Kwanini Mzee Malecela alijulikana ghafla kama “Jumanne”?

Kwenye mkutano mkuu wa ccm kwa ajili ya kupitisha jina la mgombea urais 1995 Pale idodomya inasemekana Mzee Mchonga alionyesha msuli wake na kumtaka John Malecela aondoe jina lake kwenye nafasi ya kugombea urais. Kama hataondoa yeye Mwalimu MwanaCCM kwenye kadi #1 angerudisha kadi take ya chama na kujiondoa ccm.

John hazkuwa na lakufanya zaidi ya kuondoa jina lake na mwisho mzee wa Lupaso R I P akaibuka kidedea.

Hii ya kubadili jina na kujiita Jay4 ilisambaa Sana. Ila naamini ilikuwa ni uzushi
 
Katika historia tunaelezwa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. John Malecela aliitwa na mwalimu akamwambia anafaa kuwa Rais hivyo ajiandae. Inasemekana baada ya kuambiwa hivyo na mwalimu kwanza John alimweleza mkewe na alipofanya ziara nchini Iran alimweleza Mfalme kuwa anatarajia kuwa Rais wa Tanzania na hapohapo akapewa jina la Jumanne.

Kama mnavojua Iran ni nchi ya kiislam. Inasemekana baada ya kufika Tanzania kutoka ziara mwalimu alimfukuza akaenda kujificha kijijini kwao kongwa. Je, kuna ukweli wowote kuhusu hili?

Naamini hapa JF kuna watu wazima waliokuwepo kipindi hicho tunaomba mtueleze ukweli wa jambo hili. Je ni kweli?

Nawasilisha.
Like a father like a son. Hips don't lie
 
Shukrani kwa maelekezo yako mkuu.
 
Ahsante kwa kunielewesha mkuu. Kwanini umesema Malecela hakuwa na haiba ya kuwa Rais wa Tanzania?

Muvi nyingine nzuri alikuja kuchezewa na BWM 2005 Chimwaga(Kabla haijawa Chuo Kikuu)

Aliingia ukumbini kwenye kujieleza akakuta BWM kakaa halafu siti ya pembeni yake tupu.

Akaulizwa wewe cheo chako no nani ndani ya CCM akasema Makamu Mwenyekiti

Akaambiwa njoo ukae hapa tupitishe wagombea. Ndo ikawa imetoka hiyo
Ukabakia mchezo wa kina JK na SAS na JK akapenya

Kuhusu kwanini haikuwezekana na hana haiba hiyo ni stori ya siku nyingine.

Natamani tu naye aandike kitabu aisee kabla Mungu hajampenda zaidi. Sijui kwanini viongozi wetu hawaandiki historia zao wenyewe wakiwa hai.

JK yuko anaandika autobiography yake tayari
 
Kwenye mkutano mkuu wa ccm kwa ajili ya kupitisha jina la mgombea urais 1995 Pale idodomya inasemekana Mzee Mchonga alionyesha msuli wake na kumtaka John Malecela aondoe jina lake kwenye nafasi ya kugombea urais. Kama hataondoa yeye Mwalimu MwanaCCM kwenye kadi #1 angerudisha kadi take ya chama na kujiondoa ccm.

John hazkuwa na lakufanya zaidi ya kuondoa jina lake na mwisho mzee wa Lupaso R I P akaibuka kidedea.

Hii ya kubadili jina na kujiita Jay4 ilisambaa Sana. Ila naamini ilikuwa ni uzushi
Sasa umeeleza tu kuwa alivyolazimishwa kujitoa bila kueleza sababu ni nini.
 
Muvi nyingine nzuri alikuja kuchezewa na BWM 2005 Chimwaga(Kabla haijawa Chuo Kikuu)

Aliingia ukumbini kwenye kujieleza akakuta BWM kakaa halafu siti ya pembeni yake tupu.

Akaulizwa wewe cheo chako no nani ndani ya CCM akasema Makamu Mwenyekiti

Akaambiwa njoo ukae hapa tupitishe wagombea. Ndo ikawa imetoka hiyo
Ukabakia mchezo wa kina JK na SAS na JK akapenya

Kuhusu kwanini haikuwezekana na hana haiba hiyo ni stori ya siku nyingine.

Natamani tu naye aandike kitabu aisee kabla Mungu hajampenda zaidi. Sijui kwanini viongozi wetu hawaandiki historia zao wenyewe wakiwa hai.

JK yuko anaandika autobiography yake tayari
Hahaha umafia Wa vyeo ulianza kitambo sana kumbe
 
Kwanza Malecela kwao sio Kongwa acha uongo. Kwao ni Mvumi

Pili ni kweli "inasemekana" alisilimishwa na kuwa muislam ili apewe hela za kampeni na Jina alilopewa ni hill Jumanne

Tatu, katika uchaguzi wa 1995 hakuna aliyekua na nguvu kumshinda Malecele(Chigweyemisi) kwao ndo wanamuita hivyo kimeanguka mchana sijui kwanini

Nne, bila msuli wa mwalimu hata ule mpambano wa Mkapa na Kikwete usingetokea Malecela angeshinda mapema sana

Tano, Hakua na haiba wala uwezo wa kuwa Rais kwa mtazamo wangu. Na Nyerere alifanya vizuri sana kumblock
Umemaliza kila Kitu Ndugu na nitashangaa tena kuona Mjadala ukiendelea.
 
Katika historia tunaelezwa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. John Malecela aliitwa na mwalimu akamwambia anafaa kuwa Rais hivyo ajiandae. Inasemekana baada ya kuambiwa hivyo na mwalimu kwanza John alimweleza mkewe na alipofanya ziara nchini Iran alimweleza Mfalme kuwa anatarajia kuwa Rais wa Tanzania na hapohapo akapewa jina la Jumanne.

Kama mnavojua Iran ni nchi ya kiislam. Inasemekana baada ya kufika Tanzania kutoka ziara mwalimu alimfukuza akaenda kujificha kijijini kwao kongwa. Je, kuna ukweli wowote kuhusu hili?

Naamini hapa JF kuna watu wazima waliokuwepo kipindi hicho tunaomba mtueleze ukweli wa jambo hili. Je ni kweli?

Nawasilisha.
Wewe utakua chadema maana ndio waomini wa uongo na uzushia 😂😂
 
Malecela alikuwa mtu wa watu,na pale alipoteuliwa kuwa waziri wa kigeni alijiogezea umaarufu kisiasa.Kwani kabla ya pale foreign ministry ilikuwa chini ya Raisi Nyerere.

Lakini hakudumu,Mwalimu akampangia wizara nyingine.

Lakini mdomo ulikuja mponza akiwa waziri wa uchukuzi , wasafiri wa gari moshi walimfuata ofisini kwake wakiwa na jaziba baada kukosa usafiri wa train kwenda bara reli ya kati kwa kipindi kirefu.Akawajibu kwa kimombo go to hell.

Kama nuksi magazeti ya umma yalizipa kipaumbele matamshi yake,kama sikosei alikuja ondolewa uwaziri na kuwa balozi wetu Uingereza.

Lakini kitendo cha Raisi Mwinyi kumteua kuwa waziri mkuu kilimuudhi Raisi Mstaafu Mwalimu Nyerere. Kwani ndipo wabunge G45 wakiongozwa na akina Njeru Kasaka,Kinyondo,Jenerali Ulimwengu walipofaulu kupitisha mswaada wa serikali tatu.

Sio hilo tu Mwalimu Nyerere alidai Malecela ameshindwa kumshauri vizuri Rais Mwinyi maswala mbali mbali.Kama haitoshi akamtungia kitabu.

Yawezekana jina la Jumanne ilikuwa ni majungu tu katika kumnyima uraisi.
 
Back
Top Bottom