Kwanini wazungu huwa hawali sana kama sisi Waafrika?

Wazungu wako 2 hao uliokutana nao ndio uje kututolea mfano hapa?

40% ya wamarekani ni overweight na obese kutokana na kula hovyo na ulaji usiopangiliwa na inakadiriwa kufikia 2030 60% ya wamarekani watakua overweight kutokana na kula hovyo wewe unasema wazungu hawali sana? Kwa hiyo overweight wameitoa mbinguni?

Ukiangalia mataifa na watu walionenepeana hovyo Duniani utakuja kutuweka sisi waafrika na kula yetu ya hovyo unayoisema?

Shuleni mnasoma nini siku hizi? Yaani sample size ya watu 2 tayari ushafanya conclusion? Aisee.
Wale waliovimbiwa sio wazungu bana ni hao Wapopo wanafakamia junk food tu mtaani maana ni cheap.
Mzungu hasa hali hizo taka.
 
Usiwaite "wazungu" hao ni watu tu kama wewe, hili neno ni moja ya kitu kinachomfanya mwafrika amuone mzungu kama demigod.

Sio wote mkuu kuna watu wanakula kuliko unavyofikiria, hao wachache uliowaona haipaswi kuwa conclusion.
hii mindset ya kuona kila wanachofanya wao ni perfect ni mdudu kwenye kichwa cha mwafrika.

Hawa jamaa kutokana na uchumi wao inapelekea kula kila muda wanapojisikia, hivyo chakula kinakuwa kitu cha kawaida kwao.
Mostly hawana ile ya kula milo mitatu kwa siku kama sheria ya jeshi au masikini mweye shida au mtu aliyepitia maisha ya kuona chakula kama dhahabu.
Imagine kuna watu hawali siku nzima sasa mtu kama huyo unategemea acheke na sahani ya ugali?

So unategemea mtu anayekula na kunywa kila baada ya saa moja aweze kufukia ugali kilo mbili? Nah that's impossible.
Hata wewe jaribu uwe unakula, kunywa na kutafuna'tafuna kila unapojisikia tuone kama utaweza kufukia kilo ya ugali samaki, kwanza utakuwa ujisikii kula sana.

Na wanakuwa na afya sababu wanakuwa wameridhika, Hii sio wao tu bali kila mtu sababu wote ni binadamu tu.
 
Mind set...

Raised that way...

Discipline....

Ustaarabu....

Binadamu aliyefikia hatua ya kufanya kila kitu kwa kiasi ikiwemo chakula pia, ..... nashindwa kuelezea ila ni hatua flani ambayo wengine hawaiwezi.

Na inapendeza ikiwa self discipline.
Sawa kabisa, umemaliza
 
Wazungu wepi hao unawaelezea hapo unadhani wazungu wote wanafanana tabia zao?
Wazungu wanakula kiafya na kufuata taratbu za ulaji tofauti na waafarica
Utakuta mtu ana umri wa miaka 50,60,70 anakula milo 3 kwa siku sawasawa na Mtu wa umri wa miak 10,20
Mmeng’enyo wa chakula unapungua umri unapozidi kwenda na mwili wako lazima kuendana na mabadiliko ya chakula.
Kuna umri wa kula milo 3,2 na 1 kwa Siku ukiendana na kula matunda
 
Wazungu wanakula huenda hata kutuzidi. Say wao wanakula kidogokidogo (mara nyingi) wakati sie twala mara 1 kwa mkupuo.
 
Hao wazungu kwa taarifa yako mleta mada wanakula sana na ndio wanaongoza huko duniani kwa kuwa na uzito uliopitiliza, kuna kipindi huwa kinaonyeshwa Dstv wengi wao wanapunguzwa uzito kwa kufanyiwa upasuaji na unakuta ni vijana wadogo tuu.
 
Zungumzieni..vyotee lakini msigusiee pombee@m nmekaa na wazung..kwenye maishaa yang ckuwah kujua kitu kinaitwa starter....hyo starter wazungu wanayokulaa si waafrikaa humalizi...n mzigooo..@bt kwa kwel Kama alivosemaa mdau pale juu sisi waafrica tunakula Sana bt kwa Mara moja..
Wazungu nao wanakulaa Sanaa.bt.kwa intervals
 
nimekaa america, na kama kuna mtu anakudanganya kuwa wazungu hawali basi amekuingiza chaka. wanakulla sana ila kwa mara nyingi, depending on the type of activity wanayofanya, wengine wanaweza hata kula kuku mzima peke yake. vikombe vya chai hivi mnavyoviita huku kule kimoja sawa na hivi vya kwetu viwili. vidogo hakuna. kahawa unayokunywa wewe hapa kama kikombe kimoja kule ni mara mbili yake. wanakula kuliko sisi, ila sema sisi tunakula mataputapu mengi kwa uroho wa vyakula kwasababu hatunavyo vya kutosha ila wao wanakula kuliko sisi vyakula bora.
 
Tuwaite jina gani ukitoa hilo mzungu? Maana wao wenyewe hawachukii kuitwa hivo
Waite kutokana na wanapotoka kama ni Americans au Europeans.
Hii itafanya kusiwe na ile hali ya distinction ya mmoja kuwa superior na mmoja kuwa inferior bali kitakachowatofautisha hapo ni sehemu mnazotoka sababu wote ni binadamu tu.

Wewe unapomuita mmarekani "mzungu" huwa unajisikiaje?
Ni kama huyo mmarekani ni alien au demigod fulani hivi na sio binadamu kama wewe.
 
Huwezi kula kama unao uhakika wa kula.
Hata watoto wanaosumbua kula ni wale kwao mambo safi uhakika.
Watoto wasiosumbua kula ni wale wasio na uhakika wa kula,sahani wanafuta.
Nafkiri chakula ni kitu cha bei rahisi sana hapo nyumbani.
Kwetu uporoto huko unapata kabeji,ndizi ,viazi,matakapela,miwa,kila kitu buree mpk vinaoza.
Acha matunda .
Samaki wewe tu unaenda kuvua mwenyewe.
Ukitaka kuku au nyama vipo.
Ila ni Anasa na km una hela.
Chakula kipo 24 /7 upenuni tu hapo.
EnzI zetu tunapika bonge la ugali na mahomeboy alafu unaenda nyuma ya nyumba mnachukua maparachichi mawili makubwa kama kichwa cha mtu mnayatawanya mnagonga ugali mpk unaisha.
Chumvi tu km ipo.alafu mnaenda kupiga ball mmeshiba haswa
 
S
Wazungu wako 2 hao uliokutana nao ndio uje kututolea mfano hapa?

40% ya wamarekani ni overweight na obese kutokana na kula hovyo na ulaji usiopangiliwa na inakadiriwa kufikia 2030 60% ya wamarekani watakua overweight kutokana na kula hovyo wewe unasema wazungu hawali sana? Kwa hiyo overweight wameitoa mbinguni?

Ukiangalia mataifa na watu walionenepeana hovyo Duniani utakuja kutuweka sisi waafrika na kula yetu ya hovyo unayoisema?

Shuleni mnasoma nini siku hizi? Yaani sample size ya watu 2 tayari ushafanya conclusion? Aisee.
sijui aliona wazungu wa Czech? Au jamaa hajui wazungu aliona Wanepal akadhani ni wazungu! Nimefanyakazi na Wamarekani, Waholanzi wanapiga menu kama hawana akili nzuri, masaa yote wanatafuna tu!
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom