Kwanini Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela aliitwa ‘Jumanne’?

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,680
2,000
Katika historia tunaelezwa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. John Malecela aliitwa na mwalimu akamwambia anafaa kuwa Rais hivyo ajiandae. Inasemekana baada ya kuambiwa hivyo na mwalimu kwanza John alimweleza mkewe na alipofanya ziara nchini Iran alimweleza Mfalme kuwa anatarajia kuwa Rais wa Tanzania na hapohapo akapewa jina la Jumanne.

Kama mnavojua Iran ni nchi ya kiislam. Inasemekana baada ya kufika Tanzania kutoka ziara mwalimu alimfukuza akaenda kujificha kijijini kwao kongwa. Je, kuna ukweli wowote kuhusu hili?

Naamini hapa JF kuna watu wazima waliokuwepo kipindi hicho tunaomba mtueleze ukweli wa jambo hili. Je ni kweli?

Nawasilisha.
 
GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
4,117
2,000
Kwanza Malecela kwao sio Kongwa acha uongo. Kwao ni Mvumi

Pili ni kweli "inasemekana" alisilimishwa na kuwa muislam ili apewe hela za kampeni na Jina alilopewa ni hill Jumanne

Tatu, katika uchaguzi wa 1995 hakuna aliyekua na nguvu kumshinda Malecele(Chigweyemisi) kwao ndo wanamuita hivyo kimeanguka mchana sijui kwanini

Nne, bila msuli wa mwalimu hata ule mpambano wa Mkapa na Kikwete usingetokea Malecela angeshinda mapema sana

Tano, Hakua na haiba wala uwezo wa kuwa Rais kwa mtazamo wangu. Na Nyerere alifanya vizuri sana kumblock
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
42,209
2,000
Hujaelewa

Malecela alikuwa waziri wa kawaida wakati wa Nyerere ..
Nyerere alipanga kumpa uwaziri mkuu
Ndo inadaiwa akafanya Sherehe nyumbani kwake kabla ya kuteuliwa
Nyerere aka cancel uteuzi..

Hivyo hakufukuzwa cheo chochote
Ila alipewa uteuzi mwingine

Wakati Mwinyi anakuwa Rais ..
Wapambe wakamshauri Ampe Malecela uwaziri mkuu
Main reason watu walitaka wapate watu
Ambao sio vibaraka wa Nyerere

Nyerere bado alionekana anaingilia urais wa Mwinyi.. kwahiyo Kumteua Malecela kum replace Warioba ilikuwa ideal kuwa anaondoka kibaraka wa Nyerere (Warioba)
Anakuja mtu aliepishana na Nyerere huko zamani...

Jina la Jumanne alizushiwa wakati anataka kuwa Rais..alizushiwa na wapinzani wake kuwa kabadili dini ili Mwinyi ampendelee Urais na apate pesa za nchi za kiisalam zimsaidie kampeni..

Ukweli hakubadili dini..maadui zake walimpakazia..Ila alikuwa so powerful
Mpaka Nyerere akamlazimisha ajitoe kugombea urais ndo Mkapa akapita
 
Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
6,065
2,000
Kwenye mkutano mkuu wa ccm kwa ajili ya kupitisha jina la mgombea urais 1995 Pale idodomya inasemekana Mzee Mchonga alionyesha msuli wake na kumtaka John Malecela aondoe jina lake kwenye nafasi ya kugombea urais. Kama hataondoa yeye Mwalimu MwanaCCM kwenye kadi #1 angerudisha kadi take ya chama na kujiondoa ccm.

John hazkuwa na lakufanya zaidi ya kuondoa jina lake na mwisho mzee wa Lupaso R I P akaibuka kidedea.

Hii ya kubadili jina na kujiita Jay4 ilisambaa Sana. Ila naamini ilikuwa ni uzushi
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
57,684
2,000
Katika historia tunaelezwa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. John Malecela aliitwa na mwalimu akamwambia anafaa kuwa Rais hivyo ajiandae. Inasemekana baada ya kuambiwa hivyo na mwalimu kwanza John alimweleza mkewe na alipofanya ziara nchini Iran alimweleza Mfalme kuwa anatarajia kuwa Rais wa Tanzania na hapohapo akapewa jina la Jumanne.

Kama mnavojua Iran ni nchi ya kiislam. Inasemekana baada ya kufika Tanzania kutoka ziara mwalimu alimfukuza akaenda kujificha kijijini kwao kongwa. Je, kuna ukweli wowote kuhusu hili?

Naamini hapa JF kuna watu wazima waliokuwepo kipindi hicho tunaomba mtueleze ukweli wa jambo hili. Je ni kweli?

Nawasilisha.
Like a father like a son. Hips don't lie
 
Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,680
2,000
Kwenye mkutano mkuu wa ccm kwa ajili ya kupitisha jina la mgombea urais 1995 Pale idodomya inasemekana Mzee Mchonga alionyesha msuli wake na kumtaka John Malecela aondoe jina lake kwenye nafasi ya kugombea urais. Kama hataondoa yeye Mwalimu MwanaCCM kwenye kadi #1 angerudisha kadi take ya chama na kujiondoa ccm.

John hazkuwa na lakufanya zaidi ya kuondoa jina lake na mwisho mzee wa Lupaso R I P akaibuka kidedea.

Hii ya kubadili jina na kujiita Jay4 ilisambaa Sana. Ila naamini ilikuwa ni uzushi
Shukrani kwa maelekezo yako mkuu.
 
Ahsante kwa kunielewesha mkuu. Kwanini umesema Malecela hakuwa na haiba ya kuwa Rais wa Tanzania?

Muvi nyingine nzuri alikuja kuchezewa na BWM 2005 Chimwaga(Kabla haijawa Chuo Kikuu)

Aliingia ukumbini kwenye kujieleza akakuta BWM kakaa halafu siti ya pembeni yake tupu.

Akaulizwa wewe cheo chako no nani ndani ya CCM akasema Makamu Mwenyekiti

Akaambiwa njoo ukae hapa tupitishe wagombea. Ndo ikawa imetoka hiyo
Ukabakia mchezo wa kina JK na SAS na JK akapenya

Kuhusu kwanini haikuwezekana na hana haiba hiyo ni stori ya siku nyingine.

Natamani tu naye aandike kitabu aisee kabla Mungu hajampenda zaidi. Sijui kwanini viongozi wetu hawaandiki historia zao wenyewe wakiwa hai.

JK yuko anaandika autobiography yake tayari
 
FYATU

JF-Expert Member
Dec 7, 2011
5,366
2,000
Kwenye mkutano mkuu wa ccm kwa ajili ya kupitisha jina la mgombea urais 1995 Pale idodomya inasemekana Mzee Mchonga alionyesha msuli wake na kumtaka John Malecela aondoe jina lake kwenye nafasi ya kugombea urais. Kama hataondoa yeye Mwalimu MwanaCCM kwenye kadi #1 angerudisha kadi take ya chama na kujiondoa ccm.

John hazkuwa na lakufanya zaidi ya kuondoa jina lake na mwisho mzee wa Lupaso R I P akaibuka kidedea.

Hii ya kubadili jina na kujiita Jay4 ilisambaa Sana. Ila naamini ilikuwa ni uzushi
Sasa umeeleza tu kuwa alivyolazimishwa kujitoa bila kueleza sababu ni nini.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom