Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,988
Nimekaa tena na kuzungumza na kigogo wangu na safari hii tumejikuta na tatizo jingine at least ndivyo tulivyoliona tuko tayari kusahihishwa..
a. Waziri Mkuu anateuliwa na Rais na kupitishwa na Bunge. Waziri Mkuu anatoka miongoni mwa wabunge wa kuchaguliwa lakini hachaguliwi na Watanzania wote. Na hachaguliwi na Wabunge bali anateuliwa tu na Rais toka chama chenye wabunge wengi au anayeonekana kuungwa mkono na wabunge wengi.
b. Rais anaunda baraza la mawaziri baada ya kushauriana na Waziri Mkuu. Mapendekezo ya Waziri Mkuu au mashauri yake hayamfungi Rais kuunda baraza anavyotaka yeye. Katiba iko wazi kabisa kuwa katika utendaji wake Rais halazimishi kusikiliza ushauri wa mtu yeyote.
c. Mawaziri wanaapa mbele ya Rais na siyo mbele ya Waziri Mkuu na wanafanya kazi kwa kile kinachoitwa "ridhaa ya rais" a.k.a at the pleasure of the president. Mawaziri Wakuu kinidhamu na kiutendaji wanawajibika moja kwa moja kwa rais.
d. Mawaziri wanaongozwa na Waziri Mkuu katika utendaji kazi wa siku kwa siku na wanaweza kupewa maelezo na Waziri Mkuu. Lakini Waziri Mkuu hana uwezo wa kuwawajibisha. Hawezi kumfukuza Waziri au Naibu Waziri. Mwenye jukumu hilo ni Rais aliyewateua.
e. Waziri Mkuu akijiuzulu kwa kashfa au akifukuzwa kazi Baraza zima la Mawaziri LINAVUNJIKA AUTOMATICALLY. Sasa kama Baraza hakuliunda yeye, hakuliapisha yeye, na hana mamlaka ya kulisimamia kinidhamu au kiutendaji, kwanini baraza livunjike? Ninafahamu kwenye nchi kama Canada, Australia, Israel na Uingereza Mawaziri Wakuu ni watendaji - wanaunda mabaraza yao ya mawaziri na wana uwezo wa kuwawajibisha mawaziri walio chini yao hivyo wao wanapojiuzulu na mabaraza nayo yanavunjika. Sasa sisi wa kwetu:
a. Hajachaguliwa na wananchi
b. Haundi baraza la mawaziri
c. Hamwapishi Waziri hata mmoja - hakuna waziri anayeapa kumtii Waziri Mkuu
d. Hana uwezo wa kumfukuza au kumsimamisha Waziri
sasa kwanini yeye Waziri Mkuu akijuzulu baraza zima livunjike na kutuingiza katika mgogoro na gharama za kuunda baraza zima jipya wakati tatizo linawezekana kuwa lilikuwa ni la Waziri Mkuu tu? Kwa mfano baada ya baraza la mawaziri kuundwa siku chache zijazo ikatokea kuwa Waziri Mkuu hawezi kuendelea na kazi yake kwa sababu zinazotajwa kikatiba baraza lililoundwa tu LITAVUNJIKA NA Rais atatakiwa kupata Waziri Mkuu mwingine ambaye atashauriana naye na kuunda baraza jingine (laweza kuwa na mawaziri wote wale wale)
Kichwa kinauma.. i got to stop. Nahitaji kwenda vacation!! this is insane!!!