidi kukutembelea kila tunapoweza vijijini, wilayani na mikoa tunayotoka.
 
Historia zipo wakuu sema hamjaamua kufuatilia kumbuka civilization ilianza Afrika huko Misri kuna jamii iliitwa kemit hawa walikuwa watu weusi kabla ya Misri hii yenye mchanganyiko wa asili, kuna tawala kama axuminte huko Ethiopia, Nubians ambao walijenga piramids kabla ya Misri, huko Afrika Magharibi kulikuwa na tawala kubwa tu kama Mali, Songhai, Ghana n.k.

Afrika kusini mwa sahara kulikuwa na tawala za Shona, Zulu, Ndebele n.k. Watu kama kina Mansa-kankan Musa ambaye anasemekana ni binadamu tajiri zaidi kuwahi kutokea duniani enzi hizo hata tawala za wazungu hazijazaliwa, fuatilia safari yake ya kwenda hija Macca.

Kuna vitabu vimeandikwa kuhusu ancient africa. Kuna maandiko mengi tu ya wasomi wa kiafrika huko Mali hadi leo yapo na wasomi wa zama hizi wanaextract information na kuandika vitabu.

Jiulize swali kuwa kabla ya wazungu kufika afrika watu hakuwapo!? Kama walikuwapo na palikuwa na mifumo ya kitawala, je! Hapakuwa na kumbumbuku zilizosaidia hii mifumo kujiendesha?
 
Kwa mfano ukifuatilia Biblia utagundua kuwa maandiko mengi yamebasr eneo la mashariki ya kati. Je! Asia, Africa ukiacha na Misri na Ethiopia ambazo zipo karibu na Mashariki ya kati, pia Amerika yote hazikuwapo?

Kuna Jamii kama Wa-Aztec huko Mexico na Indians ambazo zina historia ya mamilioni ya miaka alafu unaambiwa Christopher Columbus ndio aligundua bara la Amerika. Mimi nadhani ukitaka kumtawala mtu ni muhimu kumsahaulisha asili yake ndo mana Afrika tupo weak sababu hatujui tulitoka wapi, tulikuwa na knowpedge kiasi gani, na nguvu kiasi gani?

Hapo ndipo mzungu alituweza na bado atatuweza hadi tutakapo kumbuka sisi ni nani? Hii inaitwa mental slavery kina Bob Marley na Burning spear na wanaharakati kibao wenye asili ya afrika wamezungumzia.
 
Mtumwa hana historia. Usemi huu unaakisiwa kwa namna nyingi.

Nitaanza na utambulisho wa mtu katika jamii yake.

Huwezi kwenda mfano Ujerumani ukakuta mtu asiye Mmakonde akawa na jina la Chakumwenda Chipumbu. Utakuwa wajerumani wana majina yao asilia. Cha ajabu ukienda Songea utakutana na Mgoni anaitwa Otto Reinhardt.

Twende visiwa vya Karibian huko Jaimaica. Utakutana na kina Campbell kibao ilhali wao ni weusi titii hawana jina la Mandingo. Ukiwachunguza utabaini kina Campbell wa Jamaica walikuwa watumwa wa bwana Campbell mscotishi yaliyekuwa na mashamba makubwa ya miwa kisiwani Jamaica. Na kila aliponunua watumwa aliwapa jina la ubini la Campbell kwa lazima ili watambiluke ni mali ya bwana mkubwa Campbell.

Sisi huku Afrika ambao tulibahatika babu zetu kutokamatwa na kupeleka utumwani, tumekubali kupoteza majina yetu ya kujitambulisha koo na sehemu zetu za asili bila kucharazwa bakora wala kuwa chini ya utumwa.

Tumekubali kupoteza asili, majina ya ukoo, simulizi za mdomo, majina ya mashujaa, majina ya watabiri wa jadi, tiba-asilia, elimu jadi ya utunzaji ardhi/ kilimo/ mifugo / misitu /uvuvi, dini za asili , tamaduni, stadi za kuishi ktk mazingira yetu n.k kwa kuaminishwa kuwa lazima tuingie katika dini za kuja kwa majahazi na merikebu toka mbali.

Inasikitisha leo hii hatujui majina ya wahenga wetu, miti tuliyokuwa tunakwenda kuweka kafara zetu za jadi, Mahoka, Masika Zolelanga, Mulungu n.k Tunakaririsha Miungu na Mitume ya mbali na kwetu iliyotumika katika mazingira na historia tofauti na ya mababu zetu.

Sifa moja ya mtumwa ni kukosa historia ya asili yake katika kila hali, huku tukidanganyana kuwa mkataa kwao ni mtumwa wakati kiukweli sisi sote tumeshakataa 'kwetu' ingawa tunadanganyana kuwa tuna kwetu na huwa tunajitahidi kuutembelea kila tunapoweza vijijini, wilayani na mikoa tunayotoka.
Kweli kabisa mkuu, ndio maana na mimi niaongezea hapo ili kumtawala mtu inabidi asili yake uipoteze, asahau lugha, ufahamu wake wa mambo na uwezo wake n.k. Ndio kilichofanyika Afrika.
 
Unakumbuka hasara za kuhifadhi historia kwa Matumizi ya Mdomo../Kurithishana historia kwa njia ya masumilizi toka kizazi kimoja kwenda kingine...

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Ndio mkuu, ingawa kuna sehemu hadi leo hii unaweza kupata historia ya maelfu ya miaka kutokana na utamaduni huo. Kwa mfano David Haeley kwenye kitabu cha Roots alipata taarifa kutoka kwa Grauts wa kabila la Mandinka huko Gambia ambao walirithi hadithi kutoka vizazi na vizazi.
 
