Kwanini Waziri Mkuu akifa/akijiuzulu Baraza la Mawaziri linavunjika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Waziri Mkuu akifa/akijiuzulu Baraza la Mawaziri linavunjika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 23, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nimekaa tena na kuzungumza na kigogo wangu na safari hii tumejikuta na tatizo jingine at least ndivyo tulivyoliona tuko tayari kusahihishwa..

  a. Waziri Mkuu anateuliwa na Rais na kupitishwa na Bunge. Waziri Mkuu anatoka miongoni mwa wabunge wa kuchaguliwa lakini hachaguliwi na Watanzania wote. Na hachaguliwi na Wabunge bali anateuliwa tu na Rais toka chama chenye wabunge wengi au anayeonekana kuungwa mkono na wabunge wengi.

  b. Rais anaunda baraza la mawaziri baada ya kushauriana na Waziri Mkuu. Mapendekezo ya Waziri Mkuu au mashauri yake hayamfungi Rais kuunda baraza anavyotaka yeye. Katiba iko wazi kabisa kuwa katika utendaji wake Rais halazimishi kusikiliza ushauri wa mtu yeyote.

  c. Mawaziri wanaapa mbele ya Rais na siyo mbele ya Waziri Mkuu na wanafanya kazi kwa kile kinachoitwa "ridhaa ya rais" a.k.a at the pleasure of the president. Mawaziri Wakuu kinidhamu na kiutendaji wanawajibika moja kwa moja kwa rais.

  d. Mawaziri wanaongozwa na Waziri Mkuu katika utendaji kazi wa siku kwa siku na wanaweza kupewa maelezo na Waziri Mkuu. Lakini Waziri Mkuu hana uwezo wa kuwawajibisha. Hawezi kumfukuza Waziri au Naibu Waziri. Mwenye jukumu hilo ni Rais aliyewateua.

  e. Waziri Mkuu akijiuzulu kwa kashfa au akifukuzwa kazi Baraza zima la Mawaziri LINAVUNJIKA AUTOMATICALLY. Sasa kama Baraza hakuliunda yeye, hakuliapisha yeye, na hana mamlaka ya kulisimamia kinidhamu au kiutendaji, kwanini baraza livunjike? Ninafahamu kwenye nchi kama Canada, Australia, Israel na Uingereza Mawaziri Wakuu ni watendaji - wanaunda mabaraza yao ya mawaziri na wana uwezo wa kuwawajibisha mawaziri walio chini yao hivyo wao wanapojiuzulu na mabaraza nayo yanavunjika. Sasa sisi wa kwetu:

  a. Hajachaguliwa na wananchi
  b. Haundi baraza la mawaziri
  c. Hamwapishi Waziri hata mmoja - hakuna waziri anayeapa kumtii Waziri Mkuu
  d. Hana uwezo wa kumfukuza au kumsimamisha Waziri


  sasa kwanini yeye Waziri Mkuu akijuzulu baraza zima livunjike na kutuingiza katika mgogoro na gharama za kuunda baraza zima jipya wakati tatizo linawezekana kuwa lilikuwa ni la Waziri Mkuu tu? Kwa mfano baada ya baraza la mawaziri kuundwa siku chache zijazo ikatokea kuwa Waziri Mkuu hawezi kuendelea na kazi yake kwa sababu zinazotajwa kikatiba baraza lililoundwa tu LITAVUNJIKA NA Rais atatakiwa kupata Waziri Mkuu mwingine ambaye atashauriana naye na kuunda baraza jingine (laweza kuwa na mawaziri wote wale wale)

  Kichwa kinauma.. i got to stop. Nahitaji kwenda vacation!! this is insane!!!
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Pole Mwanakijiji. Namna hii ya kufikiri kwako, lazima kichwa kikuume.

  Aya (b).

  Kwa hiyo Pinda (Mh. Mizengo) akisema Mama Zakia Meghji hafai kupewa uwaziri panaweza kuchimbika? Hii nilikuwa sijui.

  Kwenye hitimisho:
  Kama mawaziri wanaripoti kwa rais na hawana uchafu wowote. Ni wasafi. Bahati mbaya kiranja wao kalikoroga yeye kama yeye, kuna haja gani ya kuvunja Baraza la Mawaziri? Hapo hata mimi sielewi.

  Bora kusiwe na Cheo cha Rais, au Rais awe na madaraka madogo tu kama ilivyo Ujerumani.
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yote yamo ndani ya katiba
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Da! Mwanakijiji nakuhurumia sana.
  Nakuhurumia kwa kujibebesha mzigo wa maswali magumu.
  Katiba sio Msahafu wala Biblia na kwa bahati nzuri hili hata viongozi wanaong'ang'ania isibadilishwe wanalijua.
  Hivyo basi yapo mafungufu mengi mno.
  Anyway. SIna jibu la swali lako na mimi pia nina kaswali.
  Je, Waziri anapotimuliwa au kutoendelea na madaraka yake, kwanini naibu waziri(wa wizara hiyo) yeye huendelea tu na cheo chake?
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji inawezekana wewe ni nabii ........ na uwezo wako wa kufikiri hata sangoma hafikii
   
 6. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kaka nakupongeza kwa ili, katiba yetu imejaa takataka nyingi sana kiasi kuwa kuisafisha haitawezekana ni bora tukatengeneza mpya.

  Tunahitaji kuwa na katiba mpya itakayopitishwa na wananchi wote ambayo itaondoa matatizo yote tuliyonayo, tunahitaji Rais aingie bungeni mwenyewe badala ya waziri mkuu. ili kosa wamelirudia tena kwenye marekebisho ya zanzibar hakukutakiwa kuwa na makamu wa pili mtendaji, ilitakiwa rais aende mwenyewe bungeni
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Nov 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Haya maswali kwa kweli yote si ya kwangu.. si unajua mnaweza kuwa mnapiga stori na marafiki na mjadala ukanoga halafu wote mkabakia na "sijui". Huyu bwana ambaye ninamheshimu amenirushia maswali ambayo kwa kweli yamenifanya na miye niwarushie na nyie vile vile. Nina uhakika kuna watu wengine wengi tu wanajiuliza maswali haya haya..
   
 8. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2010
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  hivi sehemu gani (website) ambayo ninaweza kupata katiba ya tanzania?
   
 9. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Tatizo la kutegemea KATIBA kinyonga...
   
 10. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  assume kuwa pm anachaguliwa na wananchi wote*wengi* kwa kigezo cha kwamba amepigiwa kura na wabunge waliochaguliwa na wananchi kuwawakilisha.
  Itabaki kuwa waziri mkuu amechaguliwa na wananchi kama ambavyo rais amechaguliwa lakini hii kwa namna nyingine.
  Off topic qn.
  Baada ya kusuluhisha mgogo uliosababishwa na uchaguzi nchini kenya,kikwete alisema raila atakuwa waziri mkuu mwenye mamlaka kama ya pm wa tanzania lakini pm wa tz anamzidi kidogo.
  Tofauti ya pm wa tz na wa kenya ni ipi kiutendaji?
   
Loading...