... unlike jamii za Ulaya na Far & Middle East ambao wamekuwa na permanent settlements for centuries, jamii nyingi za kiafrika zimekuwa zikihamahama until the recent past ndio angalau zime-settle permanently. Katika mazingira ya kuhamahama ni vigumu sana kutunza historia!

Kwa mfano, Roma ilijengwa mwaka 740 K.K. means the Romans by then (2761 years ago) walishakuwa na permanent settlements wakati leo hii Afrika bado kuna jamii zinahamahama maporini huko! Hivi maporini unatunza wapi historia?
tuseme wazee wetu walikuwa akili ya kuandika story hawana
 
Kile kitendo cha machifu kukubali na kuwapokea wageni na kukubali kuwa sisi hatukuwa na kitu chocho vyote vyetu ni vya kishenzi na sisi ni washenzi ndiyo lilipoanza tatizo
ndo maana wazungu wana tyambia tulikuwa manyani kwa kuwa hajui back ground yetu
 
Kwa mfano ukifuatilia Biblia utagundua kuwa maandiko mengi yamebasr eneo la mashariki ya kati. Je! Asia, Africa ukiacha na Misri na Ethiopia ambazo zipo karibu na Mashariki ya kati, pia Amerika yote hazikuwapo? Kuna Jamii kama Wa-Aztec huko Mexico na Indians ambazo zina historia ya mamilioni ya miaka alafu unaambiwa Christopher Columbus ndio aligundua bara la Amerika. Mimi nadhani ukitaka kumtawala mtu ni muhimu kumsahaulisha asili yake ndo mana Afrika tupo weak sababu hatujui tulitoka wapi, tulikuwa na knowpedge kiasi gani, na nguvu kiasi gani? Hapo ndipo mzungu alituweza na bado atatuweza hadi tutakapo kumbuka sisi ni nani? Hii inaitwa mental slavery kina Bob Marley na Burning spear na wanaharakati kibao wenye asili ya afrika wamezungumzia.
inawezekana kuwa wamechukua kumbu kumbu zetu
 
Iraq ina historia kuanzia 5000 BC na hata huyo mzee Ibrahim alitokea huko Ur kwenye bonde kati ya Tigris na Euprates. Je huyu alikuwa ni mzungu. Waliweza kuandika na kuchonga na kuumba vitu ambavyo mpaka sasa vipo.

Sisi ukikuta chombo alichotumia babu mzaa babu yako unakichoma na ndo maana hatuna historia. Miti iliyotumika kuabudia na kutolea sadaka ilishakatwa na hakuna kumbukumbu ya wapi tuliabudu.

Angalia magofu yaliyopo Kilwa baada ya miaka 100 yawezekana hayatakuwepo na tutasema tulitawaliwa na wazungu wakati mwarabu kaingia hapa kalne ya 10.

Hadithi za mapokeo tulizokuwa tunasimuliwa na wazee wakati wa jioni tukikoka moto au wakati wa mvua, siku hizi hakuna sababu wazazi wapo bize na smati foni.

Waafrika hatukuwa na maandishi ila michoro. Waafrika ambao walikuwa na maandishi ni wahabeshi, wamisri ingawa wao walitumia michoro zaidi ya herufi. Sisi ilikuwa ni michoro ambayo hatukuweza kurithishwa hivyo haikuwekwa kwenye mapokeo.
Anza wewe, tulia na wanao kila jioni uwasimulie hadithi ulizorithishwa na wazazi wako au hata hekaya za Abunuasi.
inabidi sisi tutafute history zetu,wamechukua mafuvu ya machief zetu wameweka kwenye makumbusho yao
 
Kwa mfano ukifuatilia Biblia utagundua kuwa maandiko mengi yamebasr eneo la mashariki ya kati. Je! Asia, Africa ukiacha na Misri na Ethiopia ambazo zipo karibu na Mashariki ya kati, pia Amerika yote hazikuwapo? Kuna Jamii kama Wa-Aztec huko Mexico na Indians ambazo zina historia ya mamilioni ya miaka alafu unaambiwa Christopher Columbus ndio aligundua bara la Amerika. Mimi nadhani ukitaka kumtawala mtu ni muhimu kumsahaulisha asili yake ndo mana Afrika tupo weak sababu hatujui tulitoka wapi, tulikuwa na knowpedge kiasi gani, na nguvu kiasi gani? Hapo ndipo mzungu alituweza na bado atatuweza hadi tutakapo kumbuka sisi ni nani? Hii inaitwa mental slavery kina Bob Marley na Burning spear na wanaharakati kibao wenye asili ya afrika wamezungumzia.
hivi biblia ndo ilichochea tukatawaliwa
 
... unlike jamii za Ulaya na Far & Middle East ambao wamekuwa na permanent settlements for centuries, jamii nyingi za kiafrika zimekuwa zikihamahama until the recent past ndio angalau zime-settle permanently. Katika mazingira ya kuhamahama ni vigumu sana kutunza historia!

Kwa mfano, Roma ilijengwa mwaka 740 K.K. means the Romans by then (2761 years ago) walishakuwa na permanent settlements wakati leo hii Afrika bado kuna jamii zinahamahama maporini huko! Hivi maporini unatunza wapi historia?
misri walijengaje mapramid?basi waafrica tumechukuliwa technology kibao wamezificha ndo sasa hivi wanazitoa tunawasifu kumbe ndo zetu
 
Back
Top Bottom